Kuhusu panya road bado ngazi za juu za uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam hawapo serious

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
792
1,269
Hili janga ni kubwa kuliko mnavyofikiria kila siku kuna watu wanauliwa, wanatiwa vilema na kuibiwa mali zao lakini bado hakuna hatua madhubuti zilizo chukuliwa ili kudhibiti hilli janga

Mpaka sasa kamati ya ulinzi ya mkoa na wilaya zake wameshindwa kuweka network ya mawasiliano ili ikitokea wamevamia sehemu wakamatwe kiurahisi

Kwa mfano Leo hii panya road wanavamia nyumba ya jirani inasemekana huwa wanakuwa wengi hivyo itakuwa sio rahisi majirani kutoka na kuenda kutoa msaada

Msaada pekee ambao ungeweza kutolewa na jinarani ni kuwasiliana na vikosi vya polisi vilivyo karibu ili wawahi eneo la tukio kuwakamata hao panya road

Kwa maelezo ya waliovamiwa na panya road inathibishisha kabisa panya road wakiingia katika nyumba wanakaa kati ya dakika 20 hadi 30 huo mda unatosha kabisa kuwapigia polisi na kuwahi eneo la tukio ila mpaka sasa hizo namba hakuna

Jana mkuu wa mkoa umesema Dar imeongezewa polisi 300 sasa wataisadia vipi jamii wakati hakuna mawasiliano yoyote yanayounganisha hao polisi na wananchi kipindi cha usiku
 
Hili janga ni kubwa kuliko mnavyofikiria kila siku kuna watu wanauliwa, wanatiwa vilema na kuibiwa mali zao lakini bado hakuna hatua madhubuti zilizo chukuliwa ili kudhibiti hilli janga
Hawa hawawezi kuwa serious kwakuwa wao na familia zao wana security ya kutosha sisi wengine wametuacha tupambane na hali zetu na ndiyo maana wakifanya jambo wanataka tuwapongeze na kuwashukuru
 
Akili za nyumbu wanazijua wenyewe, watakuja kutetea wahalifu hapa eti ni haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom