Kuhusu kutafuta hifadhi kwa viongozi wa upinzani katika mataifa yanayoheshimu uhuru na haki ya kuishi

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Na Mwl, John Pambalu

Mwaka 2015 baada ya uchaguzi uliompa ushindi Mhe. Magufuli. Aliyekuwa Mkt wa Chadema mkoa wa Geita na mgombea ubunge Jimbo la Busanda marehemu Alphonce Mawazo. Alipokea taarifa za vitisho juu ya uhai wake, hakuamua kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini, siku chache baadaye aliuawa kikatili mchana kweupe mita chache kutoka kituo cha polisi huku jimboni Busanda mkoani Geita.

Kiongozi mwingine wa Chadema na mkosoaji wa serikali ya awamu ya tano Ben Saanane alipokea taarifa za kutishia uhai wake. Hakuona sababu za kukimbia nchi akaendelea kubaki nchini. Siku chache baadaye alipotea na mpaka leo hakuna anayejua yuko wapi Ben Saanane.

Mwaka 2017 Mhe. Tundu Lissu alipokea vitisho juu ya uhai wake. Yeye alijaliwa kujua mpaka namba za gari za waliokuwa wakimfatilia. Lissu hakuona umuhimu wa kutafuta hifadhi. Siku chache baadaye alishambuliwa kwa risasi za moto kwenye nyumba za serikali zenye ulinzi full-time. Mpaka leo hata hao wanaodai nchi iko swali hawajawahi kusema ni wakina nani walimshambulia Lissu.

Nataka kusema nini?.

Wapinzani wanaotishiwa uhai wao kuamua kuondoka nchini kutafuta hifadhi ni hekima ya kimungu. Yusuph alimkimbiza Bethlehem mtoto Yesu kukwepa tishio la kupoteza uhai wa mtoto Yesu baada ya mfalme Herode kutangaza watoto wote wa kiume wauawe.

Mhe. Lissu na Lema ambao wameondoka nchini kutafuta hifadhi nje ya nchini wanastahili pongezi hata Yesu alipelekwa uhamishoni ili abaki salama.

Wasalaam
John Pambalu
Mkt Bavicha taifa
maxresdefault.jpg
 
HAKIKA HII NCHI SI SALAMA TENA WALA SI KISIWA CHA AMANI KAMA ILIVYOJIPAMBANUA NA WAASISI WQ TAIFA LETU.

Rais wa kula FEKI anaroho ya ajabu sna akili za Hovyo sana.
Mwalimu Nyerere aliwataja MAADUI WAKUU WATATU WA TAIFA LETU KUWA.
UMASIKINI
UJINGA.
MARADHI.

Hivi vyote jiwe HAVIONI anakwenda kupambana KUUA VIONGOZI WA UPINZANI.

HAKIKA MKAPA HUKO ULIKO UMETUKOSEA SANA WATANZANIA
hatukuzoea kuishi hivi.

Saruji ni 35000/=
ACHA TUISOME NAMBA.
CCM HOYE.
 
Kuomba msaada kwa watu wema ni jambo la kawaida .
Kwenye Biblia kuna mfamo wa Msamaria mwema .
Huyo msamaria mwema hakuwa Myahudi lakini alimsaidia myahudi aliyevamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa sana. Ndugu zake hawakuwa na roho ya kumsaidia na walimpita kwa mbali sana huku wakiwa wanaendelea na ibada zao kama kawaida. Alisaidiwa na Mtu wa nchi nyingine ambapo waliishi wasamaria.

Lakini pia tujiulize kama Tunaomba msaada kwa Mungu rusiyemuona ,inakuwaje tushindwe kuwaomba msaada binadam tunaowaona ambao wameumbwa na Mungu na kupewa roho za huruma?

Dunia hii tangu kumbwa haijawahi kukosa Viumbe au binadam wa kuwasaidia wale wanaoonewa .
Na watu wanaoonea wenzao hawajawahi kuwaonea muda wote bila kutokea nguvu ya kuwashinda waoneaji na sehemu yao ikabaki kuwa historia Mbaya.
Utumwa ulikuja na kupita japo ulinufaisha watawala na matajiri wa enzi hizo.
Ukoloni ulikuja na kupita japo uliwanufaisha matajiri na watawala.

Udikteta bado unaisumbua dunia na watu wasio na nguvu ndio wanaopata shida lakini wanaonufaika ni watawala na familia zao na marafiki zao. Ukiwaangalia wabunge wa CCM pale hungeni utajiuliza wapo kwa manufaa ya nani zaidi ya wao na familia zao. Walijiwekea sheria ya kujilipa mishahara mikubwa na sasa bei ya sementi imepanda wao haiwezi kuwaumiza mana mshahara mili.12 atanunua tu sementi . Wanateua marafiki na ndugu zao kuwa kwenye nafasi zenye mishahara mikubwa ili wasiumize na uhaba wa fedha mitaani na biashara zikiyumba wao haziwahusu mana mishahara yao inawakidhi mahitaji yao . Wanaoumia ni wale wazalendo wanolipwa Laki nne kwa mwezi lakini hawaruhusiwi kudai nyongeza mana wanaokalia madaraka wana madaraka ya kuwafukuza kazi kama mbwa bila hata kuwalipa Chochote.
Nchi ya Kijamaa inayotawaliwa na mabepari.

