Kuhusu Magari Yanayojiendesha

Kuhusu Magari Yanayojiendesha

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Huenda hujaamua kudadisi kwa undani Muelekeo wa Dunia yetu na mustakabali wake lakini nipende kukujuza kwamba mambo yanakwenda kwa kasi KULIKO unavyoweza kudhani kulinganag na Teknolojia ya elektroniki na megatonic

Nakukumbusha kwamba tayari dunia ina ndege zisizo na marubani, tayari kuna maroboti yanayofanya kazi kama binadamu na sasa HUENDA HATA KUSIWE NA HAJA YA NCHI KUWA NA MAJESHI DUNIANI kutokana na Digitized Military Technology

Leo naanza na Hii ya magari yasiyo na dereve )Self Driving Cars)


Kampuni ya Apple imetangaza mipango yake ya kuunda magari yanayojiendesha. Kampuni hiyo imekiri hayo kwa mara ya kwanza kwenye barua kwa wasimamizi wa uchukuzi Marekani.

Apple imesema inafurahishwa sana na uwezo wa mifumo ya kutumia kompyuta kwenye maeneo mengi, "ikiwemo uchukuzi".

Hata hivyo kampuni ya Ford, ambayo pia ina mipango ya kuunda magari kama hayo, ambayo inadhamiria yataweza kutumiwa barabarani mwaka 2021, ilisema inaendelea na mpango wake ikifahamu kwamba Apple nao wanaunda magari kama hayo.
upload_2017-7-5_8-37-19.jpeg


Magari hayo yanaongozwa kwa kutumia kompyuta pekee, huku yakiwa na uwezo mkubwa wa kuepuka au kutosababisha ajali barabarani.............Magari hayo ambayo husafiri kwa hadi kasi ya kilomia 16.1 kwa saa, yanaelekezwa na kompyuta ikiwa ni pamoja na kujiengesha pasi na wasi wowote

Semi-autonomous vehicles already park themselves, hit the brakes to avoid fender benders, keep themselves in the correct lane on the highway, and can even be summoned to their drivers.
upload_2017-7-5_8-37-19.jpeg
upload_2017-7-5_8-37-37.jpeg


Kimuonekano, magari haya yanatofautiana na magari mengine kwa kuwa na kifaa cha hali ya juu kinachosaidia magari hayo kutambua maeneo yaani unaweza kuyaita ukiwa popote panapofikika na yakaja kama unamuekekeza binadamu (GIS)

upload_2017-7-5_8-37-37.jpeg


Magari haya yanabeba watu wanne na hayana usukani wala breki, kadhalika yana kamera ya utambuzi wa zaidi ya mita 100 mbele ili kubaini tuko lisilo la kawaida...Hata hivyo wakatiI wataalamu wanabuni magari yasiyo na dereva waliamini kuwa huenda ikawa ni suluhisho la ajali za barabarani na kuwaondolea watu usumbufu wa kujiendesha, lakini kangaroo wameonekana kuyapa wakati mgumu kwani wanaporuka huonekana wako mbali na wakitua huonekana wapo karibu ...........hata hivyo utafiti unaendelea kubuni kamera maalum za kutambua mienendo ya Kangaroo
Zinazosomwa | KANGAROO HUYACHANGANYA MAGARI YANAYOJIENDESHA

Kampuni inayounda magari hayo imesema kuna manufaa mengi ambayo yatapatikana kijamii kutoka kwa magari yanayojiendesha. mojawapo ni kwamba KWA MIONGO IJAYO HUENDA WATU WASIHITAJI KUMILIKI MAGARI maana Self Driving Car zitakidhi mahitaji ya wengi na kuwapunguzi adha za kiuchumi kama matengenezo na Mafuta (If you can get milk why keep a cow.?)

Kwa taarifa yako ni kwamba hata mmiliki wa kampuni kubwa duniani ya uchukuzi almaarufu UBBER hamiliki hata GARI MOJA BINAFSI ZAIDI YA kutegemea Uber na hicho kinakwenda kutokea

Nchini Uingereza, gari la kujiendesha lilifanyiwa majaribio Milton Keynes majira ya joto, na majaribio zaidi yamepangiwa kufanyika London karibuni.
 
Miaka ya mbeleni kampuni ya PEASI kutoka TANZANIA imesema itatengeneza BAISKERI inayojichalanga yenyewe
 
Back
Top Bottom