Kuhusu udhamini wa azam tv: Vilabu 13 vya ligi kuu tanzania bara vyaishukia yanga

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
[h=3]VILABU 13 VYA LIGI KUU TANZANIA BARA VYAISHUKIA YANGA KUHUSU UDHAMINI WA AZAM TV[/h]

[h=1][/h]Katika siku za hivi karibuni, kumekuwapo na mjadala kuhusiana na hatua ya klabu ya Yanga kupinga udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania unaotarajiwa kufanywa na Azam Media.


Tumeona ni vema tukatoa msimamo wetu wa pamoja kuhusiana na hatua hiyo ya wenzetu kwa lengo la kuweka rekodi sawa. Tunataraji hatua hii ya vilabu hivi 13 itafunga mjadala huu na tungependa wana habari, kama mtaamua kuuendeleza, basi muundeleze katika mlengo ambao wadau, yaani sisi vilabu vinavyoshiriki mashindano hayo, zimeamua kuufuata.


Tunapenda kukumbusha kwamba kwa muda mrefu, kilio cha vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania kilikuwa ni ukosefu wa wadhamini na kwa bahati nzuri kuna dalili kwamba Mungu ameanza kukisikia kilio hicho msimu huu.



Kwa faida ya umma, tungependa kutoa takwimu za nchi jirani zinazotuzunguka. Kenya, kila klabu hupata Sh milioni saba za Kenya (sawa na Sh milioni 125 za Kitanzania) kwa mwaka –fedha ambazo zimeifanya ligi ya Kenya kuwa na uwiano na ushindani wa kweli (fedha hizo ni mjumuisho wa gharama za matangazo ya televisheni na udhamini wa bia ya Tusker).



Tanzania leo tunajivunia kuwazidi Kenya kutokana na udhamini wa Azam ambapo kwa mwaka huu, kila klabu itapata zaidi ya Sh milioni 170 (Jumla kutoka milioni 100 za Azam na milioni 70 za Vodacom).



Hatuna sababu ya kutaja viwango vya udhamini kwa nchi nyingine jirani kama Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia nk kwa vile zote zina udhamini wa chini kuliko Kenya. SuperSport, ambao wanaliliwa na baadhi yetu, udhamini wao kwa ligi ya Uganda ni dola 350,000 ambazo ni pungufu kulinganisha na dola milioni moja zilizotolewa na Azam Media hapa nchini.



Ni imani yetu kwamba udhamini huu utaifanya ligi ya Tanzania kuwa bora kuliko zote za Afrika Mashariki. Hili litasaidia kutengeneza timu bora ya Taifa ya Tanzania. Tungependa kutoa ufafanuzi wa masuala machache ambayo yaliongelewa na wenzetu wa Yanga kama sababu za kupinga udhamini huu.



BODI YA TPL
Kwa mujibu wa Katiba za FIFA, CAF na TFF, Haki za Televisheni zipo chini ya FA ya nchi husika. TFF iliamua kukasimu shughuli ya majadiliano kwa Kamati ya Ligi ambayo ilishirikisha vilabu vyote 14, ikiwamo Yanga na wawakilishi wake walihudhuria mchakato mzima hadi mwisho.


Hoja ya Yanga kuwa bodi haina nguvu/Mamlaka kisheria kwa kuwa ni ya mpito inakosa mashiko kwa sababu kimsingi ni TFF ndiyo iliyoingia mkataba kwa sababu ndiyo iliyopewa mrejesho na Kamati ya Ligi kwamba mchakato umekwenda sawasawa.



Hoya ya kuwa Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA. Hili si kweli hata kidogo. Mmoja wa wajumbe wa TPL ni Seif Ahmed almaarufu Seif Magari; ambaye vyeo vyake ndani ya Yanga vinajulikana.



Kama alikuwa hahudhurii vikao vya TPL, hilo ni suala la Wanayanga wenyewe kumuhoji kwanini alikuwa hahudhurii hivyo na hivyo kuinyima klabu yake ushiriki katika mijadala muhimu kwa maslahi ya soka hapa nchini. Ifahamike pia kwamba TPL haikuhodhi mchakato huu bali ilitoa fursa kwa vilabu vyote vya Ligi Kuu kushiriki ambapo Yanga ilikuwa ikiwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga na Katibu Mkuu, Lawrance Mwalusako.



