kuduman201036
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 4,058
- 2,184
nasikia ni jennister na wizara yake hii ni kwa mujibu wa Mh sspeaker.
Nimekupata like kwa sababu uko sahihi sana... Wafanyakazi wenyewe wako kimya eti wanalaumu bunge!! Lissu as you have said it well ametoa ufafanuzi wa kufa mtu, Infact amemuibua Ndugai! But as expected wafanyakazi wako kimyaaa....Hii hoja Tundu Lissu ameifafanua vizuri na Ndugai naye amejitetea kwa kadiri anavyoona. Tusubiri serikali tuone wanakaza shingo au wataona soo. Nia haikuwa nzuri hata kidogo.
Hii ni fursa ya wananchi kujua ni watu gani watetezi wao, na wepi ni wasaliti wao. Japo nathubutu kusema watawala wa nchi hii wana bahati nzuri, kwa sababu % kubwa ya wananchi ni wajinga (uelewa wao ni mdogo kuhusu haki zao).
Je ni kazi ya bunge kutunga kanuni????Kweli kabisa Naunga mkono hoja asilimia mia moja. Hapa wawakilishi wetu bungeni ndiyo wa kulaumiwa' kwa nini wanakubali hizi kanuni kandamizi ambazo hazina tija kwa wastaafu? Hii inaonyesha jinsi gani wabunge wasivyo kuwa makini na sheria pamoja kanuni zizopitishwa kwenye chombo hicho! Labda zinapokuwa zinahusu masilahi yao tu! Mbona wao wabunge wakistaafu wanalipwa kiinua mgongo chao chote, tena bila masharti? Tunataka na wafanyakazi nao iwe hivyo hivyo mfanyakazi akiacha kazi apewe stahiki zake zote, bila kupangiwa masharti.