Kuhusu Kufunga Mfumo wa Gas (CNG) Kwenye Subaru Forester.

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,692
Reaction score
2,098
Kwema Wakuu,

Mwezi uliopita nilihama rasmi kutoka kutumia RAV4 mpaka Subaru Forester ya 2011. RAV4 nliokua nikitumia ni "Kili time" ya mwaka 2000, engine 1ZZ, CC 1770, front wheel.

Sasa nimekuja kwenye Subaru, CC 2000 full time 4wd naona kama mambo hayaendi hivi kwa upande wangu. Yaan mazoea mabaya mafuta niliyokua naweka Kwa RAV4 nimeongeza consumption kwa kama 40% to 50% hapo ndio kwanza imported, likianza kuchoka si ndo itakua shida zaid?

Sina mishe nyingi sana, wala sio mzee wa masafa marefu. Sijatoka Dar Kwa Self Drive mwaka wa 7 labda huu. Makazi Makumbusho na kazi Posta, muda wote foleni hivyo hata speed 80 kama sio darajani pale tanzanite mara moja moja sikumbuki lini nilishawahi kuendesha hii speed.

Sasa naona nifunge mfumo wa CNG, nasoma promo zake kua unaokoa gharama za mafuta kwa % nyingi tu, mnanishauri vipi Wataalam? Ita athiri Chochote kwenye gari labda? Kuna Magari sio suitable labda kufunga huu Mfumo?

Na nikifunga nikaona ni miyeyusho si nikiutoa gari itarud kua poa tu kama mwanzo? Au ndio "nikishaharibu" ndo mwanzo huo nitegemee kua mgeni wa kudumu wa mafundi Subaru kila Leo?

Msaada wenu muhimu wakuu,
🙏🏾

NB;
Ukifunga CNG Ikapata Ajali (Kuungua Labda), Bima watalipa?

Au inabidi uwataarifu kabla ili mkubaliane upya terms na premium?
 
Aisee ungekuwa karibu na Mimi ningekupiga Kofi ili kama kichwani mwako kuna wazo Hilo la kufunga gesi liondoke!
Wewe umesikia wapi Subaru inafungwa mfumo wa gesi? Watanzania mbona mnakosa elimu hata hizi ndogo juu ya magari?
1) CNG ni mfumo wa kishamba Sana hata Huko ulaya hautumiki
2) CNG inatumika kwenye Bajaj Tu
3 CNG ni zaidi ya bomu
Wazungu baada ya kuona CNG ni UJINGA walianzisha magari chotara ( hybrid car) kama umeshindwa kumiliki Subaru tafuta IST itakusaidia .
Mimi Nina Subaru forester XT kama ni ishu ya fuel consumption huku ndiyo balaa lkn najitahidi Sana kufanya kuepuka safari zisizokuwa na tija. Kama huwezi kumiliki Hilo gari uza nunua IST
 
Subaru nyingi tu zimefungwa. Nyingi sana. So hilo swali ni irrelevant. Ungesema tu hushauri mtu kufunga kwa sababu..... Taja.
 
Mkuu,
Ahsante Kwa maoni. Nimeona umetaja sababu tatu,
1) Ushamba
2) Kwenye Bajaj tu
3) Bomu.

Niongezee hata technical reason ya huu mfumo kutokua mzuri Mkuu. Inawezekana kuna sababu ya Wazungu kuukataa labda hiyo Gas kwao ni adimu au gharama.
 
Yes mkuu,
Technical reasons zitasaidia zaid uelewa.

Wafungaji wenyewe nimewacheki wanasema mfumo hauna shida, but perhaps wako kibiashara zaidi ndo nikaona nichek na wataalam wa humu.
 
Mkuu hongera kwa chuma iyo. CNG tunaibania Forester bwana, maana ukifunga kuna power loss kubwa sana ukiwa kwenye CNG mode, power loss utaiona kwenye kuovertake (sema umesema sio mtu wa highway), kupanda kilima au ukibeba mzigo mkubwa (even watu wanene kuanzia abiria watatu).

Kuna mtu alishawahi sema pia humu issue ya engine wear. Kwasababu Petrol ina additives inayofanya iwe na lubricating properties wakati CNG haina.

Pia kuongeza mtungi wa gesi, kule nyuma ukiwa kwenye petrol mode inamaanisha consumption itakua kubwa zaidi, mfano gesi imeisha, ila sio issue sana vituo vipp vingi hapa Mjini.

Pia angalia issue za ECU, na sensor maana gari ipo tunned kufanya combustion ya petrol leo ikikutana na CNG kuna possibility ya kuzingua.

Ila faida pia zipo mfano lengo kuu kusave mafuta. Ina save sana.