Hii maana yake ni kwamba hoja kuwa Yanga haikushirikishwa ni mfu. Yanga walitumia neno UTARATIBU WA DUNIA NZIMA wakisema eti hakuna mahala duniani ambapo kampuni yenye klabu inayocheza ligi husika kupewa mkataba wa udhamini au urushwaji wa matangazo.



Inaonekana Yanga hawakufanya utafiti kwani ligi ya Afrika ya kusini ina timu inayoitwa Super Sports United na inarushwa na kituo cha TV chaSupersports. Pia majirani zetu Kenya wana timu inayoitwa Tusker FC huku ligi hiyo ikidhaminiwa na bia ya Tusker.



Tunawashauri Yanga kuwa ni vema kufanya utafiti kabla ya kuibuka na hoja za namna hii ili kuepuka kuwapotosha wanachama wao. Yanga pia katika hoja zao wamepinga utaratibu wa kugawana mapato sawa. Hoja hii ni ya msingi na majadiliano yetu yalilitazama hili kwa kina lakini tukaona kwa mazingira ya Tanzania na uchanga wa ligi yenyewe kwa sasa ni heri kugawana sawa ili pesa kwa usawa ili itoke kwa wakati na kusaidia vilabu kujiendesha.


Yanga wanakosea wanaposema eti wao wanastahili kupewa zaidi kwa sababu ni klabu kubwa na yenye mashabiki wengi kwa kuwa sababu hii haitumiki sehemu yoyote duniani.


Tuchukulie mfano wa nchi ya England ambako ingawa Liverpool ina washabiki wengi kuliko Manchester City na Chelsea, imezidiwa kwenye mapato ya televisheni na timu hizo.



Hii ni sababu kinachoamu mapato mwisho wa siku ni kiasi cha mechi za timu ambazo zimeonyeshwa na televisheni kwenye msimu husika na nafasi ya timu kwenye msimamo wa ligi.



Hata hivyo, ikumbukwe kwamba nchini England, malipo haya hufanyika baada ya msimu kumalizika na hapo ndipo watu hukaa chini na kupigiana hesabu za nini kilipatikana. Sasa ukitumia mfumo huu, ina maada timu zitalazimika kusubiri ligi iishe ili kuangalia msimamo ya ligi kisha kugawana mapato. Sote tunajua jinsi timu zinavyoteseka kwa kukosa nauli, posho, mishahara, pesa za kambi nk.



Kwa mazingira yetu ya Tanzania kwa sasa, mfumo kama huu haufai. Hii ni kwa sababu timu zinahitaji fedha kuanzia kwenye maandalizi ya mechi ya kwanza na hazikopesheki fedha kwenye mabenki. Tanzania inachohitaji kwa sasa ni ligi yenye ushindani tofauti na sasa ambapo ushindani uko kwa timu chache zenye uwezo wa kifedha.



Tukizijengea uwezo timu zote taifa litakuwa na ligi nzuri na hatimaye timu nzuri ya taifa. Pia itawezesha wadhamini wengi zaidi kuingia kwenye mpira na hivyo timu nyingi zaidi kufaidika.

Tukifikia huko, tunaweza kukaa chini na kutazama mfumo wa kugawana mapato utakaokuwa bora zaidi wakati huo.


Mambo ya Kuzingatia.Tangu ligi ianze hapa nchini takribani miaka 50 iliyopita, hakuna timu iliyowahi kulalamikia mfumo wa kugawana mapato sawa kwa kila mechi ambao umekuwa ukitumika. Mfano mapato ya mlangoni tumekuwa tukigawana sawa na Yanga haijawahi kulalamika, Pesa za udhamini wa Vodacom tangia ilipokuwa ikidhaminiwa na TBL hadi leo hii tumekuwa tukigawana sawa na Yanga haijawahi kulalamika kutaka kupata zaidi kwa kuwa eti ina mashabiki wengi, pia hata pesa za haki ya matangazo ya Televisheni zilizowahi kutolewa huko nyuma nailiyokuwa ikiitwa GTV, na Star TV kwa nyakati tofauti pesa ziligawiwa sawa kwa kila timu.


