haulecarolus
New Member
- Apr 1, 2012
- 2
- 2
Ndugu zangu watanzania, nawaomba sana kuhusu suala hili la tume ya katiba tujaribu kuwa na uvumilivu wa kisiasa tukishaanza kupandikiza mambo ya udini hatari iliyo mbele yetu itakuwa kubwa sana, tume imeapishwa leo, watoa maoni ni sisi wananchi na waamuzi wa mwisho wa suala hili la katiba ni sisi wananchi, ndio tukakao piga kura za maoni kuikubali au kuikataa hiyo rasimu ya katiba itakayoletwa.
Sikatai maoni ya wanaoona kuna uwiano mdogo wa udini kwa wajumbe walioteuliwa yaani 9 kwa 21, labda nimshauri tu mh rais jk ameliona hili au lilimpita kushoto?
Kama ameliona basi alifanyie kazi kama alivyofanyia kazi musuada ule kule bungeni kwa kuwasikiliza wadau mapema ili hili nalo lisije likaleta kizazaa. Ila sisi wadau ebu tuwe na subira kidogo. Mungu ibariki tanzania, haule.