Kuhusu kilichoandikwa mapema leo kunihusu

George Kiddy

Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
12
Reaction score
7
Ndugu zangu, mapema leo asubuhi mmeona post ya BAVICHA-IRAMBA ikisema kuwa nimetangaza rasmi kugombea UBUNGE katika jimbo la Iramba-Magharibi. Hilo haliwezi kuwa tangazo langu rasmi kwa sababu zifuatazo:-

1. Mgombea wa nafasi kubwa na nyeti kama hiyo hawezi kusemewa na yeyote ila yeye binafsi. Hivyo basi kama nia hiyo ninayo nitatangaza rasmi mimi mwenyewe muda wakufanya hivyo ukimea (ukiwadia).

2. Jumuiya ya chama (kama ilivyo Bavicha) sio haki kumuunga mkono mwanachama yeyote ambaye hata hajaidhinishwa na chama kugombea nafasi husika. Hii inaleta picha mbaya kwa yeyote mwingine mwenye nia yakugombea nafasi husika.

3. Muda wakutangaza kugombea haujafika hivyo kufanya hayo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama pamoja na kanuni zake. Napenda ieleweke kuwa mimi kama Mwanasheria na mdau wa siasa kwa muda mrefu naielewa Sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini, na katiba ya CHADEMA naielewa KINDAKINDAKI ("in and out"), hivyo siwezi kuikiuka kwa namna iwayo yote.

Aidha nimesikitishwa sana na Baraza hilo la vijana la CHADEMA kwakunilisha maneno na kusema uongo kuwa nilitoa matamshi hayo pale Katala Beach Hotel, jambo hili sio la kweli.

Kwa ufafanuzi tu kuhusu hili ni kwamba miezi takribani miwili kasoro iliyopita nilialikwa hotelini hapo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya "SIO KOSA LANGU" iliyoigizwa na wanafunzi wa chuo cha uhasibu (T.I.A-Singida Campus).

Pale sikuongelea suala lolote la kisiasa kama nilivyoripotiwa na BAVICHA-IRAMBA zaidi yakutoa mchango wangu na kushiriki mnada wa DVD hizo.

Nawaombeni radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, hasa wale wenzangu wenye nia ya kugombea nafasi hiyo adhimu, nawaambia msizimie moyo mapambano yangali bado. Aidha nawashukuru nyote mliofurahishwa na tangazo hilo na kunitia moyo kuwa naweza, napenda muelewe kuwa hili ni suala la muda tu, ukifika na nia ikingali basi nitawaombeni ushirikiano.

Asanteni sana.
George Kidindima,
04/02/2014.
 
Mkuu kabla hujalaumu Bavicha -Singida jiridhishe hao waliopost tangazo JF ndio wenyewe au ni maadui zetu kwa sababu hata yule gaidi mwegulu anaweza kuanzisha ID kwa jina hilo kupima upepo.. George Kiddy
 
Last edited by a moderator:
Bahati haiji mara mbili...we endelea kusubiri wakati UMEE lkn ndo kwa heri hivyo.
 
George Kiddy At least umeonesha maturity, vijana wenye njaa na wavivu wa kufikiri wapo vyama vyote na hawa ndio walimchimbia kaburi Zitto Kabwe akavimba kichwa kumbe ndio alikuwa anajimaliza mwenyewe.

Hongera sana kwa hilo na vijana tunawashauri watafute shughuri za kufanya kwenye siasa tukutane weekend au baada ya kumaliza shughuri zetu binafsi.
 
Last edited by a moderator:
George Kiddy M/kt wa CHADEMA Mkoa wa Singida awajibike kwa hili,
Chama hakiwezi kuendeshwa kikanjanja namna hii!
Katibu wa Kanda hio husika na kichwa cha habari.
 
Last edited by a moderator:
Sijaelewa kabisa.
Mwanasheria hebu panga hoja vizuri.
Achana na hearsay.
 
Wewe gombea tu, au jamaa ameshakutishia. Kama wananchi wa huko wamekuona unafaa wewe songa mbele bana.....
 
You r smart my bro, tunathamini mchango wako wa kuifanya Chadema kuwa moja.
 