Hii ni kwa sababu kikanuni, timu zote zinazoshiriki kwenye ligi ni sawa na zote zinaweza kuwa bingwa au kushuka daraja. Ni mdudu gani huyu aliyeingia kwenye soka ya Tanzania na kuanza kuleta siasa za kubaguana? Baba wa Taifa alipata kutuasa kwamba dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu. Ikianza, haitaishia kwenye ligi pekee na itakwenda hadi mahali tusipotaka.



MGOGORO WA MASLAHI.
Yanga imekuwa ikilalamikia uwepo wa kiongozi mwandamizi wa makampuni ya Bakhresa kwenye bodi ya Ligi na kusema inaleta mgongano wa maslahi. Sisi vilabu tunaamini kwamba uwepo wa kiongozi huyu ndiyo umesaidia makampuni yake kuwekeza fedha kwenye mpira. Na mifano ipo hai tukianzia na michuano ya Vijana ya Uhai Cup, ujenzi wa kituo cha michezo cha Chamazi ambacho kinatumiwa na timu nyingi za Tanzania.



Na sasa tunafaidika na udhamini huu mnono ambao haujapata kutokea katika historia ya Tanzania. Tungependa viongozi wengi zaidi wa makampuni yanayoheshimika hapa nchini wakijitokeza kuongoza mpira badala ya kuanza kuwapinga. Kwa mfano tungependa kuona Mkurugenzi wa Benki ya CRDB akiwa kiongozi wa Ashanti, bosi wa Barrick akiongoza Mbeya City na Mkurugenzi wa Tanga Cement akiongoza Coastal Union.



Hivi ndivyo namna mpira unavyoweza kuvutia wawekezaji. Ndiyo maana tulifurahi wakati Yusuf Manji, alipoomba uongozi Yanga.

Bado tunataraji kwamba naye atajitosa kuingiza fedha zake kwenye ligi ya Tanzania (mpira) kama alivyofanya Bakhresa ambaye pamoja na kutumia fedha zake Azam FC, bado ameamua kusaidia na timu nyingine kwa ujumla.Tunapenda kumuahidi Yusuf Manji kwamba iwapo naye atataka kudhamini Ligi Kuu iwe kibiashara au kiufadhili, sisi tutamuunga mkono na hatutajali suala la mgongano wa maslahi.



UPOTEVU WA MAPATO
Wenzetu Yanga wamedai kwamba kwa kuonyesha mechi kwenye televisheni, mapato yake ya mlangoni yatapungua.

Hili pia halikufanyiwa utafiti wa kutosha. Katika siku za karibuni, mechi zilizoingiza mapato makubwa zaidi ya milangoni ni zile ambazo zilionyeshwa Live kwenye televisheni za ndani na nje ya nchi. Mifano ni mechi za watani wa jadi msimu uliopita zilizoonyeshwa Live na SuperSport na mechi za Kombe la Kagame zilizoonyeshwa wakati huo.



Hata mechi ya Taifa Stars na Ivory Coast iliyoonyeshwa Live pia, ilijaza uwanja. Ulaya ambako karibu kila familia inamiliki televisheni na umeme wa uhakika, bado watu wanajaa katika viwanja vya soka. Mpira kuonyeshwa kwenye televisheni unaufanya utangazike zaidi na watu watake kuona. Kuna faida nyingi za mpira kuonyeshwa kwenye televisheni kuliko hasara moja ya kufikirika ambayo Yanga wanaiona.



Ingekuwa vema iwapo Yanga wangetoa takwimu za kuonyesha ni kwa namna gani mechi kuonyeshwa kwenye televisheni kuliwahi kupunguza mapato ya milangoni. Kwa faida ya umma, mpira kuwa kwenye televisheni kuna faida zifuatazo; jezi kuongezeka thamani na hivyo kuvutia makampuni makubwa kutaka kudhamini klabu wakitumia fursa ya kutangaza bidhaa zao, matangazo ya viwanjani (touchline fence) kuwa na thamani zaidi ambapo kwa sasa vilabu havipati chochote, kuchochea michezo ya kubahatisha, kutabiri matokeo na kupata habari kupitia simu za mkononi na hivyo vilabu vitaanza kutengeneza fedha za kutosha.



