Kuisifia na kuikosoa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuisifia na kuikosoa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mopaozi, Jun 8, 2011.

 1. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Natoa rai wakuu ianzishwe thread special huku JF ya kuipongeza na kuisifia serikali na nyingine ya kuikosoa serikali.

  Inanichanganya kuona kila post ina comments za kuiponda serikali ina maana hakuna mazuri yanayofanywa? Kama ni kweli basi hali ingekuwa mbaya sana kungekuwa na vita saa hizi kama Somalia, so tuache unafiki ukumbi wa kuipongeza serikali pia uwepo ili mazuri iliyotufanyia tuyaweke wazi na watu watume post zao huko.

  Mods wazitoe post za watu watakaoenda kinyume ktk post zao maana kila siku post ni za kuiua tu serikali khaaa!!!!!!!!! Hata Mungu anajua kuwa kuna mazuri yanayofanywa na atawahukumu kwa unafiki wetu tunaouonyesha kuwa hakuna jema hata moja lililofayiwa na serikali; yaani siku nzima post zinatumwa na watu juu ya kuiponda/kuichafua/kuizandiki/kuidhalilisha/kuishirangia/kuilaani/kuinyanyapaa serikali yao kana kwamba waliounda serikali ni machizi hawana akili hata moja hivi hii ni haki kweli!

  Wewe hapo uanashangaa nini wakati kutwa kutuma post za kuilaani serikali ya nchi yako..kama kusingelikuwa na mazuri we ungekuwa wapi saa hizi? Jiulize, naam jibu unalo!!
   
 2. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wazo zuri sana subiria vimeo uone watakavyo dharau wazo lako, hawa jamaa c wanalipwa kila wakiponda srikali? Viziwi, vpofu na mabubu. Foxy piga bastola
   
 3. j

  jakamoyo JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  umeonge point mkuu, ila watu wengine wana fikra mgando thats y kazi yao ni kuponda tu serikali. wanafikiri kukosoa kila wakati ndio kuwa great thinker kumbe wanakosea.
   
 4. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mazuri mengi sana mfano kumsafirisha Mh Mbowe kwa 50 million kwenda arusha halafu wasimulize swali hata moja?
   
 5. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,068
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Hakuna haja yakuwasifia nakuwapamba watawala,sisi ni waajiri wao na wakati wanaomba kazi kwa hiari yao walituhaidi maisha bora.

  Lakini baada ya kuanza kazi mambo yakwenda kinyume na matarajio ya wananchi maisha bora yamebaki kwenye takwimu tu vitabuni, ndio maana unaona tunahoji kulikoni inawezekana wewe ni wale wachache wanaofaidika na mfumo huu.

  Pamoja na hayo watawala wamejiwekea vyombo mbalimbali vyakuwapamba nakuwasifu hata pasipostahili sifa,ni wajuzi sana kwa hilo nadhani na wewe ulikuwa shahidi kwenye kampeini zao za uchaguzi.

  Waache watu wahoji watawala kwa nini hawatimizi ahadi zao.
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Sasa mkuu wangu,

  Nani afanye jukumu hili la 'kuitetea' serikali? Mazuri yakiwepo yanajionyesha.

  Unataka kusema JF hakuna hata sehemu serikali imepongezwa? Ume-search au umehisi tu?
   
Loading...