Kuididimiza sekta ya MITUMBA ni kuondoa ajira na kuongeza umaskini kwa jamii

MTISHBI

Member
Feb 2, 2012
15
8
Katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017 Serikali imeonesha nia ya kuididimiza kwa kupandisha kodi na hatimaye kuiua kabisa sekta ya mitumba miaka michache ijayo. Sekta ya mitumba inatoa ajira kwa watu wengi sana wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume kwa nchi nzima.

Sidhani kama viwanda vitakavyoanzishwa vitaweza kutengeneza ajira kwa idadi kubwa ya watu kama ile ya watakao poteza ajira kwa mitumba kupigwa marufuku, hivyo serikali ifikirie upya adhma yake hiyo. Ni bora wakaboresha mifumo ya kukagua mizigo kabla ya kuingia nchini kuliko kusema mitumba ina madhara.
 
Hiii ni Villagelization nyinyi hamjui Karikoo Kulikua Kuna City ndo wanapambana na Machinga sasa hivi kuna Polisi (FFU) Hakuna wagambo tena mji umetakata.
 
Katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017 Serikali imeonesha nia ya kuididimiza kwa kupandisha kodi na hatimaye kuiua kabisa sekta ya mitumba miaka michache ijayo. Sekta ya mitumba inatoa ajira kwa watu wengi sana wazee kwa vijana, wanawake kwa wanaume kwa nchi nzima.

Sidhani kama viwanda vitakavyoanzishwa vitaweza kutengeneza ajira kwa idadi kubwa ya watu kama ile ya watakao poteza ajira kwa mitumba kupigwa marufuku, hivyo serikali ifikirie upya adhma yake hiyo. Ni bora wakaboresha mifumo ya kukagua mizigo kabla ya kuingia nchini kuliko kusema mitumba ina madhara.

Kwani watanzania lazima tuagize mitumba?nguo mpya hatuwezi? Acha ulalamishi usio maana. Magari used mpaka chupi tuagize used! Haiwezekani bana kama mitumba ndio mmeona ni biashara pekee basi mtaisoma no. Mabadiliko machungu lakini hatuna namna lazima tufanye.tusipende pepo ili hali tunakuwa waoga wa kifo.
 
Mkuu sio ulalamishi umeshawahi nunua hata fulana ya KTM ukavaa jaribu kwanza.mitumba imeajir wengi sana kwahyo tunahitaji viwanda vyenye ubora Wa kutengeneza pamba Kali ili hawa wauza mitumba watuuzie hzo zenye ubora otherwise ntaendelea kuvaa mitumba kocopy fashion za nje maana hamna kiwanda cha bongo kinachomvalish a hata Ali kiba ili vijana wapende vya nyumbani kupitia yeye..lakin wauza mitumba wananipigisha mapigo ya kina chriss brown
 
Back
Top Bottom