Ulaya wamesonga mbele kutokana na televisheni. Anayekataa mpira kuonyeshwa kwenye televisheni ni sawa na mtu anayegoma kutumia mfumo wa digitali katika ulimwengu wa leo.



UWAZI KWENYE MCHAKATO WA KUUZWA KWA HAKI ZA MATANGAZO
Yanga wameandika kwenye taarifa yao rasmi eti hakukuwa na uwazi kwenye mchakato wa kuipata kampuni ya kurusha matangazo ya Televisheni. Sote tunajua kuwa vituo vya televisheni vilivyopo nchini kama Star TV ambayo iliwahi kurusha mechi kadhaa msimu uliopita vilikuwa vikijua kuwa kuna nafasi hiyo na TFF mara kadhaa wamekuwa wakitangaza hilo kupitia idara ya Habari ya TFF.



TFF kwa mfano walikwenda mbali kwa kuialika Supersports kuja kuonesha mechi bure kwa kilichokuwa kikiitwa Super Week ili kuwashawishi waje kuwekeza na mara ya mwisho ni Yanga hawa hawa walioongoza harakati za kuikataa Supersports kuonesha mechi bure wakisema kuwa kama ni kuwavutia inatosha. Katika mazingira kama haya tunastaajabishwa na ukigeugeu wa Yanga leo kusema eti tenda haikuwekwa wazi. Sote tunajua kuwa ni Super Sports pekee tuliokuwa tukiwategemea na kuwashawishi ambao hawakuonesha kuhitaji kuja kuwekeza. Kwa nini leo tuikatae Azam TV?



Yanga wanaposema eti TFF/Kamati ya Ligi imeipa haki za matangazo kampuni ambayo haina ofisi wala kituo cha televisheni kilicho hewani kwa sasa wanasahau kuwa huko nyuma TFF iliwahi kuwapa haki za matangazo GTV ambao hawakuwa na ofisi wala kituo cha TV na baada ya miezi michache walifungua ofisi zao na kuleta vingamuzi na kuaza kurusha mechi zetu.



Vilabu vilifaidi udhamini ule kabla ya ile kampuni kufilisika. Kwa hiyo hii si mara ya kwanza kwa jambo hili kufanyika na kama Azam TV hawataonesha mechi za ligi hiyo sisi kama vilabu haituhusu kwani ni hasara yao.



Tunachowaomba Azam Media sisi kama vilabu ni kuhakikisha wanatulipa pesa zetu kwa haraka ili zitusaidie kwenye maandalizi,Tunawaomba Yanga wasichafue hali ya hewa kwa kuwa wao hawana shida ya Pesa.



Sisi Umoja wa Vilabu 13 vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania tunapinga, kwa nguvu zote, madai ya Yanga kwamba hatukushirikishwa kama vilabu kwenye mchakato huu. Mfumo wa ugawanyaji wa mapato tuliouchagua, tuliuchagua wenyewe bila kushurutishwa na yeyote na tunadhani ndiyo mfumo unaotufaa kwa sasa hadi hapo ligi yetu itakapokuwa na nguvu maana kwa sasa inaruhusiwa klabu kupata fedha mwanzoni kulingana na hali halisi ya vilabu vyetu.



Tunawashauri wenzetu wa Yanga waanze kuamini kwenye kitu kinachoitwa Uwajibikaji wa Pamoja (Collective Responsibility). Mambo yanayoamuliwa kwenye vikao hayapaswi kupingwa nje ya vikao. Kama hoja ililetwa kwenye vikao na ikazidiwa nguvu na hoja nyingine, hakuna sababu ya kuikataa kwa sababu tu hukubaliani nayo. Mfumo wa kidemokrasia una kanuni moja kuu; Wengi Wape.



