Kuhusu mashine za EFD

ndunajr

Senior Member
Apr 28, 2015
174
191
Habarini wana jamvi,
kwa kuwa naamini jamvi hili ni jamvi makini na kwa kuwa najua hapa ni mahala pekee pa kupata misaada mbali mbali ya kujifunza,kupata uelewa na ustaarabu.

Naomba kuuliza swali, mimi ni mjasilia mali na kwa sasa nataka kufungua duka langu la soda za jumla hasa pepsi.

Hofu inakuja pale kwenye matumizi ya mashine za EFD nikiwa naamini kabisa TRA lazima wanitake kutumia. Mfano kreti ya soda moja nanunua shilingi 9400 kutoka pepsi wenyewe na mimi nitauza shilingi 10,000.

Sasa katika makato ya asilimia 18 kupitia risiti ya EFD mimi faida yangu nitaipateje au kinachofanyika ni nini hasa, makato yanakuaje??? Yani naomba tu kusaidiwa pasi na mizaha na kebehi.[HASHTAG]#asubuhinjema[/HASHTAG]
 
Eeh Ndugu kuwa makini sana na hizo machine ukifanya mchezo itakata mtaji wako wote.Soda unanunua sh 9,400/= unauza sh 10,000/= hapo faida bila ya Tra ni sh 600/= ss hapo pana 18% ya Tra...kuwa makini kabla hujaamua
 
Back
Top Bottom