Ndugu zangu, mapema leo asubuhi mmeona post ya BAVICHA-IRAMBA ikisema kuwa nimetangaza rasmi kugombea UBUNGE katika jimbo la Iramba-Magharibi. Hilo haliwezi kuwa tangazo langu rasmi kwa sababu zifuatazo:-

1. Mgombea wa nafasi kubwa na nyeti kama hiyo hawezi kusemewa na yeyote ila yeye binafsi. Hivyo basi kama nia hiyo ninayo nitatangaza rasmi mimi mwenyewe muda wakufanya hivyo ukimea (ukiwadia).

2. Jumuiya ya chama (kama ilivyo Bavicha) sio haki kumuunga mkono mwanachama yeyote ambaye hata hajaidhinishwa na chama kugombea nafasi husika. Hii inaleta picha mbaya kwa yeyote mwingine mwenye nia yakugombea nafasi husika.

3. Muda wakutangaza kugombea haujafika hivyo kufanya hayo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama pamoja na kanuni zake. Napenda ieleweke kuwa mimi kama Mwanasheria na mdau wa siasa kwa muda mrefu naielewa Sheria ya usajili wa vyama vya siasa nchini, na katiba ya CHADEMA naielewa KINDAKINDAKI ("in and out"), hivyo siwezi kuikiuka kwa namna iwayo yote.

Aidha nimesikitishwa sana na Baraza hilo la vijana la CHADEMA kwakunilisha maneno na kusema uongo kuwa nilitoa matamshi hayo pale Katala Beach Hotel, jambo hili sio la kweli.

Kwa ufafanuzi tu kuhusu hili ni kwamba miezi takribani miwili kasoro iliyopita nilialikwa hotelini hapo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya "SIO KOSA LANGU" iliyoigizwa na wanafunzi wa chuo cha uhasibu (T.I.A-Singida Campus).

Pale sikuongelea suala lolote la kisiasa kama nilivyoripotiwa na BAVICHA-IRAMBA zaidi yakutoa mchango wangu na kushiriki mnada wa DVD hizo.

Nawaombeni radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, hasa wale wenzangu wenye nia ya kugombea nafasi hiyo adhimu, nawaambia msizimie moyo mapambano yangali bado. Aidha nawashukuru nyote mliofurahishwa na tangazo hilo na kunitia moyo kuwa naweza, napenda muelewe kuwa hili ni suala la muda tu, ukifika na nia ikingali basi nitawaombeni ushirikiano.

Asanteni sana.
George Kidindima,
04/02/2014.

Waambie ndugu zako mkuu, maana hawa BAVICHA hivi sasa wamekuwa mavuvuzela kutokana na kuongozwa na mbmumbumbu HECHE.
 
Umeogpa kufa dogo?mbona wewe wa kiume?
Usimwogope siku hizi hana sumu.
 
Wewe gombea tu, au jamaa ameshakutishia. Kama wananchi wa huko wamekuona unafaa wewe songa mbele bana.....

Kwa Chadema kila mtu ni msemaji, wewe,Yeriko,Mungi,Arushaone,Lema, vifaranga...........kila mtu husemea chama.......na kwasababu Dr.Slaa kwa sasa ni Mbunge wa JF amekuwa aki-like post zenu
 
George Kiddy At least umeonesha maturity, vijana wenye njaa na wavivu wa kufikiri wapo vyama vyote na hawa ndio walimchimbia kaburi Zitto Kabwe akavimba kichwa kumbe ndio alikuwa anajimaliza mwenyewe.

Hongera sana kwa hilo na vijana tunawashauri watafute shughuri za kufanya kwenye siasa tukutane weekend au baada ya kumaliza shughuri zetu binafsi.

Dogo MatolaKwa Chadema kila mtu ni msemaji, wewe,Yeriko,Mungi,Arushaone,Le ma nk...........kila mtu husemea chama.......na kwasababu Dr.Slaa kwa sasa ni mgombea Ubunge wa JF amekuwa aki-like post zenu. Hata kama JF ingekuwa jimbo chadema haiwezi kushinda milele!
 
Back
Top Bottom