Imetolewa na
Vilabu 13 vya Ligi Kuu ya Tanzania


Simba SC, Azam FC, Ashanti United, JKT Ruvu, Ruvu Shooting Stars, Mgambo JKT, JKT Oljoro, Rhino Rangers, Mbeya City, Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar, Coastal Union na Kagera Sugar.

MWISHO
 
Hao wadudu wanao itwa Yanga wasitake kutuaribia ligi yetu Kama hawataki ni vyema wakajitoa kwenye hii ligi mapemaa kuliko kulinga linga. Wao wanafikiri wa TZ bado tupo kwenywe enzi zile? (Yanga yangu) sisi tusha toka huko
 
Hao wadudu wanao itwa Yanga wasitake kutuaribia ligi yetu Kama hawataki ni vyema wakajitoa kwenye hii ligi mapemaa kuliko kulinga linga. Wao wanafikiri wa TZ bado tupo kwenywe enzi zile? (Yanga yangu) sisi tusha toka huko

Yanga ndio habari ya mjini. Hao wengine wanafuata mkumbo tu - wanapelekwa kama magari mabovu wakati wajanja wachache wameisha kula kitu kidogo ili kuzidi kumnemesha Azam
 
"UWAZI KWENYE MCHAKATO WA KUUZWA KWA HAKI ZA MATANGAZO

Yanga wameandika kwenye taarifa yao rasmi eti hakukuwa na uwazi kwenye mchakato wa kuipata kampuni ya kurusha matangazo ya Televisheni. Sote tunajua kuwa vituo vya televisheni vilivyopo nchini kama Star TV ambayo iliwahi kurusha mechi kadhaa msimu uliopita vilikuwa vikijua kuwa kuna nafasi hiyo na TFF mara kadhaa wamekuwa wakitangaza hilo kupitia idara ya Habari ya TFF"

Ni wasiwasi na uelewa wa wawakilishi wa hivyo vinavyojiita vilabu 13 kwenye masuala ya tendering. Hivi wanaposema vituo vya TV vilivyoko hapa nchini vilijua kwamba kuna nafasdi hiyo TFF wana maana? TFF ilitangaza tender au ilikwenda kuzungumza na kituo kimoja kimoja kivyake? Kama TFF ilitaka mchakato uwe wazi, wangetangaza kwenye vyombo ya habari TV stations walete tender zao. Inawezekana ingepatikana TV station iliyo tayari kutoa pesa nyingi zaidi ya hizi zilizotolewa na Azam. Mtindo uliotumika kumpata huyo Azam unashawishi utoaji wa rushwa na haukubaliki.

Tiba
 
Unatumika bila kujijua ndugu yangu tena YANGA mwenzangu wewe!
Plz JITAMBUE!

Labda wewe ndio hujitambui. Hapa si suala la uYanga in the first place. Huyo Azam kaonyesha mpira wapi kwa kuanzia? Maadam kataja 100m basi watu wamelewa hawaelewi kitu. Anze kwanza na TV yake, aonyeshe hata mechi mbili tatu, mchakato aunze na tenda iwe wazi. Hivi kweli mshindi wa kwanza apate sawa na mwisho? Gharama wanazoingia kufikia hapo ni sawa - kuanzia usajili, kambi, usafiri nk
 
Labda wewe ndio hujitambui. Hapa si suala la uYanga in the first place. Huyo Azam kaonyesha mpira wapi kwa kuanzia? Maadam kataja 100m basi watu wamelewa hawaelewi kitu. Anze kwanza na TV yake, aonyeshe hata mechi mbili tatu, mchakato aunze na tenda iwe wazi. Hivi kweli mshindi wa kwanza apate sawa na mwisho? Gharama wanazoingia kufikia hapo ni sawa - kuanzia usajili, kambi, usafiri nk
KILA TIMU INA HAKI YAKI VILE VILE WANANCHI WANAYO HAKI KUKUBALI AU KUKATAA YA YANGA TUACHIE WANAYANGA WAAMUE SIO KUWASHURUTISHA ETI WAKUBALI UDHAMINI SIO HAKI ZA ZA TIMU ZILE 13 HATA KIDOGO KWA SABABU YANGA HAWANUNUI MBUZI KWENYE GUNIA .:smile-big:
 
