Kuhusu Mgombea mwenza wa UKAWA

Kuhusu Mgombea mwenza wa UKAWA

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Kumekua na taarifa za kupotosha kuhusu Mgombea mwenza wa UKAWA Mh.Juma Duni na kutaka kuleta propaganda za kupuuzi kuwadanganya Watanzania! Ifahamike kwamba Mgombea huyu anafanya kazi kubwa sana kupiga kampeni pamoja na baadhi ya Viongozi wa vyama washirika vya UKAWA kama Ndugu Issa Mohamedi M/kiti CHADEMA Zanzibar, na Viongozi wengine waandamizi wa CUF taifa. Kama tunavyoelewa kwa hali ya kisiasa iliyo wakati huu ambapo vyombo vingi vya habari vimekua haviripoti kwa makusudi matukio mengi ya UKAWA ikiwa ni pamoja na mikutano ya Mh Duni.Kwa wanaofuatilia vizuri ni kwamba Mh Duni anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha UKAWA wanashinda ushindi wa kishindo.

Pia ifahamike kua Kazi kubwa ya Mh Duni ni kuhakikisha kwamba kura zote za wanaCUF bara na visiwani zinaenda kwa wagombea wa vyama vinavyounda UKAWA maana ndicho chama alichikiwakilisha siku zote! Hakuna mwananchi asiyefahamu kwamba ni kwanini Mh Duni amejiunga CADEMA, kazi yake kubwa ni kuhakikisha maslahi ya CUF yanalindwa ndani ya UKAWA ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wagombea wote wa CUF ngazi zote walikosinamishwa wanaibuka kidedea.Mh Duni alijiunga CHADEMA ili kukidhi matakwa ya sheria ya Uchaguzi ili kuunganisha nguvu ya vyama vyote vya UKAWA.

Kuna watu humu wabapotosha kwamba Mh Duni katengwa kwenye kampeni na CHADEMA kitu ambacho ni uongo uliokubuhu na ni wa kupuuzia mbali! Ukweli ni kwamba Mh Duni yupo ndani ya kampeni kila siku ingawa baadhi ya vyombo vya habari havioneshi matukio hayo kwa sababu zao binafsi. Baadhi ya vyombo vya habari tukiacha Radio one, ITV na baadhi ya magazeti vinaona aibu ndio maana vinajaribu kuonesha japo kidogo tena kwa kuficha kampeni za Mgombea urais wa CHADEMA Mh Lowassa, sasa kama kwa Lowassa ni hivyo unafikiri kwa Mh Duni itakuaje?
 
Na jana alikuwa Dodoma huko vijijini anapiga kijiji kwa kijiji. Kata kwa kata, jimbo kwa jimbo
 
Duni anapiga campaign kma kawaida hawa jamaa wa lumumba ndo wazingua eti kajitoa, duni anapiga vijijin hukoo
 
Maccm yamepanic yamebaki kupiga propaganda za kijinga.
 
Duh! Hizi ni propaganda za kipuuzi aiseee? Hao mnaowasema ITV wanaonesha mpaka mikutano ya CHAUMA. Sasa inakuwaje mikutano ya Juma Duni Haji inashindwa kurushwa hewani? Pia kuna Channel Ten ambayo kila siku inaripoti habari za Lowasa.

Vipi kuhusu Juma Duni Haji? Then umesema kuwa Juma Duni Haji ameletwa ili kuhakikisha haki za CUF ndani ya UKAWA zinalindwa. Zitalindwaje sasa ilhali Juma Duni Haji si mwanachama tena wa CUF?

Tamko hili limeandaliwa na mtu mjinga kupita wote ndani ya CHADEMA
 
Muwe mnaangalia TV pia.. Juzi alikuwa Dodoma
 
eti ccm ni ileile mbele kwa mbele mtama mwaka huuu lazima mzikwe
l
e
 
Lizaboni

Wewe ni miongoni mwa wanaccm wanaopotosha kuhusu Mh Duni, Kichwani mwako unafahamu ni kwanini Mh Duni alijiunga CHADEMA! Kila nilichoandika ndio ukweli halisi na Kama kuna kiingine elezea humu usipotoshe.
 
Last edited by a moderator:
Lkn inafurahisha sana mkuu, wanapojaribu kupotosha, wananchi wameshagundua hila zao, hawayumbi. Maeneo mengi nimeshuhudia, hivyo mbinu zao haziwasaidii kwa asilimia kubwa.
 
