Kuhusu SONGO SONGO Gas | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu SONGO SONGO Gas

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Keynes, Jan 16, 2011.

 1. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Jamani wana JF naomba michango yenu kuhusu ule ubadilishaji wa magari kutoka mfumo wa kutumia petroleum fuel kwenda kwenye gas uliokua unafanywa na TPDC umefikia wapi?
  Kama kuna mtu mwenye taarifa kamili tunaomba atuelimishe.

  My concerns.
  Matumizi ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje 60% ya matumizi yote hua inatumika kuagiza mafuta mazito ya kuendesha mitambo ikiwa ni pamoja na petrol kwa magari.
  JE SERIKALI SASA HAIONI WAKATI UMEFIKA WA KUJIKOMBOA KWA KUTUMIA GAS YETU?
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nenda BICO University of Dar es Salaam katika garage yao inaitwa BICO Garage opposite na jengo la Mama lishe, wanatoa hiyo huduma ya kubadili mfumo wa gari kutumia gas. BICO ni authorized agent wa TPDC kwa shughuli hiyo.
   
 3. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  nashukuru mkuu sasa nikishabadili mfumo wa gari yangu .....je vituo vya kujazia gas viko wapi??
   
 4. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kituo cha kujazia kipo Ubungo Maziwa, opposite na mitambo ya umeme ya TANESCO/DOWANS.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wakuu tunaomba nondo zaidi hapa. Je ni magari yote waweza fanya hivi? Je option ya pertol inakufa mojakwa moja au bado unaweza kuitumia?

  Mikoani ni wapi service hii ipo?
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Utashangaa umebadili mara wanaanza mgao wa gesi
   
 7. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  So far, ni magari yenye kutumia petrol ndo yanaweza kubadilishwa. Kinachofanyika ni kwamba unaongezwa mfumo mwingine wa kutumia gas. Mfumo wa petrol unabaki kama kawaida na utaendelea kufanya kazi bila kuathiriwa. Kinachotokea ni kwamba ukishawekewa mfumo wa gas, kuna kuwa na switch nadhani kwenye dashboard, gas/petrol. Kwa hiyo unakuwa na gas na petrol kwa pamoja. gas ikiisha una-switch kwenye petrol and vice versa. Kwa maelezo zaidi waone TPDC au fika BICO UDSM utapata melezo yote na gharama za kubadilisha mfumo.
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hii mada imekaa pahala pake. umetufungua akili.thanks
   
 9. m

  mzambia JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Na ukibadili tu mfumo watapandisha bei ya gesi hii ndo ccm bwana
   
 10. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mkuu ngereja inaonekana una ufahamu sana na haya mambo.
  Je kuna maadhara yoyote katika kubadilisha mfumo kwenye gari? Na je ni kwa nini serikali haifanyi uhamasishaji kwa wananchi ili kuweza kupunguza hela tunazopeleka nje kwa ajili ya kununua petroleum oil?
  Pia nadhani watanzania wanahitaji somo ili waweze kuagiza magari yanayotumia gas moja kwa moja kutoka nje.
  Naomba uniambie jina la gas inayotumika hapa kwetu maana sipo karibu na dar es salaam.....nadhani kuna majina specif za hizi gas ili kama mtu unanunua gari ujue unahitaji gari linalotumia gas ya aina gani?
  THANK YOU.
   
 11. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Gas inayotumika na inayotangazwa na TPDC ni natura gas ya kutoka Songosongo kitaalam inaitwa Compressed natural gas (CNG), hii ni aina ya gas ambayo ni tofauti na ile inayoitwa LPG (Liquefied petroleum gas). Kwa kuwa mimi siyo mtaalamu wa masuala ya petroli na gas, basi unaweza kujisomea mwenyewe kutoka kwenye wikipedia au google. Ila CNG ni gas ambayo hailipuki hata ikiachwa on has katika matumizi ya nyumbani. Lakini LPG ikiachwa ikivuja ikakutana na oxygeni, matatizo.
   
 12. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  yah, hata mimi wasiwasi wangu ni kwa nini serikali haihamasishi kubadilisha magari ili yanze kutumia gesi. nakumbuka nilimwona yona kilagane wa tpdc kama mara moja tu hivi kwenye TV akihamasisha na wakat huo ilikuwa ni maandalizi, walipozindua rasmi sijamsikia tena
   
 14. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Miss Judith usitarajie hayo maana kila shughuli itakayofanyika tanzania....viongozi badala ya kuweka maslahi ya nchi mbele wanaweka 10% mbele kwanza na kwa bahati mbaya viongozi wa tz hua wanakula 90% badala ya 10%.
  Vita iliyopo kwa sasa ni nani apewe tender ya jumla kuagiza petroleum fuel kutoka nje (Nadhani mnakumbuka mpango wa serikali wa kuagiza mafuta kwa single source) badala ya kuangalia matumizi mbadala kama vile mungu alivyotajalia hiyo gas. Hawawezi kufanya uhamasishaji maana wafadhili wa mafisadi wengi ndo wamiliki wa vituo vya mafuta.

  Nchi nyingine duniani ambazo zipo nyuma ya technolojia hua zinatumia natural resources zake kikamilifu ili kujiendeleza.
  Mfano netherland waligundua natural gas kwenye north sea miaka ya 70's mpaka leo ni matajiri na wanasambaza gas ulaya nzima.
  Sisi tuna laana gani kila tunachogundua ndani ya nchi yetu tunauzia wageni? watoto wetu watakuja kuishi kwenye nchi gani?
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Sikushauri kubadili mfumo wa gari yako pasipo kuwa na uhakika wa upatikanaji wa gas yenyewe. TPDC ni asasi ya kiserikali. Kama asasi nyingine yoyote ya serikalini, hawa jamaa hawana haraka kabisa na hii mambo ya maendeleo. Wanajua kusai MOU za kutafuta mafuta tu
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hakuna uhamasishaji maana hakuna Dowans hapo. Tunafanya kazi na low energy, how could we move into excitation state aliyoiona Albert Einsten?
   
 17. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  ukipenda pia unaweza kwe pale chuoni DIT na ulizia kilipo kituo cha vehicle CNG conversion kilipo na utapatiwa hii huduma pia.
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ngereja, asnte sana kwa taarifa hizi muhimu kwetu. Watanzania tukibadilisha mifumo ya magari yetu walau kwa asilimia 50 % ya magari yote basi tutaokoa sana mahitaji ya fedha za nchi za nje kwenda kuagizia mafuta.

  Faida yake nishilingi kupata nguvu zaidi, soko letu la ajira kuimarika na gharama ya uzalishazi kwa gesi hiyo nchi kuendelea kupungua kwa kadri ya kila gari litakalobadilisha mfumo wake kwenda huko toka kwa Petrol na Diesel ya kuagizwa kutoka Middle East.

  Lakini kwanza BIDCO itangulie kutoa elimu juu ya matumizi salama ya gesi hiyo kwenye magari, tahadhari za kuchukua na wao kujitangaza kibiashara kwenye vyombo vya habari nchini ili kasi ya kubadili mfumo uwe murua.

  Wana JF, mawazo zaidi hapa.
   
Loading...