Kuhusu Majukumu ya kazi ya Waziri mkuu na makamu wa rais

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,034
1,792
Habari zenu Wakuu,

Nimepata kusikia kuwa baadhi ya Mataifa makubwa yakiwa na Waziri mkuu basi Makamu wa raisi hayupo au akiwepo makamu wa raisi basi waziri mkuu hayupo kwa hiyo naombeni kujua tu kazi kubwa ya waziri mkuu na makamu wa raisi ni nini au kuna mwingiliano wa kazi zao (kufanana)?

Ahsanteni
 
hilo linategemea mambo makuu mawili 1. aina ya serikali ( monarch) ambayo mwenye mamlaka kiutendaji ni waziri mkuu, serikali za aina hii hazina Rais wala Makamu wa Rais 2. Katiba, katiba za nchi mbalimbali, ndo zina ruhusu nani awe nani, mfano Kenya hawana waziri mkuu, Tanzania katiba inamtaja waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali
 
Ahsante sana kwa hiyo ina maana hawa wawili huwa kila mti ana kazi yake (haziingiliani)?
 
hilo linategemea mambo makuu mawili 1. aina ya serikali ( monarch) ambayo mwenye mamlaka kiutendaji ni waziri mkuu, serikali za aina hii hazina Rais wala Makamu wa Rais 2. Katiba, katiba za nchi mbalimbali, ndo zina ruhusu nani awe nani, mfano Kenya hawana waziri mkuu, Tanzania katiba inamtaja waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali

Hujamwelewa vizuri. Nadhani yeye anazungumzia Indian menu ambapo wana Rais na Waziri mkuu bila makamu wa Rais na American menu ambapo wana Rais na makamu wa rais bila Waziri mkuu. Hiyo ingine ni British menu
 
Sisi tz tumeiga mfumo wa Urusi na Uchina. Ila kwa tz makamu wa rais hana majukumu yaliyo wazi, kwa waziri mkuu ni bize kweli kweli hasa kipindi cha bunge ndio kiongozi wa kuitetetea serikali humo mjengoni.
 
Ahsante sana kwa kujua tatizo langu hapo ndo panaponichanganya Mkuu
 
Kuhusu makamu wa rais kweli sijaona kazi ya maana inayo muwajibisha zaidi ya kungua miradi na kushiriki makongamano, labda ni zawadi kwa upande wa pili maana awamu hizi makamu wanatoka kule.
 
Lengo ni kuhakikisha mmoja wa viongozi wakubwa wa JMT (Rais na Makamu wake) wanatoka pande zote za muungano. Mmoja akitokea Tanganyika, mwingine atokee Zanzibar.

Zanzibar wana serikali yao. Kwa hiyo Waziri Mkuu, anasimamia shughuli za serikali hasa upande wa Tanganyika. Japo katiba haisemi hivyo moja kwa moja.
 
Habari zenu Wakuu, nimepata kusikia kuwa baadhi ya Mataifa makubwa yakiwa na Waziri mkuu basi Makamu wa raisi hayupo au akiwepo makamu wa raisi basi waziri mkuu hayupo kwa hiyo naombeni kujua tu kazi kubwa ya waziri mkuu na makamu wa raisi ni nini au kuna mwingiliano wa kazi zao (kufanana)? Ahsanteni
Mimi nadhani uwepo wa Makamu wa Raisi ni ili kuleta usawa wa pande mbili za Muungano; kwamba Raisi akitoka bara makamu anatoka visiwani. Kuhusu waziri mkuu huyu nadhani ni mtendaji wa bara, visiwani hana kazi kule
 
Sisi tz tumeiga mfumo wa Urusi na Uchina. Ila kwa tz makamu wa rais hana majukumu yaliyo wazi, kwa waziri mkuu ni bize kweli kweli hasa kipindi cha bunge ndio kiongozi wa kuitetetea serikali humo mjengoni.
For ours, VP symbolises presence of Zanzibar in the Union Government, period. Virtually does not have specific role. PM is right hand assistant to the President with full executive mandate to supervise performance of Government hierarchy. The President is the supreme leader with full executive powers over both the country and state.
 
Does PM has any role to play regarding Zanzibar?
 
Kwa Tanzania Makamu wa Rais majukumu yake hayana nguvu, ila umuhimu wake ni pale ikitokea Rais amefariki ghafla, yeye ndo ana take over
 
Ukiangalia mfumo wetu wa serikali, rais na. Makamu wake ndio viongozi wakuu wa nchi, waziri mkuu na raisi wa Zanzibar ndio wakuu waTanganyika na Zanzibar. Hili la waziri mkuu haliwekwi wazi lakini logically cheo chake kinaishia kigamboni huko majini hana chake.

Hivyo WM majukumu yake ni kusimamia shughuli zote za serikali na bungeni
 
Kwa Tanzania kila kitu kinawezekana ndiyo maana tuna maraisi wawili, makamu wa maraisi watatu, mawaziri wakuu wawili, mabunge mawili Serikali mbili na kuna wakati tulikuwa tuna mrema kama naibu waziri mkuu
 
Back
Top Bottom