Lizaboni

Mmeishiwa hoja mmebaki kubwabwaja tu, subirini Oct 25 mtanyooka tu. Tulijiandikisha kwenye BVR kwa kazi moja tu NAYO NI kuitoa CCM magogoni.
 
Babu Duni huwa anaonyeshwa japo mara chache ila kimsingi ni kwamba yupo Dom na anapiga kampeni haijawahi tokea mpaka wana Dom wamenyoosha mikono juu kukubali kwama ni mabadiliko tumaana hakuna namna.

Bravo Babu Duni

.viva ukawa
 
Duni Hadji ana mission kubwa ya kuipatia Zanzibar mamlaka kamili, hivyo hawezi kujitoa sasa hata mkimtemea mate usoni. Hawezi jitoa..! Ibara 37(5) ya katiba ya JMT inamuahidi Babu Duni urais.

Kwa kuzingatia ukweli kuwa japo maradhi ya mgombea urais si ya kumtoa duniani Leo au kesho ila itafika muda mahakama itamtaja kuwa hana sifa ya kuendelea kushika wadhifa huo. Hatua hiyo itamfanya Duni akabidhiwe mikoba rasmi. Hapo mission itakuwa complished.
 
Kumekua na taarifa za kupotosha kuhusu Mgombea mwenza wa UKAWA Mh.Juma Duni na kutaka kuleta propaganda za kupuuzi kuwadanganya Watanzania! Ifahamike kwamba Mgombea huyu anafanya kazi kubwa sana kupiga kampeni pamoja na baadhi ya Viongozi wa vyama washirika vya UKAWA kama Ndugu Issa Mohamedi M/kiti CHADEMA Zanzibar, na Viongozi wengine waandamizi wa CUF taifa. Kama tunavyoelewa kwa hali ya kisiasa iliyo wakati huu ambapo vyombo vingi vya habari vimekua haviripoti kwa makusudi matukio mengi ya UKAWA ikiwa ni pamoja na mikutano ya Mh Duni.Kwa wanaofuatilia vizuri ni kwamba Mh Duni anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha UKAWA wanashinda ushindi wa kishindo.

Pia ifahamike kua Kazi kubwa ya Mh Duni ni kuhakikisha kwamba kura zote za wanaCUF bara na visiwani zinaenda kwa wagombea wa vyama vinavyounda UKAWA maana ndicho chama alichikiwakilisha siku zote! Hakuna mwananchi asiyefahamu kwamba ni kwanini Mh Duni amejiunga CADEMA, kazi yake kubwa ni kuhakikisha maslahi ya CUF yanalindwa ndani ya UKAWA ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wagombea wote wa CUF ngazi zote walikosinamishwa wanaibuka kidedea.Mh Duni alijiunga CHADEMA ili kukidhi matakwa ya sheria ya Uchaguzi ili kuunganisha nguvu ya vyama vyote vya UKAWA.

Kuna watu humu wabapotosha kwamba Mh Duni katengwa kwenye kampeni na CHADEMA kitu ambacho ni uongo uliokubuhu na ni wa kupuuzia mbali! Ukweli ni kwamba Mh Duni yupo ndani ya kampeni kila siku ingawa baadhi ya vyombo vya habari havioneshi matukio hayo kwa sababu zao binafsi. Baadhi ya vyombo vya habari tukiacha Radio one, ITV na baadhi ya magazeti vinaona aibu ndio maana vinajaribu kuonesha japo kidogo tena kwa kuficha kampeni za Mgombea urais wa CHADEMA Mh Lowassa, sasa kama kwa Lowassa ni hivyo unafikiri kwa Mh Duni itakuaje?

Acha porojo tuoneshe kampeni za Duni juzi jana na leo atakua wapi.hiyo ITV yenu pia haioneshi duni anafanya nini.Duni kasusa
 
Inasemekana maalim seif kamtanguliza juma duni ukawa ili apate uenyekiti wa cuf kirahisi
 
Acha porojo tuoneshe kampeni za Duni juzi jana na leo atakua wapi.hiyo ITV yenu pia haioneshi duni anafanya nini.Duni kasusa
Wewe kama nani humu? Utafahamu vipi kampeni za Mh Duni ilihali hazikuhusu? Huwezi kufuatilia kampeni za Duni zaidi ya kusubiri kuandika habari za kupotosha humu? Kwa vijana wanaomjua Duni hawawezi kuuliza ujinga huo humu.
 
Back
Top Bottom