Kuitwa kwenye usaili jubilee insurance

Feb 13, 2017
77
40
Habari za mda huu wakubwa. Natumaini ni wakheri wa afya,

Mimi kijana mtanzania nina umri wa miaka 25, na elimu yangu ni stashahada kwa fani ya maendeleo jamii.

Leo mchana nilipigiwa simu ya usaili kwa nafasi ya sales agent kwa kampuni ya bima jubilee insurance. Sasa ombi langu naomba kujuwa kwamba viwango vyao vya mshahara na commission vipoje.. Asanteni
 
tafuta buti kubwa lenye soli pana la kutembelea ofisi kwa ofisi, nlidhani ungeuliza maswali ya interview yanakuaje na majibu au ufanyaje upite kwenye interview!!
 
Maswali ya kawaida mno plus hawazingatii interview utapitishwa na kupewa training sababu wanahitaji agents sababu waliitisha Miezi miwili iliyopita ila watu waliacha hivyo wameitisha tena.
Uwe fundi wa kuongea na kukatiza mitaa na office.
 
yaani kiufupi unakuwa dalali wao, kwa lugha nyingine unaitwa insurance broker, kama una mtaji unaweza kufungua ofisi yako ndogo ukawa wakala wa makampuni zote za bima, faida ya kuwa insurance broker ni kwamba ukipata mteja unaweza kumuuzia bima kutoka kampuni yeyote ya bima, na vile vile unaweza kutambua kampuni ipi ya bima wapo vizuri kwenye malipo ya commision na kwenye malipo ya madai. kwahiyo sales agent jiandae kwa kazi hizo
 
Nadhani kuna tofauti kati ya "insurance broaker", "insurance agent", na "insurance over-counter agent"

Huyu jamaa yeye anaangukia kwenye insurance over- counter agent. In short anakabidhiwa vitendea kazi tu kama vile form za premiums, form za kurekodi taarifa za potential clients na makaratasi mengine, etc. Hata kama atakuwa anaishi hewani sawa tu. Ila kazi apige. Jua lake, mvua yake, upepo wake, vumbi lake, njaa yake, kiu yake, jasho lake, kutukanwa na prospective clients kwa kuwatabiria kifo (mfano Jubilee life insurance) yeye etc etc etc....

Yaani yeye hatosajiliwa kama insurance agent.

Hao wengine lazima wawe registered na pia insurance broaker/ agent haruhusiwi kiwakilisha kampuni zaidi ya moja.

Correct me.
 
Mkuu hyo kaz inataka moyo sanaa watanzania wa sasa kuwashawish watumie jubilee insuarance hasa hzo products zao ni shida sanaa, but piga kazi
 
Hiyo shughuli haina tofauti na zile kazi za networking market, forex na forever living.
 
Nadhani kuna tofauti kati ya "insurance broaker", "insurance agent", na "insurance over-counter agent"

Huyu jamaa yeye anaangukia kwenye insurance over- counter agent. In short anakabidhiwa vitendea kazi tu kama vile form za premiums, form za kurekodi taarifa za potential clients na makaratasi mengine, etc. Hata kama atakuwa anaishi hewani sawa tu. Ila kazi apige. Jua lake, mvua yake, upepo wake, vumbi lake, njaa yake, kiu yake, jasho lake, kutukanwa na prospective clients kwa kuwatabiria kifo (mfano Jubilee life insurance) yeye etc etc etc....

Yaani yeye hatosajiliwa kama insurance agent.

Hao wengine lazima wawe registered na pia insurance broaker/ agent haruhusiwi kiwakilisha kampuni zaidi ya moja.

Correct me.
You are very correct.
Mimi ambayo naipenda ni hiyo ya kuwa agent.
Lakini nimesikia kwamba hawawezi kukupa Hadi uwe na experience kwenye kazi zao.
Yaani uwe ulipitia kuwa muajiriwa au insurance over-counter agent.
Je hii Ina ukweli wowote?
 
Back
Top Bottom