Kuisaka Maiti Ya Osama bin Laden Baharini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuisaka Maiti Ya Osama bin Laden Baharini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa serikali ya Marekani imeshindwa kuwathibitishia watu kuuliwa kwa Osama bin Laden na maiti yake kuzikwa baharini kama wanavyodai, mtaalamu mmoja wa kupiga mbizi baharini wa nchini Marekani amepanga kutumia dola laki nne kuisaka maiti ya Osama bin Laden kwenye bahari ambayo maiti yake ilidaiwa kutupwa.

  Bill Warren ambaye ni mtaalamu wa kupiga mbizi baharini mwenye makazi yake mjini San Diego, California nchini Marekani, ameamua kuisaka maiti ya Osama bin Laden baharini ili kujua kama kweli Osama bin Laden aliuliwa na maiti yake ilitupwa baharini.

  Akitumia teknolojia za kisasa zilizotumika kuisaka meli ya Titanic, boti za wapiga mbizi na submarine, Warren ametenga dola laki nne kuusaka mwili wa Osama bin Laden baharini.

  Kazi ya kuusaka mwili wa Osama itaanza mapema mwezi ujao kwa kuanzia upande wa bahari ya Hindi magharibi mwa India.

  Warren mwenye umri wa miaka 59 alipoulizwa sababu ya kutumia pesa zake kuusaka mwili wa Osama alijibu kwa kusema "Nafanya hivi ili kujua kama kweli Osama aliuliwa, tunaamini rais Obama ameshindwa kuwathibitishia watu kuwa Osama bin Laden ameuliwa".

  "Nina mpenzi wangu Mrusi ambaye amekuwa akiniambia kuwa Majasusi wa Urusi hawaamini kama Osama bin Laden ameuliwa kweli, mimi simuamini rais Obama wala serikali yake", aliongeza Warren.

  "Serikali ya Obama ilitakiwa itoe picha kama ilivyofanya wakati alipouliwa Saddam Hussein", alisema Warren.

  Serikali ya Marekani imedai inazo picha za kuuliwa kwa Osama bin Laden ingawa ni wanasiasa wachache sana walichaguliwa kuonyeshwa picha hizo.
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Source pls.
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mkuu wasomali watalipwa kiasi gani? Maana si ajabu teyari wapo baharini wanatafuta maiti ya OBL
   
Loading...