Hakuna Sababu ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kutenga Budget kubwa ya kununua Grader ikiwa kuna Maeneo Ndani ya Manispaa ya Morogoro kuna uhitaji wa Maboresho ya zahanati, Madarasa na madawati, na pamoja na miundombinu mingine ikiwa ni pamoja na Maboma ya shule za sekondari, kuna huduma za jamii Direct kama ilivyo sawa na Matakwa na Kiu ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Kama kuna uhitaji wa Grader katika Manispaa, ikumbukwe kuna Tarura na Tanroads hawa wana hivi vifaa na vyote vinahudumia na kutoa mahitaji yaleyale yanayokusudiwa na Halmashauri ya kununua Grader.
Hivyo nashauri Budget hii ielekezwe kwenye ujenzi wa Zahanati, Umaliziaji wa Maboma ya shule za sekondari na Huduma za jamii.
Mh. Diwani acha kutafuta umaarufu wa kijinga.haya unayoyasema hapa waambie hapo kwenye kikao. Huku mtandaoni unatuambia sisi tunauwezo wa kubadilisha hiyo bajeti yenu hapo manispaa ya Morogoro?