Kama alivyosema Mapondela, sheria yetu ya Ndoa ya mwaka 1971 haitambui ndoa za mikataba, tafsiri ya ndoa iliyotolewa na mkuu hapo ni sahihi kabisa, lakini napenda kuongezea kitu kidogo ili watu waelewe vizuri, kuna kitu kinachoitwa dhana ya ndoa (pressumption of marriage) ambapo ili hii iweze kutumika ni lazima wahusika wawe wameishi pamoja kwa muda usiopungua miaka miwili na jamii yote inayowazunguka iwe imewajengea dhana kuwa wao ni wanandoa, matumizi ya dhana hii yanakosewa na wengi sana, baadhi ya watu wanafikiri kuwa ukikaa ma mwenzi wako kwa muda wa miaka miwili basi nyie ni wanandoa, haipo hivyo kwani ingelikuwa hivyo basi sheria ingekuwa inarasimisha mahusiano yasiyo rasmi, kifupi tu ni kwamba ili watu mtambulike kuwa ni wanandoa ni lazima mfunge ndoa inayotambulika kwa mujibu wa sheria za nchi.
Dhana hii ya ndoa huwa inatumika tu kumlinda mwenzi mmoja ili asipoteze haki yake ambayo angestahili kuipata kutokana na kuishi na huyo mwenzake kwa muda wote huo walioishi, kwa hiyo si ajabu mtu akaenda mahakamani na ku-base madai yake kwenye dhana ya ndoa na bado akashindwa madai yake.