KUISHI KWINGI NI KUONA MENGI !

KUISHI KWINGI NI KUONA MENGI !

Isengelo

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Posts
539
Reaction score
927
Heshima kwenu wanajanvi.

Bila kuwachosha niende kwenye mada moja kwa moja

Kuna mama mmoja ni rafiki wa Mke wangu na tunaishi eneo moja wilayani.

Mama huyu alimsomesha mtoto wake wa kwanza wa kiume shule za kiingereza (English medium) kuanzia chekechea hadi kidato cha nne.

Bahati nzuri, kijana alichaguliwa kidato cha tano Mwaka 2017.

Baada ya kumaliza muhula wa kwanza, kijana huyu alirejea nyumbani sehemu tunayoishi akiwa na malalamiko Kibao kwa mama yake; Oh mama Mimi sirudi shule tena, nimeacha shule.

Mama yake alivyomhoji kulikoni, akasema, walimu hakuna, chakula kibaya wadudu Kama chawa, kunguni wanasumbua.

Mama alimbembeleza mwanaye arudi shule bila mafanikio. Ndipo alipohitaji nguvu ya ziada toka kwangu nimsihi mtoto arudi shule.

Nilichofanya nilimwambia yule mama umemueleza baba yake
akajibu ndiyo, lakini baba naye kazidiwa nguvu.

Wakuu kwa nia njema nilitafuta ridhaa ya Mke wangu ambaeye ni rafiki ya mama yule ili nimnasihi mtoto arudi sh shule, Mke wangu alikubaki.

Nilimtafuta yule kijana tukaenda kubarizi sehemu na kuanza kumwambia arejee shule.

Cha ajabu na cha kusikitisha wanajanvi, kijana yule aliporudi nyumbani siku ile, mnamo majira ya SAA tatu za usiku, alimfungia mama take ndani ya nyumba yao na kuanza kuwaita watu akiwemo baba yake, Mke wangu, balozi na majirani akidai ameniona Mimi na mama yake tumeingia chumbani na kujifungia.

Baada ya watu kujaa, na kuizunguka nyumba ndipo alipofungua milango na watu hao waliingia ili hayo aliyasema ni kweli?

Baada ya msako wa nyumba nzima aliyekuwemo humni mama yake pekee.

Nilichogundua Mimi maneno yangu yakumtaka aende shule hayakumfurahisha na hicho ndicho kisasi chake kwangu.

Tetesi zilizopo mtaani, kijana huyu amerubuniwa na kabinti aache shule ili, waishi pamoja Kama mume na Mke,

Karibuni wakuu kwa ushauri
 
mkuu tenda wema nenda chako, duniani kuna kiumbe mmoja tu ambaye ni wa ajabu kuliko viumbe vyote yaan binadam. unaweza kuwa umekaa na mtu mnacheka lakini ukifunguliwa moya wake na ukaona anachokuwazia unaweza ukakimbia toka ubungo hadi chalinze bila kugeuka nyuma kwa hofu, mimi wakati mwingine huwa najitafakari hadi nasema kweli pale Mungu aliporegrect kwa kumumba mwanadam ni kweli kabisa kwasababu naweza kaa ndani ya dakika kumi lakini nilichokiwaza ni upuzi mtupu
 
Kama amesema shule mbaya kwanini kati yenu hakuna aliyemuuliza kama anataka kubadilishiwa shule?

Hakuna sehemu uliyosema kama mlimpa option ya kwenda shule nyingine.

Katika wote waliomshauri kurudi shule kwanini ni wewe tu ndiyo kakutungia kisasi?

Kijana wa form five kurubuniwa aache shule na binti ili waishi ni kesi nadra mno. Mmeongea na huyo binti?
 
Umenena vizuri mkuu, alimwambia mama yake amtafutie shule ya private alizozoea, lakini kutokana na uchumi wa mama Huyo kuyumba Hana uwezo tena.

