Kuitwa kwenye Usaili: Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)

Hazchem plate

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
11,045
15,380
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 6, 8, 9, na 10 Aprili, 2019 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
  • Usaili wa Vitendo utafanyika tarehe 8 na 9 Aprili , 2019 na usaili wa mahojiano kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu usaili ambapo utafanyika umeainishwa kwa Kada husika ;
  • Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
  • Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, Kidato cha VI, Vyeti vya mafunzo ya Udereva, leseni ya udereva na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji kwa kada hii.
  • Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI, (ISIPOKUWA WAOMBAJI WALIOHITIMU MWAKA 2018)
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA); na Waombaji kazi ambao majina yao hayaonekani katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi
Ili kuona orodha ya Walioitwa kwenye Usaili, tafadhali soma >>>
 

Attachments

  • TANGAZO-LA-KUITWA-KWENYE-USAILI-NGORONGORO..pdf
    1.3 MB · Views: 214
Rejea kichwa cha habari.
Pakua PDFView attachment 1060201

Siyakukothamela Sonini na nini
Shukrani sana kwa taarifa yako,nilihisi tu yakuwa mwezi wangetoa na kweli wametoa,nashukuru nami nipo katika kuitwa kwenye Usaili,ila kuna kimoja ambacho nakifiria kuna sifa mojawapo ya kigezo sina ni kile chakuwa na Leseni ya Udereva hapo sijui mnanishaurije jamani
 
Ivi mfano katika ile post walisema uwe na leseni ya udereva na ukawa huna sijui inakuwaje hapo
 
Shukrani sana kwa taarifa yako,nilihisi tu yakuwa mwezi wangetoa na kweli wametoa,nashukuru nami nipo katika kuitwa kwenye Usaili,ila kuna kimoja ambacho nakifiria kuna sifa mojawapo ya kigezo sina ni kile chakuwa na Leseni ya Udereva hapo sijui mnanishaurije jamani
Kama huna leseni kwa nafasi ya udereva usijisumbue kwenda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom