CCM yampongeza Rais Samia kwa kuelekezwa sheria kandamizi zianishwe na zifutwe

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi Wetu,
Tanga

Dunia na watanzania wameendelea kumheshimu na kumsema kwa mazuri Mwl Julius Kambarage Nyerere huku kila wakati jina akiwa midomoni na moyoni mwa watu ikiwa ni miaka 37 tangu ang'atuke madarakani na miaka 23 tangu afariki dunia. Hali inayotajwa kuwa tofauti kwa viongozi aina yake waliopigania uhuru wa mataifa yao katika nchi 54 barani Afrika.

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana wakati akiwahutubia viongozi na Wana-CCM wa mkoa wa Tanga kwenye mkutano wa ndani uliofanyika ukumbi wa Lembeni Korogwe Mjini mkoani Tanga alipokuwa kwa ziara ya siku moja y uimarishaji chama.

Kinana amesema ni Nchi za Tanzania na Afrika Kusini ndizo zimebaki na utamaduni wa kuwapa heshima hii viongozi wake waliopigania uhuru. Mwl Nyerere anafanyiwa haya yote kwa sababu enzi za uhai na uongozi wake kwa aliweza kufanya mambo yaliyogusa mioyo na maisha ya watu.

"Mwl Nyerere hakumbukwi kwa mambo yanayoonekana, husikii watu wakisema wanamkumbuka kwa sababu ya kujenga barabara au hospitali au shule bali wanamkumbuka kwa sababu alipigania utu, uhuru, usawa, uadilifu, heshima na haki."

Kinana alisisitiza kwamba mambo hayo aliyopigania Mwl Nyerere yamekuwa misingi imara ya Tanzania. Ambapo alisema wao kama CCM hawana budi kuendelea kuienzi.

"Nawasihi Wana-CCM wenzangu tumuenzi Mwl Nyerere kwa kuhimiza na kuishi maisha ya uadilifu, kukemea na kupinga rushwa za aina zote, kuweka mbele maslahi ya watu kuliko binafsi, kuwa watetezi wa haki za watu na kuacha utamaduni wa kuiogopa serikali kiasi cha kushindwa kuihoji au kuishauri pale inapohitajika kufanyika hivyo." Amesisitiza Kinana

Amewataka wana-CCM kuipongeza serikali pale inapostahili, kuikosoa na kuishauri pia pale inapohitajika. Kazi ya kusemea mafanikio ya utekelezaji wa ilani na mazuri yanayofanywa na serikali inapaswa kufanywa na kila mwanachama ili wananchi wajue na itaimarisha imani yao kwa chama na serikali yao.

Pia amesema CCM inampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake ya kutaka kila wizara nchini iainishe sheria zinazoonekana kuwa kandamizi ili zifutwe kwa lengo la kuwapa nafuu wananchi na kuchochea uwekezaji nchini.

Mwelekeo wa serikali ya CCM awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuimarisha uchumi na kuongeza kipato kwa wananchi wa kipato cha chini hususani wafanyabishara wadogo, machinga, bodaboda na waendesha bajaji kwa kuwawekea mazingira mazuri na wezeshi ya kufanya shughuli zao kwa uhuru na utulivu. Hivyo ndio maana Rais Samia ametoa maelekezo hayo ya kufutwa kwa sheria kandamizi.

"Ninawahakikishia kazi ya serikali za CCM ni kurahisisha mazingira ya ufanyaji shughuli za kiuchumi nchini ili wananchi wajitafutie kipato kwa uhuru na utulivu. Nawagiza madiwani na wabunge Nchi nzima msikubali kuwa sehemu ya kupitisha sheria ambazo wananchi wenu hawajashiriki kwa kutoa maoni yao. Kwa kufanya hivyo tutaepukana na utungaji wa sheria unao wakandamiza wananchi wetu."

Kinana alihitimisha kwa kusema serikali pekee haiwezi kuajiri kila mtu nchini bali inalo jukumu la msingi la kuweka mazingira mazuri na rafiki ili watu wake wajiajiri wenyewe na kuvutia wawekezaji wakubwa kuwekeza mitaji yao ili kuzalisha ajira zaidi kazi ambayo serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inafanya na amewahakikishia watanzania wataifanya kazi hiyo vizuri sana.

Ndg Kinana amehitimisha ziara yake mkoani Tanga ambapo yeye na msafara wake wameelekea Kilimanjaro kuendelea na ziara hiyo ya uimarishaji wa chama.

IMG-20220425-WA0102.jpg
IMG-20220425-WA0085.jpg
IMG-20220425-WA0089.jpg
IMG-20220425-WA0079.jpg
IMG-20220425-WA0060.jpg
IMG-20220425-WA0063.jpg
 
Kinana bana. Kuna mwana CCM mwadilifu na asiye fisadi?

Wamepata kiki ya kupambana na mwendazake kila wanapopata nafasi; utafikiri hakuwa mwanaCCM mwenzao. Kumbe wanaficha uozo uliojaa katika chama.

Kama ana ubavu si aongelee hatua za kinidhamu zitakazochukuliwa na chama dhidi ya ufisadi wa kinyama ulioanishwa katika ripoti ya CAG?




Screenshot_20220425-172953.jpg
tapatalk_1565855230907.jpg
 
kuna swali najiuliza sipati jibu

tangu baada ya uchaguzi wa 1995 Colonel Kinana hataki cheo chochote Serikalini…ila kwny Chama anakubali wakati wengine piga ua wanataka kuingia kwny serikali
 
Sheria ya Ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 nayo ni kandamizi mno kwa waajiri na waajiriwa pia...ianagaliwe vizuri.
 
CCM hawana jingine la kufanya zaidi ya kumpongeza mama kwa kuwa ametokana na CCM, ni kama vile walivyokuwa wanampongeza jambazi pamoja na ujambazi wake kwa kuwa alikuwa ni mtu wao.
 
Back
Top Bottom