Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Moderators naomba msiunganishe uzi huu kwa kuwa una faida kwa watu wote kujua taratibu za usafiri wa ndege, ambao ATCL kwa makusudi imeamua kupotosha umma katika kile kinaitwa "damage control"
Kilichofanyika Mwanza hadi Diamond kuachwa ni jambo la kawaida katika usafiri wa ndege. Ni kwamba booking zinapofanywa kwa ajili ya safari ya ndege, huwa kama kuna abiria wengi basi shirika litabook zaidi ya uwezo wa ndege wa kubeba abiria. Hii hufanywa hivi kwa kuwa si watu wote wanao book kuondoka siku fulani wanaondoka siku hiyo. Ndege sio kama basi kwamba ikijaa wataacha kubook.
Sasa pale Mwanza kilichofanyika ni kwamba siku hiyo ATCL walikuwa wana abiria zaidi ya uwezo wa ndege. Hili linapotokea huwa watakaosafiri na ndege ni wale waliokuwa wa kwanza ku-check in - yaani first to check in first to travel.
Sasa Diamond hakuchelewa kufika airport kulingana na muda wa safari ya ndege. Alifika ndani ya muda unaotakiwa. Lakini kilichotokea ni kwamba ile idadi ya watu ambao ndege ingeweza kubeba ilikuwa imetimia. Hivyo Diamond na wengine ikabidi waachwe.
Sasa kosa ni la nani? Si kosa la Diamond wala ATCL. Kosa la ATCL hapa ni kuupotosha umma kwamba Diamond alichelewa. Hakuchelewa, bali walikuwa wana-overbooking hivyo wakachukua abiria waliocheck in kwanza. Kosa la Diamond ni kusema seat zao "ziliuzwa". Hapana, walichukuliwa wale waliocheck in kwanza.
Kawaida basi, ATCL walitakiwa kuwahudumia abiria wote ambao hawakuweza kusafiri kwa ajili ya overbooking. Walitakiwa hata wawape hoteli ya kulala hadi kesho yake, ambapo wangepewa fursa ya kwanza kusafiri na ndege inayofuata. Lakini ATCL hawakutaka kufanya hivyo, wakaamua kusema abiria ndio wamechelewa ili kukwepa lawama na gharama.
Sasa kama ATCL imeamua kutoa huduma bora kwa Watanzania, kwanza wawe wakweli, wasipotoshe umma na kukwepa uwajibikaji unaotokana na overbooking. Hilo ni jambo la kawaida na wao kama shirika la ndege wanajua walipaswa kuwafanyia nini Diamond na wengine waliokosa ndege ile kwa kuwa ilikuwa imejaa.
Na kwa watu wengine, kama unahisi kuna overbooking kutokana na route kuwa na watu wengi, ni vema uwahi sana kucheck in. NI jambo la kawaida kwa mashirika ya ndege kufanya overbooking, japo si jambo la kawaida kwa mashirika ya ndege kupotosha umma kwamba abiria walioachwa kwa overbooking walichelewa. Technically si kweli kwamba wanakuwa wamechelewa. Kwanza kama wangekuwa kweli wamechelewa wangelipishwa flight change au no show fee.
Kwa hiyo ATCL hawakumtendea haki Diamond, kwa kuwa wamemfanya aonekane ni muongo badala ya kuomba radhi kwamba hakusafiri kwa ajili ya suala la overbooking, na si kwamba "alichelewa", bali walichukua wale walio-check in mbele yake. Tunaelewa kwamba ATCL walitaka kufanya damage control kutokana na kauli za Diamond. Hata hivyo, huwezi kurekebisha kosa kwa kufanya kosa. Two wrongs do not make a right. Hata kama Diamond aliongea mambo kwa hasira, haiwapi ATCL haki ya kudanganya umma ili kufanya damage control. ATCL wangekanusha kuhusu seat za kina Diamond "kuuzwa" na kueleza ukweli.
Kuepuka lawama, ATCL wangeweza pia kumpa Diamond free upgrade ya Business Class, kwani hilo pia ni jambo la kawaida kunapokuwa na overbooking. Huenda hiyo ingekuwa win-win kwa ATCL na Diamond.
Kwa wale wanaojua Kiingereza;
The Reason Airlines Over-book Flights
Most airlines over-book their flights and accept bookings for more seats than are available in order to minimize their impact on the percentage of passengers who either don’t show up for the flight or who cancel their booking at the last-minute. Unfortunately, this business practice can sometimes backfire and inconvenience passengers if more individuals than expected show up for the flight.
Here's the best way for an airline to handle overbooked flights
The trouble comes when more passengers show up for a particular flight than there are available seats. In those situations, airlines need to have proactive mechanisms that treat customers fairly without breaking the bank.