Kuhusu uchaguzi wa jimbo la Mbinga Magharibi

Kuhusu uchaguzi wa jimbo la Mbinga Magharibi

Mtu kafa tu jana jamani mnaanza kutaka jimbo lake , je akifufuka

Kweli kufa kufaana
 
Walimwengu mnamambo, mtu hata bado kuzikwa mshaanza kufikiri nani atalithi viatu vya marehemu, si vyema jamani ila kama baada ya siku 90 kisheria ndo apatikane mrithi na isitoshe bunge kuvunjwa mwezi June, mi nadhani mrithi wa viatu vyamarehemu atapatikana October!
 
Nadhani sheria iko wazi. Hakutakuwa na uchaguzi mdogo ndani ya kipindi ambacho hakizidi miezi 18 kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Marehemu ataendelea kuliwakisha jimbo la mbinga mpaka October
 
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge
Uchaguzi
katika
majimbo za
uchaguzi
Sheria
ya 1984 Na.15
ib. 13
Sheria ya
2000
Na.3 ib.15
76.-(1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na
uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.
(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika
jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa
kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote
isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.
(3) Bila ya kujali masharti ya ibara hii yaliyotangulia, ifahamike
kwamba ikiwa tarehe ya kuvunjwa Bunge imetangazwa au
inafahamika kutokana na matukio yaliyoelezwa katika ibara ndogo
ya (3) ya ibara ya 90, basi uchaguzi wa namna hiyo hautafanywa
katika kipindi chote cha miezi kumi na mbili ya nyuma ikihesabiwa
tangu tarehe hiyo.
 
Back
Top Bottom