Kama mtoto wa rafiki nilianza kumkemea kuhusu kuwa na Huyo binti hata kabla ya kwenda shule muhula wa kwanza. Hata yule binti alijenga chuki na Mimi. Alipopewa fedha kwa ajili ya shule alibadilisha matumizi na kuondoka na Huyo binti na kumpangia nyumba mjini karibu na shule, huo ni mrejesho wa wanafunzi wenzake.
MY TAKE

Tuwe makini na shule tunazopeleka watoto wetu, kijana sass hivi makundi sanaaa, bange mbele maisha ya kibongo movie, yasiyoendana na maisha Halisi ya kipato cha wazazi wake

Kinachosikitisha zaidi Hana uelewa Kama yeye ni kidato cha tano kweli.

Kama wewe huwezi hurumia wazazi wako ambao wamekusomesha kwa kukopa na kujibana, nini uwezo wako wa kufikiri Kama kidato cha tano?

Miongoni wa washauri ukiachilia babake ni Mimi peke yake ndo Me, wengine wote ni KE marafiki wa mama yake.
 
Watoto wanakuwa wazuri wakiwa wadogo tu ila wakishabalehe ni wachache sana wanaendelea kuwa wazuri kitabia but the rest wanageuka mikuki ya kuumiza mioyo ya wazazi hadi wazazi wanaregret kwa nn tumemzaa huyu, uzuri dunia ipo kumfundisha yule asiyetaka kusikiliza wazazi, mkuu wewe mwache huyu dogo mwalimu dunia yupo anamsubiri kwa hamu sana
 
Umenena vizuri mkuu, alimwambia mama yake amtafutie shule ya private alizozoea, lakini kutokana na uchumi wa mama Huyo kuyumba Hana uwezo tena.

Kama mtoto wa rafiki nilianza kumkemea kuhusu kuwa na Huyo binti hata kabla ya kwenda shule muhula wa kwanza. Hata yule binti alijenga chuki na Mimi. Alipopewa fedha kwa ajili ya shule alibadilisha matumizi na kuondoka na Huyo binti na kumpangia nyumba mjini karibu na shule, huo ni mrejesho wa wanafunzi wenzake.
MY TAKE

Tuwe makini na shule tunazopeleka watoto wetu, kijana sass hivi makundi sanaaa, bange mbele maisha ya kibongo movie, yasiyoendana na maisha Halisi ya kipato cha wazazi wake

Kinachosikitisha zaidi Hana uelewa Kama yeye ni kidato cha tano kweli.

Kama wewe huwezi hurumia wazazi wako ambao wamekusomesha kwa kukopa na kujibana, nini uwezo wako wa kufikiri Kama kidato cha tano?

Miongoni wa washauri ukiachilia babake ni Mimi peke yake ndo Me, wengine wote ni KE marafiki wa mama yake.

Mwanafunzi wa kidato cha tano ni mtu mzima katika nchi nyingi sana, ana maamuzi yake.

Sitetei uzinzi lakini huu ndiyo muda wa yeye kua na wapenzi kumkanya kijana wa form five asiwe na mpenzi naona ni wrong move, badala yake mngemshauri katika namna ambayo mapenzi yasiingilie majukumu na wajibu wake.

Ajue kua kuna mapenzi na wajibu, na kwa sasa wajibu wake ni kusoma na kurudi na matokeo mazuri nyumbani.

Kwa umri wake pia balehe ndiyo inamalizia kutia nanga ama ipo katikati ya kutia nanga, maamuzi anayofanya yawezekana yanakua fueled na balehe na ikitokea mkaongea naye vizuri mkaona kila maana halisi ya jibu lake.

Uwezekano ni kua, hata kudai hataki shule ni mnashambulia wrong target. Hao wanajua kabisa kua kuishi pamoja kunahitaji chanzo imara cha kiuchumi hakuna ambaye angekubali kuishi huku hawana uhakika wa kesho.

Mimi nahisi huyu mwanafunzi ni mhanga wa bullying. Bangi? Hapana nimesoma na wavuta bangi na wavuta gundi. Ukiongea naye usiende na maelekezo nenda kamsikilize yeye anataka kuekekea wapi, taka kujua anajiona wapi baada ya miaka 2? Chuo, mtaani au chumbani na huyo binti.
 
Back
Top Bottom