THK DJAYZZ
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 2,166
- 175
Wakuu ni sababu gani za msingi hupelekea hoteli kupewa hadhi ya nyota tano ? Ningependa kufahamishwa.
Swali la msingi sana mkuu, wataalam njooni jamvin
Hoteli kupewa hadhi ya nyota 5, licha ya hoteli hiyo kuwa kubwa, kwa maana ya kuwa na vyumba vingi vya kulala, lakini sababu nyingine kubwa ni hoteli hiyo kuwa na facilities nyingi zinazopatikana hapo hotelini.Wakuu ni sababu gani za msingi hupelekea hoteli kupewa hadhi ya nyota tano ? Ningependa kufahamishwa.
Wakuu ni sababu gani za msingi hupelekea hoteli kupewa hadhi ya nyota tano ? Ningependa kufahamishwa.
Mi nataka kujua gharama za kukodi chumba kwa siku.
huwa zinatofautiana kulingana na nchi na nchii, ila kwa Tz, ni kuanzia tsh. 507,000/=@kwa siku, ni pa lefu mkuuu
Kumbe nikiamua kujitoa ufahamu siku moja naweza kulala apo maana sehemu kama hizo ukiwa na mkeo ikaingia mimba hapi lazima umzae Obama tu.
hapa utazaa jk chunga hela zako
Hoteli kupewa hadhi ya nyota 5, licha ya hoteli hiyo kuwa kubwa, kwa maana ya kuwa na vyumba vingi vya kulala, lakini sababu nyingine kubwa ni hoteli hiyo kuwa na facilities nyingi zinazopatikana hapo hotelini.
Hiyo maana yake ni kuwa hoteli hiyo kuwa na huduma mbalimbali kama vile za maduka ya kubadilishia pesa, maduka ya kupata bidhaa muhimu za kibinadamu, kuwa na sehemu za kupatia vinywaji na chakula,kuwa na mawakala wa mashirika mbalimbali ya ndege, kuwa na kumbi kadhaa za mikutano, kuwa na bwawa la kuogelea, kuwa na huduma za kufuliwa nguo,kuwa na huduma za simu na internet, nk.
Kwa kifupi ni kuwa unapokuwa kwenye hoteli ya nyota 5, hulazimiki kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya kujitafutia mahitaji muhimu.
Kwa jijini Dar-es-salaam, hoteli zenye hadhi ya nyota 5 zipo kama 3 hivi, nazo ni Serena, Kilimanjaro Hyatt na Seacliff.
Mkuu hili ni somo ndefu kidogo
kwanza nchi inatakiwa iwe na bodi/kama sio nchi wadau wamiliki wa hoteli wenyewe
Pili vigezo vinaandaliwa.....hivyo vigezo vinakuwa vingi mfano...idadi ya room,ukubwa wa chumba,vifaa vinavyotumika ndani.....tambua kuna hoteli wana mpaka gold plated vijiko.idadi ya wafanyakazi..staff to guest ratio....uwezo wa wafanyakazi kucommunciate...kichina, english na lugha nyingine,,,,,,uwezo wa jengo kuhudumia watu wenye mahitai maakum kama walemavu na wasiojiweza...usalama.....huduma nyinginezo kama entertainment etc ...kumbuka vigezo vipo lukuki kutokana na ukubwa wa uchumi taifa husika
Wadau wakishakubaliana na hivyo vigezo...sasa kila mwaka kunakuwa na team ya wataalam kutika kwenye bodi/au kampuni iliyoundwa na wadau wanatemebelea kila hotel..kukagua hivyo vigezo....kila kigezo kinakaguliwa na kupewa marks......wakishamaliza ndio mwenye property/hotel anajulishwa kama amekidhi viwango vya kupewa nyota 5au4 au 3 nk
Kumbuka hii ni muhimu saana kwani inasaidia saana kwenye maskoko..mfano SUPERBRANDY KWA VYOMBO VYA HABARI HUKO NYUMBANI,KWA MIAKA MINGI ITV ILIKUWA INAONGOZA NA WALIKUWA WANAJIVUNIA SAANAA HILO LAKINI MWAKA HUU AZAM WAMEWAZIDI...HUWEZI TENA SIKIA WANAJITANGAZA NI SUPERBRAND KITUO BORA TANZANIA.
Nivyo hivo kwa mahoteli unapopata nyota tanu wanazitumia kujitanagaza...na hii sio guarantee kwamba utakuwa na hivyo vigezo muda wote vinafanyiwa kazi, maboresho na kadhalika
Kwatanzania tunasua sua hatuna hiyo bodi ilka ndani ya wizara ya maliasili na utalii kuna kitengo kinahusika kuna kipindi nasikia walizifanyia assessement hotel mikoa tofauti kwa kutumia vigezo walivyotengeneza hoteli nyingi haziku qualify kuwa assessed hii nikutokana na kujengwa ovyo mfano travel time magomeni ni hoteli kubwa ila vyumba vidogo,reception yenyewe mtu mrefu akiingia lazima ainame.....kwa hivyo vigezo tu huwezi ukaendelea ku assess property ya namna hiyo...ilitakiwa mwekezaji wakati anajenga ajulishwe hii kitu na serekali...tatizo serekali haina wataalam wa kutosha
Kwanini Hotel kama serena unakuja kuna property zao wanajii ta nyota tano.....tambua ile ni chain hotel na wana different property na za madaraja mbalimbali mfano lodges, commercial hotel inns etc,wanakuwa na standards zao na wanakuwa na team ya watalam wanaofuatilia kila nchi waliowekeza kuhakikisha hizo standards zkinafuatwa
Mfano kwa chain hotel kama Holiday Inn mfano proparty kama ni 03 stars na wanaoperate in more than one country mfano ukiaenda holiday inn dsm hutaona tofauti,ukienda nairobi utakuta iko the same hata uk nk
tambua so hotel tu hata restaurant zna grading system zake very common ufaransa hata na Uk na miji mingine mikuwa duniani
Mi nataka kujua gharama za kukodi chumba kwa siku.
Kwa nyongeza iwe na chumba ambacho rais anaweza kulala na mahitaj yake akapata
huwa zinatofautiana kulingana na nchi na nchii, ila kwa Tz, ni kuanzia tsh. 507,000/=@kwa siku, ni pa lefu mkuuu