Kuibuka sasa kwa kashfa ya LUGUMI ni mpango wa Mungu Watanzania wamjue waliomuamini na kumsifia

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Mungu ana makusudio kwa watu wake waliokuwa wameanza kulishwa matango pori kupitia vyombo vya habari kuwa amepatikana malaika tena mtenda haki asiyestahili hata kukoselewa na ukimkusoa wewe si mzalendo bali una wivu tu na chuki dhidi yake.

Tumeaminishwa haangali sura,hana chama, anasimamia haki,hamuogopi mtu, n.k na zaidi tumuombe kwa mungu.

Hata hivyo,limeibuka jambo ambalo litawasaidia wengi kama si wote kujua ukweli halisi kuhusu mtu huyu na kama kweli anafanya mambo yanayostahili yeye kuombewa.

Mungu aliona asisubiri sana maana watu wake wanazidi kupotea-the earlier the better.

NB: Kupitia mungu huyo huyo,vice versa is also true.

Tusubiri.
 
Una maanisha mtumbua majipu au ?.Mimi nilimsikia Membe akitoa maoni yake kuhusiana na Dr Majipu nikasema ngoja nisubiri muda utasema yote bado nasubiri mwisho wa hili sakata.
Kwa tuhuma hizi nzito nilitarajia kusikia watu fulani wamesimamishwa au teuzi zao zimetenguliwa ila cha ajabu bado wako ofisini alafu tunaambiwa tumempata Sokoine!!!
 
Teh Teh kuna siku ulisema una subiri amtumbue aliye mteua na hili likipita utasema tena...
Bawacha mmeshakuwa kama watoto Yatima ni kulialia tuu.
Inawezekana alifanya hivyo baada ya kelele kuzidi ila bado kuna wengine wanadunda.
 
Kwa tuhuma hizi nzito nilitarajia kusikia watu fulani wamesimamishwa au teuzi zao zimetenguliwa ila cha ajabu bado wako ofisini alafu tunaambiwa tumempata Sokoine!!!
Hivi wakisimamishwa bila uchunguzi wewe si utakuja hapa kuanza kusema kuwa wanaonewa? Hivi mmejisahau huwa mnasema serikali ina kurupuka? Leo hii mnataka watu wasimanishwe kazi hata niki kuuliza nani asimamishwe na kwasababu gani hujui!

Kwanini mnakuwa na vichwa vya panzi? Hivi ulimsikia mwenye kiti wa PAC jana?
 
Kasi ya kumtimua Mama Kilango ilifurahisha lakini Ligumi mhaaa haaa ha aaa eti Tanzania tumempata Sokoine wetu hata 2% bado hajamfikia.

JAMANI KWA MAMA KILANGO MMELALAMIKA KUWA HAJATENDA HAKI KWANI HAKUPEWA NAFASI YA KUSIKILIZA.SASA AMETULIA AONE WIZARA NA BUNGE WATAFIKA WAPI ILI ASILALAMIKIWE KUWA HAKUTOA MUDA WA KUTOSHA BADO MNALALAMIKA. HUU UJINGA SASA
 
"Mkikamata mafisadi wa EPA nchi italipuka" - IGP Mstaafu.
Kumbuka huyu bwana alikuwa amekula kiapo cha utiifu wakati akiyasema haya, na mlango wa nyuma aliyajua haya ya Lugumi pia. Kama viongozi wanawekwa na Mungu na wanaishia kufanya haya si ajabu ndio maana nchi yetu inaendelea kuandamwa na laana.
 
Mungu ana makusudio kwa watu wake waliokuwa wameanza kulishwa matango pori kupitia vyombo vya habari kuwa amepatika malaika tena mtenda haki asiyestahili hata kukoselewa na ukimkusoa wewe si mzalendo bali una wivu tu na chuki dhidi yake.

Tumeaminishwa haangali sura,hana chama,anasimamia haki,hamuogopi mtu, n.k na zaidi tumuombe kwa mungu.

Hata hivyo,limeibuka jambo ambalo litawasaidi wengi kama si wote kujua ukweli halisi kuhusu mtu huyu na kama kweli anafanya mambo yanayostahili yeye kuombewa.

Mungu aliona asisubiri sana maana watu wake wanazidi kupotea.

NB: Kupitia mungu huyo huyo,vice versa is also true.

Tusubiri.
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom