Kujenga au kupata nyumba kwa mortgage

davetz28

JF-Expert Member
Dec 17, 2017
543
617
Niliwahi kuja na hoja ya ujenzi wa nyumba kwa shilingi 25000000/ milioni ishirini na tano kwa Dar na ikaonekana kuwa siwezi kupata nyumba ya kisasa.

Leo nimekuja na wazo la kujenga au kupata nyumba kwa mortgage, utaratibu wa kununua nyumba au kukopa pesa ya nyumba kwa mfumo huohuo na marejesho ya muda mrefu.

Binafsi nimependa kupewa pesa kwa awamu kupitia mkopo huo kuliko kukopa nyumba na marejesho hadi miaka kumi na tano.

Nimekuja hapa kupata uzoefu waliowahi kupata nyumba kwa utaratibu huu na maoni kwa ujumla kwa wanajukwaa wengine.

Napenda kupata nyumba ikiwa imekamilika kuliko kujenga nusunusu.

Karibu kwa ushauri wenu
 
Ukipata nyumba ya mil 70 utarejesha kiasi kisichopungua laki 9 kwa mwezi na mpaka unamaliza utakua umelipa takriban mil 210. Fika bank kwa maelezo zaidi.
 
nunua kiwanja kajenge ata chumba kimoja kama unaham ya kua kwako Utajishukuru baadae. ila sio mkopo wa nyumba
 
Ukipata nyumba ya mil 70 utarejesha kiasi kisichopungua laki 9 kwa mwezi na mpaka unamaliza utakua umelipa takriban mil 210. Fika bank kwa maelezo zaidi.
Bp kama mahitaji yangu ni mil 45000000 na sio hiyo 70 mil?
 
Back
Top Bottom