Kuhusu uchaguzi wa jimbo la Mbinga Magharibi

Kuhusu uchaguzi wa jimbo la Mbinga Magharibi

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,315
Hamjambo wanaJF,

Poleni na msiba wa mh. Komba.

Nauliza, kwa mujibu wa sheria baada ya siku 90 kama mbunge wa jimbo husika amefariki au amejiuzuru na jimbo kubaki wazi, Tume ya Uchaguzi inapaswa itangaze taratibu za kupata mwakilishi kwenye jimbo husika.

Tukirejea kwenye Jimbo la Mbinga Magharibi na ukizingatia bado miezi saba mpaka uchaguzi mkuu kufanyika; Je, hilo jimbo litakaa tu bila mwakilishi hadi Oktoba kwenye uchaguzi mkuu au watatangaza uchaguzi?
 
Nashauri ili kupunguza gharama za uendeshaji chaguzi inabidi yule kijana wake ambaye ni Chadema amrithi baba yake
 
Demokrasia ina gharama zake. Km sheria inataka uchaguzi ufanyike basi utafanyika bila kujali gharama au kilimo.

Kwa kua ni mwaka wa uchaguzi.kuna uchochoro unatumika kusubiri genera elections.ilitokea mwaka 2010 nadhani pemba na huku bara kulikua na majimbo yalio wazi
 
hamjambo wa jf
poleni na msiba wa mh Komba

naoliza tu kwa mujibu wa sheria baada ya siku 90 tume inapaswa itangaze taratibu za kupata mwakilishi kwenye jimbo husika
je hilo jimbo litakaa tu bila mwakilishi hadi October kwenyd uchaguzi mkuu au watatangaza uchaguzi?

Hakutakuwa na uchaguzi maana muda ulio baki ni mchache!
 
Subirini tuzike kwanza ndio muanzishe haya mambo

R.I.D (Rest in Destruction) Komba.
 
ili kuficha aibu ya chama kikubwa ni aheri tupotezee hadi October maana raia bado wana hasira za escrow
 
Nashauri ili kupunguza gharama za uendeshaji chaguzi inabidi yule kijana wake ambaye ni Chadema amrithi baba yake

Hilo wala hakuna haja ya kushauri kwa ufupi haiwezekani kufanya uchaguzi mdogo wakati hizo siku 90 zikiisha bunge linakuwa kimebakiza miezi mitatu ili livunjwe! Uchaguzi mdogo hautakuwapo! Tunasubiri mtanange!!
 
Kama Jimbo litakuwa wazi chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu HAKUTAKUWA na uchaguzi wa marudio!Nyasa watasubiri Oktoba wamchague Mbunge wao
 
Mtoto wa Komba akagombee,walau asave mali za baba yake
 
Hakuna uchaguzi someni ibara ya 76 (3) ya katiba.ya jamjamhuri ya muungano mwaka 77
 
Sina uhakika kama kutafanyika uchaguzi kwa hivi sasa kwasababu ya gharama....na mambo mengine.
 
Hakuna uchaguzi someni ibara ya 76 (3) ya katiba.ya jamjamhuri ya muungano mwaka 77

Pia wasome ibara ya 37 (wanaweza kusoma vifungu vyote) sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010(Cap 343 R.E.2010). Hakuna uchaguzi hapo mpaka mwezi Wa 10 kwenye uchaguzi Mkuu!
 
Pia wasome ibara ya 37 (wanaweza kusoma vifungu vyote) sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010(Cap 343 R.E.2010). Hakuna uchaguzi hapo mpaka mwezi Wa 10 kwenye uchaguzi Mkuu!

Mkuu hiyo sheria iko wapi.,nimeitafuta tangu jana sijaiona,tuwekee link tuione mkuu.
 
Back
Top Bottom