Pia ni engine model gani? Kama ni FB20 ile ya cc2000 issue ya valve itabidi uifanyie modification.
 
Mkuu hongera kwa chuma iyo. CNG tunaibania Forester bwana, maana ukifunga kuna power loss kubwa sana ukiwa kwenye CNG mode, power loss utaiona kwenye kuovertake (sema umesema sio mtu wa highway), kupanda kilima au ukibeba mzigo mkubwa (even watu wanene kuanzia abiria watatu).

Kuna mtu alishawahi sema pia humu issue ya engine wear. Kwasababu Petrol ina additives inayofanya iwe na lubricating properties wakati CNG haina.

Pia kuongeza mtungi wa gesi, kule nyuma ukiwa kwenye petrol mode inamaanisha consumption itakua kubwa zaidi, mfano gesi imeisha, ila sio issue sana vituo vipp vingi hapa Mjini.

Pia angalia issue za ECU, na sensor maana gari ipo tunned kufanya combustion ya petrol leo ikikutana na CNG kuna possibility ya kuzingua.

Ila faida pia zipo mfano lengo kuu kusave mafuta. Ina save sana.
Nimekusoma Mkuu, Ahsante sana.

Nilisahau kua hata nikifunga CNG lakin bado petrol system itakuwepo. So pale ambapo nitahitajka kua kwenye mazingira ambayo CNG haina performance nzuri bas nita switch kwenye petrol.

Issues za ECU na Sensor sio kwamba huu mfumo unakua na hizo vitu pia? Au sijaelewa ni vitu gani na applicability zake?
 
Aisee ungekuwa karibu na Mimi ningekupiga Kofi ili kama kichwani mwako kuna wazo Hilo la kufunga gesi liondoke!
Wewe umesikia wapi Subaru inafungwa mfumo wa gesi? Watanzania mbona mnakosa elimu hata hizi ndogo juu ya magari?
1) CNG ni mfumo wa kishamba Sana hata Huko ulaya hautumiki
2) CNG inatumika kwenye Bajaj Tu
3 CNG ni zaidi ya bomu
Wazungu baada ya kuona CNG ni UJINGA walianzisha magari chotara ( hybrid car) kama umeshindwa kumiliki Subaru tafuta IST itakusaidia .
Mimi Nina Subaru forester XT kama ni ishu ya fuel consumption huku ndiyo balaa lkn najitahidi Sana kufanya kuepuka safari zisizokuwa na tija. Kama huwezi kumiliki Hilo gari uza nunua IST
CNG inafungwa kwenye malori wewe unasema ni Bajaji peke yake, ni mtaalamu kutoka wapi?
 
Ni kweli,

Yes mkuu,
Technical reasons zitasaidia zaid uelewa.

Wafungaji wenyewe nimewacheki wanasema mfumo hauna shida, but perhaps wako kibiashara zaidi ndo nikaona nichek na wataalam wa humu.
(Mimi sio mtaalam) Kama una mpango wa kutumia hiyo gari zaidi ya miaka 2 ndo utaona faida yake.

Assume Kila siku unaitumia wese la 10,000 Kwa mwezi kama 200,000 na mwaka 2,400,000.
Kufunga huo mfumo na modification nyingine inaweza kugharim 2M+.
 
Mkuu,
Ahsante Kwa maoni. Nimeona umetaja sababu tatu,
1) Ushamba
2) Kwenye Bajaj tu
3) Bomu.

Niongezee hata technical reason ya huu mfumo kutokua mzuri Mkuu. Inawezekana kuna sababu ya Wazungu kuukataa labda hiyo Gas kwao ni adimu au gharama.
CNG ni mfumo wa gharama kwenye ufungaji wake ndiyo maana manufacturer wa magari hawataki kuingia kwenye gesi kuanzia vituo vya gesi Hadi process zake.
USA wamepiga marufuku mfumo wa gesi na itakapofika mwaka 2030 itakuwa mwisho wa mfumo wa gesi.
 
Issues za ECU na Sensor sio kwamba huu mfumo unakua na hizo vitu pia? Au sijaelewa ni vitu gani na applicability zake?
Upo sahihi. Complete kit ya CNG inabidi ije na ECU yake (ambayo haifanyi kazi peke yake bali inasaidiana na ya Petrol), sensors zake.

Nadhani kabla haujafunga, muulize mfungaji kit zinazokua included kwa specifi gari lako.
 
Tembelea kituo cha kujaza gesi halafu ufanye utafiti wako kutoka kwa watumiaji moja kwa moja hasa ukipata wenye Subaru model ya gari yako. Binafsi mimi naichukia gesi kwa sababu ya ule mtungi kwenye buti. Labda wa design namna nyingine ya kuweka mtungi.
 
Back
Top Bottom