"UWAZI KWENYE MCHAKATO WA KUUZWA KWA HAKI ZA MATANGAZO

Yanga wameandika kwenye taarifa yao rasmi eti hakukuwa na uwazi kwenye mchakato wa kuipata kampuni ya kurusha matangazo ya Televisheni. Sote tunajua kuwa vituo vya televisheni vilivyopo nchini kama Star TV ambayo iliwahi kurusha mechi kadhaa msimu uliopita vilikuwa vikijua kuwa kuna nafasi hiyo na TFF mara kadhaa wamekuwa wakitangaza hilo kupitia idara ya Habari ya TFF"

Ni wasiwasi na uelewa wa wawakilishi wa hivyo vinavyojiita vilabu 13 kwenye masuala ya tendering. Hivi wanaposema vituo vya TV vilivyoko hapa nchini vilijua kwamba kuna nafasdi hiyo TFF wana maana? TFF ilitangaza tender au ilikwenda kuzungumza na kituo kimoja kimoja kivyake? Kama TFF ilitaka mchakato uwe wazi, wangetangaza kwenye vyombo ya habari TV stations walete tender zao. Inawezekana ingepatikana TV station iliyo tayari kutoa pesa nyingi zaidi ya hizi zilizotolewa na Azam. Mtindo uliotumika kumpata huyo Azam unashawishi utoaji wa rushwa na haukubaliki.

Tiba

Watu wanafurahia milion 100 bila kuangalia other issues, kwanza hiyo AZAM TV haipo, swali la kujiuliza hapo wamewapa tenda kwa kigezo kipi wakati huduma wanayotoa haijawahi kuonekana, ni kweli wametoa dau kubwa ambalo halijawahi kutolewa lakini huenda kama tenda ingetolewa hata hawa ambao walionekana wachovu huenda wangepanda dau.

Hii nadhani hii inawezekana TFF tu kwani haiwezekani mtu hujawahi kufanya kazi yoyote alafu upewe tenda, hata kama ametoa hizo hela bado mchakato ungefuatwa
 
Eti wanafananisha na kipindi cha nyuma yanga walikuwa wanagawana mapato wanasahau kuwa sasa hivi yanga kuna watu wenye shule na cash siyo enzi za akina ngozoma! Yanga hii ipo kidigital zaidi haiburuzwi hovyo na wako vizuri kwenye cash
 
Laiti Simba wasingepewa Mil 300 kwa kuwa na Simba TV ndani ya Azam Media nadhani nao wangekuwa pamoja na Yanga......!!Tumeona mara ngapi wakipinga hapa mechi zao kuoneshwa ila kipindi hiki wamehongwa kwanza ili wazishawishi vijitimu vidogo......!!
 
tatizo hawa yeboyebo wanachukia kila kitu chenye harufu na simba ingekuwa ni star tv wana hiyo deal ucnge sikia fyuuuu....ujinga huo mpira bongo utabak n majungu na kupoteza muda tu...
 
Yanga ndio habari ya mjini. Hao wengine wanafuata mkumbo tu - wanapelekwa kama magari mabovu wakati wajanja wachache wameisha kula kitu kidogo ili kuzidi kumnemesha Azam
Japo sikubaliani na mambo mengi ya Nyerere lakini hili naliunga kwa mademu%100. Nijuu ya wale maadui wakuu wa tatu UJINGA UMASIKINI na ELIMO. yani mpaka leo kauli ile inafanya kazi miongoni mwetu. Yani wewe upo kundi la wajinga.
 
Uongozi wa Yanga ulishakataa udhamini wa Azam TV, sasa nashangaa eti leo wanaitisha kikao cha dharura cha wanachama kujadili Azam TV. Unajadili kitu gani sasa? Ulichokwishatolea maamuzi? Au wanataka kurudi na kusema tumeona wanachama wengi wameukubali udhamini wa Azam TV?
 
Hii tenda ilitangazwa lini? PPRA wana taarifa? Vigezo vya tenda ni pamoja na kuwa na leseni hai, Azam TV ina leseni ya kurusha matangazo hapa nchini? Huo umoja wa vilabu 13 umeundwa lini? Viongozi wake ni akina nani? Walioandika utumbo huu majina na saini zao ziko wapi?

