Kuitafuta faraja ya kudumu kwenye mahusiano ni sawa na kumtafuta paka mweusi kwenye kiza

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,522
Hii dunia si pepo kusema utaishi kwa raha siku zote na hii dunia si moto kusema kila siku utakuwa mwenye tabu tu kwenye mahusiano, kubwa kinachotakikana ni subra na uvumilivu wa hali ya juu, mahusiano mengi ili yadumu yanategemea sana uvumilivu wa mtoto wa kiume na ndomaana Mungu katupa koromelo lakuweza kustahamili mambo na vitimbi vya wanawake.

Ni jukumu letu kuwastahamilia kwa madhaifu mbali mbali walokuwa nayo, kimaumbile wako hivyo na hatuwezi kufanana japo na siye tunayetu nayo. Wengi wana maamuzi ya kukurupuka sana huwa hawafikilii sana mbali na niwepesi wakujuta mambo yanapokwenda mrama.

Mwanamke ametokana kwa ubavu uliopinda ukitumia nguvu sana kuunyoosha utauvunja na ukiuacha basi jua utapinda zaidi.

Akili kichwani mwako
 
Nyoka_mzee umeandika as if ni kitu rahisi sana! lakn sivyo! Sipingani na wewe kuwa dunia si pepo kwamba utaishi na furaha milele, lakn bro, mapenzi huwa yanaumiza pande zote, kuna kipindi mapezi huwa yana raha saana yaani unaweza ukiajiona kama malaika vile na yanapogeuka yanakuwa na maumivu makali saaana!
Wapo wanawakae hata umempende vipi hawezi kutambua thamani ya upendo wako kwake! usiombe yakukute
 
Mliambiwa muishi nasi kwa akili, hilo fumbo mkilifumbua baaaasi tatizo kwisha. Shida mtatumia nguvu na kutaka sisi ndio tutumie akili kuishi nanyi, rudini kwenye misingi mtupende nasi tutawatii.
kabisa kabisa ndo tunarudishana hivyo kwenye misingi
 
Mliambiwa muishi nasi kwa akili, hilo fumbo mkilifumbua baaaasi tatizo kwisha. Shida mtatumia nguvu na kutaka sisi ndio tutumie akili kuishi nanyi, rudini kwenye misingi mtupende nasi tutawatii.
Kwahio mnafanya kusudi,kwasababu tu eti tuliambiwa tuishi nanyi kwa akili?
 
mkuu katika maisha huwezi kila siku ukawa na furaha kila mahali changamoto zipo kubwa kuwa na subra huwa kuna vipindi vya mpito

Ni kweli usemavyo mkuu...ila muda mwingine ukiwa na subira, mwanamke anakuona hufai na kutoa maamuzi kwa kukurupuka ni jambo baya sana... Kwenye ndoa kuridhishana na kupeana faraja yataka moyo sana...

Anyways; Kulingana na maelezo yako inamaanisha Faraja kwenye ndoa haipatikani kwa % 100 ee?
 
Naam faraja kwenye mahusiano haiwezi kupatikana kwa asilimia mia
kubwa kuvumiliana tu mkuu na kustahamiliana katika hilo
 
Back
Top Bottom