Mungu ndiye aliyebakia kuliokoa Taifa hili mana wanawaumiza Wengine wao wana mabunduki na hawaogopi sheria yoyote mana wapo juu ya sheria kama waliopitindisha sheria za Ubunge wa viti maalumu.
Nchi ya watawala wasiofuata sheria Bali wanawaswaga watumwa wao kufuata sheria Kali kwa vitisho
 
Na Nyie Bavicha kaeni mjitafakari.
Muepuke unafiki na usaliti ndio maana waovu wanawafikia kwa urahisi na kuwashinda .

Mtangulizeni Mungu Mbele. Kwa sasa Bila Mungu Chadema mtasambaratika kabisa. Mwenyekiti wenu wa Chama ni Mlevi,mzinzi ,Tapeli, Mbinafsi, Mwizi, Mlaghai, ana roho Mbaya . Mbaguzi ,Mdini, mkabila halafu mnategemea mtaacha kupigwa kwana laana ya walioumizwa Mwenyekiti Mbowe.

Tubuni Nyie Chadema mumkabidhi Mungu hii vita ,itaisha mapema na njia itaonekana. Maana CCM wao wamejiona wako sawa na mungu na Mungu muumba hawezi kuwafanya chociote mana hii nchi ni ya kwao waliiumba wao na Mali zake zote wameziweka Tanzania kwa juhudi zao. Hawa hamuwezi kupambana nao kirahisi bila Nyie kujishusha na kumwachia Mungu ajidhihirishe yaye mwenyewe. Hata Lisu anaonekana yupo shallow sana kwenye Imani hata za kiasili anafikiri dunia inaongozwa kwa juhudi bila roho zisizoonekana.

Kuna Mungu ndiye anayeweza kuibadili nchi kwa wakati anaotaka yeye bila watu kupenda au kutopenda . Mungu akiamua watu wamkatae mtu watamkataa. Mungu anaweza akayafanya maisha yakawa magumu mpaka kila mtu akasema sasa basi.
Lakini Juhudi zenu Bavicha Bila kushika dini mnazoamini kwa dhata mkaishia kukesha kwenye mabaa na wanawake na matusi kwa viaongozi wa nchi mtapata tabu sana.
Jishusheni kwa Mungu.

Swalini sana na kukesha mkimuomba Mungu aonyeshe nijia.
Kuweni wa kweli sio wanafiki.
Msiwarukane wengine hasa wenye mamlaka na watu wazima.
Muache Chuki na ubinafsi.

Haki siku zote inatokana na kumcha Mungu. Mtu asiyemjua Mungu anatenda haki pale anapoamua kwa manufaa yake lakini sio kwa matakwa ya sheria. Tumeona nafasi za viti maalum vya ubunge na ubunge wenyewe kupatikana kinyume cha sheria na haki. Yaani Bunge litakua ni la watu waliodhulumu nchi.

Simeni Albadiri kila kona ya nchi . Kodi zetu zinaliwa na watu waliodhulumu na kukiuka sheria . Tunakamuliwa kodi ilu wezi wakazile. Huu ni wizi na dhulma kubwa .

Inashughulikiwa kidini na kimila. Achaneni na kukimbia kimbia tu bila kujua kuwa hii ni roho iliyojiinua kwenye Taifa hili ambalo lina chama kilichoingia mkataba na Lusifer tangu mwanzo wake hivyo sio rahisi kupambana nacho bila Mungu kuingilia kati.
Hata JPM alipoingia alijaribu kupamba nw mfumo CCM lakini ameshindwa kabisa na kurudi nyuma zaidi na sasa nchi imepoteza hata umoja wake wa mwanzo na watu kuishi kwa uadui mkubwa huku kila mmoja akimwombea mwenzake mabaya.
 
MaCCM yanajiongelsha sana kwa kua Magufuli kavimba kukosa tena nyama ya Lissu.
 
HAKIKA HII NCHI SI SALAMA TENA WALA SI KISIWA CHA AMANI KAMA ILIVYOJIPAMBANUA NA WAASISI WQ TAIFA LETU.

Rais wa kula FEKI anaroho ya ajabu sna akili za Hovyo sana.
Mwalimu Nyerere aliwataja MAADUI WAKUU WATATU WA TAIFA LETU KUWA.
UMASIKINI
UJINGA.
MARADHI.

Hivi vyote jiwe HAVIONI anakwenda kupambana KUUA VIONGOZI WA UPINZANI.

HAKIKA MKAPA HUKO ULIKO UMETUKOSEA SANA WATANZANIA
hatukuzoea kuishi hivi.