Hapa kuna harufu ya rushwa! Kuna watu wamepoketi chao bila shaka.
 
dah,tamko limesimama sana,kweli watu walitulia,naunga mkono tamko kwa maslahi ya soka la bongo
 
Nawashangaa wote wanaoilaumu Yanga kuhusu swala hili. Sio tu hawajui nini Yanga inataka, lakini hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano hawaielewi. Walichokataa Yanga ni mechi zao kuonyeshwa live, ambayo ni haki yao. Tatizo liko wapi? Wangesema mechi zote zisionyeshwe, kungekuwa na sababu ya kuihoji na hata huku kuinanga. Lakini kitendo cha kuilaumu na kuinanga kwamba si malikitu kwa sababu tu imekataa mechi zake zisioneshwe, kinadhihirisha hilo mnalolipinga: kwamba Yanga ni timu kubwa na inastahiki mgao unaozingatia hilo. Namna nyingine ya kuifafanua hoja yangu ni kwa kuuliza swala : hivi Rhino au Coastal ingekataa mechi zake zisionyeshwe, timu 13 zilizosalia zingeungana kuitolea kauli? Au mjadala huu ungezuka? Jawabu sahihi na rahisi ni 'hapana', na sababu sahihi na rahisi ni 'kwa sababu timu yenyewe hazina umuhimu huo kwenye ligi'. Takeni msitake, mmedhihirisha wenyewe kwamba Yanga ina sababu za msingi, la sivyo msingeilaumu kwa kukataa mechi zake tu kuonyeshwa moja kwa moja, ambayo ni haki yake ya kimsingi na kikatiba!
 
Labda wewe ndio hujitambui. Hapa si suala la uYanga in the first place. Huyo Azam kaonyesha mpira wapi kwa kuanzia? Maadam kataja 100m basi watu wamelewa hawaelewi kitu. Anze kwanza na TV yake, aonyeshe hata mechi mbili tatu, mchakato aunze na tenda iwe wazi. Hivi kweli mshindi wa kwanza apate sawa na mwisho? Gharama wanazoingia kufikia hapo ni sawa - kuanzia usajili, kambi, usafiri nk
Sibonike
1. wewe uzowefu wa AZAM unaujulia wapi na unautakia nini?
shida yako si ulipwe? pokea hela cheza mpira, kelel za kuw ahana uzowefu inakuhusu nini wkati hiyo ni biashara yake.
AU UNAKAMPUNI NYINGINE YENYE UZOWEFU UTUL ETEE?

2.Mchakato upi unautaka wewe? hivi mbona hamjitambui? kwani kuna mtu yeyote amabaye ameshatamani kuonyesha hii ligi? ninge waelewa na kuamini mnaakili kama mngeshangilia hili sasa kwani baada ya miaaka mitatu ya mkataba wake pengine kunaweza kujitokeza wapinzani wengine hila kwa sasa nani ataweka 5Bil. kwenye biashara ambayo haijawahi kufanyika?

3. Usajili,kambi, usafiri, mbona manakuwa washamba? hivi hata ligi ya uingereza unafikiri hela za TV ndio zinaweka timu kambini na usajili? hivi unajaua kuwa Uingereza hela za TV hulipwa mwisho wa msimu? Nyinyi hapa hata mechi moja bado na hela yenu mshalipwa mnapuga kelelel.


Kifupi hamna shukrani na ni kwa sababu mnatumika waTZ ndivyo mulivyo, Ningetamani AZAM TV angewapiga chini Yanga na anedelee na ahao wengine tuone yanga tutapata nini?

TUACHE WIVU
 
Last edited by a moderator:
Laiti Simba wasingepewa Mil 300 kwa kuwa na Simba TV ndani ya Azam Media nadhani nao wangekuwa pamoja na Yanga......!!Tumeona mara ngapi wakipinga hapa mechi zao kuoneshwa ila kipindi hiki wamehongwa kwanza ili wazishawishi vijitimu vidogo......!!

yanga wamepewa wanataka ifiki 380 eti zuku wanataka kuwapa 400.
hivi huu si uajnaja w akitoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom