Mambo ya kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili

Nov 15, 2022
25
142
Tutakuwa na zoezi la Usaili wa TRA kwa nafasi mbalimbali kuanzia tarehe 17 Disemba mpaka tarehe 08 Januari, 2023.

Usaili Huu utafanyika katika kanda nne ambazo zimegawanywa katika mikoa ya Dodoma (CHUO KIKUU CHA DODOMA UDOM), Dar es Salaam (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Kigamboni, Mbeya (Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) na Mwanza (Chuo Kikuu cha Mtakitifu Agustino (SAUT).

Wasailiwa wete mlioitwa kwenye Usaili mnapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
  1. Zingatia muda na sehemu uliyopangiwa kwa ajilli ya Kufanya Usaili.
  2. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na Vitendo, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi;
  3. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;
  4. Wasailiwa wenye majina yanayotofautiana katika nyaraka zao wahakikishe wanafika na kiapo cha majina (Affidavit) au hati ya usajili wa majina (Deedpoll);
  5. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  6. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa mtaa/Kijiji unakoishi;
  7. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
  8. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
  9. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
  10. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
  11. Kwawaombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
  12. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni zakufanyia kazi.
  13. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usail.
 
Ahsante sana mkandaji kwa taarifa.

Ni matumaini yangu kila mmoja atazingatia haya maelezo na kuepusha usumbufu wa kuvutana siku ya usahili
 
Tutakuwa na zoezi la Usaili wa TRA kwa nafasi mbalimbali kuanzia tarehe 17 Disemba mpaka tarehe 08 Januari, 2023.
Usaili Huu utafanyika katika kanda nne ambazo zimegawanywa katika mikoa ya Dodoma (CHUO KIKUU CHA DODOMA UDOM), Dar es Salaam (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) Kigamboni, Mbeya (Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST) na Mwanza (Chuo Kikuu cha Mtakitifu Agustino (SAUT).
Wasailiwa wete mlioitwa kwenye Usaili mnapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
  1. Zingatia muda na sehemu uliyopangiwa kwa ajilli ya Kufanya Usaili.
  2. Kila Msailiwa anapaswa kunukuu kwa usahihi namba yake ya usaili wa mchujo na Vitendo, namba hizo zinapatikana kwenye akaunti ya kila Msailiwa katika mfumo wa maombi ya kazi;
  3. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa;
  4. Wasailiwa wenye majina yanayotofautiana katika nyaraka zao wahakikishe wanafika na kiapo cha majina (Affidavit) au hati ya usajili wa majina (Deedpoll);
  5. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  6. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria au barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa mtaa/Kijiji unakoishi;
  7. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
  8. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
  9. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
  10. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
  11. Kwawaombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
  12. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni zakufanyia kazi.
  13. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili

Samahani Mkuu, naona ndugu zetu wanaofanyia Zanzibar haujawagusa kabisa, ni makosa madogo ya kiuandishi au kwa wao ratiba imebadilika?
 
Back
Top Bottom