Saruji ni 35000/=
ACHA TUISOME NAMBA.
CCM HOYE.

Hio 35000 ya kuwauzia wapinzani ukiwa na gamba la kijani utauziwa bei ya kiwandani
 
Aisee wewe utakuwa unafumuliwa marinda alafu lazima utakuwa kiongozi wa misukule hapo Lumumba.
 
Hiyo mifano inadhihirisha jinsi viongozi wa upinzani wanavyotakiwa kutafuta mahala salama pa kwenda kuishi.
 
Walipe Madeni ya Watu,
uhamishoni wa Wapi huu ujanja waache. Tundu Lissu na Lema watafutwe wana kipya gani zaidi ya kupgopa Madeni wanayao daiwa.
 
Kuomba msaada kwa watu wema ni jambo la kawaida .
Kwenye Biblia kuna mfamo wa Msamaria mwema .
Huyo msamaria mwema hakuwa Myahudi lakini alimsaidia myahudi aliyevamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa sana. Ndugu zake hawakuwa na roho ya kumsaidia na walimpita kwa mbali sana huku wakiwa wanaendelea na ibada zao kama kawaida. Alisaidiwa na Mtu wa nchi nyingine ambapo waliishi wasamaria.

Lakini pia tujiulize kama Tunaomba msaada kwa Mungu rusiyemuona ,inakuwaje tushindwe kuwaomba msaada binadam tunaowaona ambao wameumbwa na Mungu na kupewa roho za huruma?

Dunia hii tangu kumbwa haijawahi kukosa Viumbe au binadam wa kuwasaidia wale wanaoonewa .
Na watu wanaoonea wenzao hawajawahi kuwaonea muda wote bila kutokea nguvu ya kuwashinda waoneaji na sehemu yao ikabaki kuwa historia Mbaya.
Utumwa ulikuja na kupita japo ulinufaisha watawala na matajiri wa enzi hizo.
Ukoloni ulikuja na kupita japo uliwanufaisha matajiri na watawala.

Udikteta bado unaisumbua dunia na watu wasio na nguvu ndio wanaopata shida lakini wanaonufaika ni watawala na familia zao na marafiki zao. Ukiwaangalia wabunge wa CCM pale hungeni utajiuliza wapo kwa manufaa ya nani zaidi ya wao na familia zao. Walijiwekea sheria ya kujilipa mishahara mikubwa na sasa bei ya sementi imepanda wao haiwezi kuwaumiza mana mshahara mili.12 atanunua tu sementi . Wanateua marafiki na ndugu zao kuwa kwenye nafasi zenye mishahara mikubwa ili wasiumize na uhaba wa fedha mitaani na biashara zikiyumba wao haziwahusu mana mishahara yao inawakidhi mahitaji yao . Wanaoumia ni wale wazalendo wanolipwa Laki nne kwa mwezi lakini hawaruhusiwi kudai nyongeza mana wanaokalia madaraka wana madaraka ya kuwafukuza kazi kama mbwa bila hata kuwalipa Chochote.
Nchi ya Kijamaa inayotawaliwa na mabepari.

Mungu ndiye aliyebakia kuliokoa Taifa hili mana wanawaumiza Wengine wao wana mabunduki na hawaogopi sheria yoyote mana wapo juu ya sheria kama waliopitindisha sheria za Ubunge wa viti maalumu.
Nchi ya watawala wasiofuata sheria Bali wanawaswaga watumwa wao kufuata sheria Kali kwa vitisho
Wewe upo Tanzania umeona wanachokisimulia .

Eti mtu analalamika anawindwa na vitisho kedekede.

Hao Wanakwepa kulipa madeni ya watu wanatafuta huruma ya kupata msamaha.

Tundusi alikopa bilioni 3, Lema Milioni 950 kwa ajili ya Kampeni na walitoa rushwaaa saaaanaa. Baada ya kupigwa ndo hayo yameanza kuwachanganya wada wao.

Please lipeni Madeni ya Watu.
 
Tutubu kwa dhambi gani tulioifanya ?, mbona kutowaambia ccm watubu kwa maovu ambayo wamekuwa wakifanya ?, au nawe ni mnufaika ?,
ni haki ipi ambayo una reffer ya kwamba sisi tunapaswa kuitafuta na kwa njia gani sahihi kwako ?, usihukumu kwa hila usijehukumiwa, yote haya wanayofanya ccm na serikali yake kweli huyaoni au unajitia upofu ??!!, natamani kuona ukiyasema hayo dhidi ya ccm ambao kimsingi naamini ndio wanastahili kutubu kwa hakika, Amani ni tunda la Haki,
Wasalaam
 
Hiyo kwa Tz, ni katika kutafuta KIKI, hela na kuchumia tumbo, kina Lipumba, Zitto, Mzee wa Ubwabwa, Maalim Seif, Mbowe, n.k. mbona wapo??!!!
 
Back
Top Bottom