Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

establishment

JF-Expert Member
Jun 27, 2015
1,630
2,380
Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa miaka 35 sasa, nimeoa mwaka wa 6 huu, na nina watoto wawili, ila ujumbe wangu wa leo vijana mnapoamua kuoa muwe mmemaanisha hawa wake zetu unahitaji akili ya ziada kuishi nao wengi wana upeo wa chini sana na wasahaulifu kupitiliza.

Hivyo kijana usipokuwa muelewa unaweza kuwa unagombana nao kwa sababu ambazo unaweza kuziepuka.

NB: Binafsi katika miaka hiyo ya ndoa nimejifunza na kushuhudia mengi upo wakati nilitaka kuachana na mke wangu kwa kelele zake na kutofuata ninachotaka mimi. Ila baadae nikaamua kumpotezea nimeamua kuwa kimya kama mjinga flani hivi ila akili kumkichwa

UPDATE: 22 Novemba 2016

Wake zetu tunawapenda sana ila mnaongea mno kupitiliza. Binafsi situmii kilevi, wala si mtu outgoing kivile isipokuwa mara chache nikiwa na pesa kidogo tunatafuta outing na familia ufukweni au nje ya mji Bagamoyo ama Lushoto au Arusha.

Lakini sasa huyu mke wangu yeye hataki nifanye kazi na mwanamke yeyote, duuh! Hili kwangu haliwezekani maana kwa kazi yangu nakutana na wengi (wanaume & wanawake).

Pia usafi chumbani ni ovyo ovyo si usafi wa kitanda wala nguo za ndani, nimezungumza mpaka nimechoka, kuna wakati fulani dada wa kazi eti alikuwa anafanya usafi chumbani kwetu, bila kuingilia kati huenda angepewa na cchuup afue.

Nimeamua kuwa mhanga nafua nguo za ndani ninazozikuta kwenye tenga (zikiwemo zake) na kufanya usafi chumbani.

**Ila akili kichwani asee hapa nimechamba nimeibuka na nyaa.
 

Attachments

  • VID-20230119-WA0005.mp4
    4.5 MB
Makubwa mmeanza kuwasema huku...watawanyoosha hakika ....kuna waliooa wanafurahia hawakuwahi hata kujutia kuwaoa wake zao na kuna ambao wanajutia kuoa hahaha..halafu hapo vuta picha na mwanamke ulimwacha bila sababu na alikuonyesha upendo wa dhati halafu ukamwona kama bwege,,,hapo lazima umkumbuke,,,,,tehteh....uwiii
 
Nianze kwa kusema mimi ni kijana wa miaka 35 sasa, nimeoa mwaka wa 6 huu, na nina watoto wawili, ila ujumbe wangu wa leo vijana mnapoamua kuoa muwe mmemaanisha hawa wake zetu unahitaji akili ya ziada kuishi nao wengi wana upeo wa chini sana na wasahaulifu kupitiliza.

Hivyo kijana usipokuwa muelewa unaweza kuwa unagombana nao kwa sababu ambazo unaweza kuziepuka.

NB: Binafsi katika miaka hiyo ya nda nimejifunza na kushuhudia mengi upo wakati nilitaka kuachana na mke wangu kwa kelele zake na kutofuata ninachotaka mimi. Ila baadae nikaamua kumpotezea nimeamua kuwa kimya kama mjonga flani hivi ila akili kumkichwa.

Sina la kuongeza maana nimeoa nauona moto wake, Unaweza kuyayusha hata hicho Chuma cha uvumilivu.
 
Ukitaka amani katika familia ni lazima baba awe kichwa yaani mfalme.yaani mfumo dume. Haiwezekani basi bora umkabidhi madaraka tu. Vitabu vitakatifu havikukosea kumpa mamlaka baba. Wanawake mtusamehe lakini ndio ukweli hakuna balance sheet kati ya mume na mke kwisha!
 
Hakuna Mwanaume yoyote amae ameoa hajawahi au hatoumizwa na mwanamke aliemuoa, hayupo, kama yupo basi ni mume bwege au hajitambui au amejitia ukiziwi au upofu kupisha mambo yapite.
makubwa mmeanza kuwasema huku...watawanyoosha hakika ....kuna waliooa wanafurahia hawakuwahi hata kujutia kuwaoa wake zao na kuna ambao wanajutia kuoa hahaha..halafu hapo vuta picha na mwanamke ulimwacha bila sababu na alikuonyesha upendo wa dhati halafu ukamwona kama bwege,,,hapo lazima umkumbuke,,,,,tehteh....uwiii
 
Back
Top Bottom