Kuhusu hisa za makampuni yaliyo kwenye Soko la Hisa Dar (DSE)

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
623
595
Habari za wakati huu wakuu, Niwape pole kwa mampambano mnayoyaendeleza nje ya mitandao kila mmoja kwa upande wake akiamini atapata kile anachokipigania.

Bila kupoteza wakati nielekee moja kwa moja kwenye mkeka wangu wa leo na kama unavyojieleza hapo juu,Pasi na kupoteza wakati nieleze tu mimi si mtaalamu wa masuala ya hisa ila najaribu tu kuwaza kwa sauti na kama kuna mahali nitapotosha naomba kurekebishwa.

Hali ya uchumi si nzuri

Kulinagana na taarifa mbali mbali za kiuchumi mtakubaliana na mimi kwamba wakati huu kidogo hali ya uchumi si nzuri kulingana na miaka minne iliyopita hii changamotto kwa biashara nyingi kufanya vizuri ikiwa ni kwa jumla zile biashara ambazo zilikuepo na hizi changa zinazoanza wakati huu. hali ya mzunguko wa hela iko chini kiasi kwamba hadi sisi tulio na imani kali za dini tunajikuta tunabet mara moja moja kuona kama tunaeka ibukia huko (joke).

Kwenye mkwamo huu wa uchumi naamini pia hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la hisa DSE zimeathirika na hali hii (sina hakika) kama ni kweli hisa zimeathirika na hali hii nawaza jambo hapa kwa nini tusijitose kununua hisa za makampuni yenye kuonesha uhai hapo mbeleni mambo yakija kuwa sawa tujikute tayari tumepata hisa za thamani kubwa kwa bei rahisi? Ikiwa hili linawezekana basi hii itakua inaitwa kitaalam "KUFA KUFAANA" Nimefatilia mtikisiko wa uchumi wa 2008 wapo uliowafilisi kwa kupanic na kuuza share zao kwa bei ya hasara na waliozinunua kwa bei ya chini wakati ule waliweza kupata faida baada ya wakati ule wa mpito kumalizika.

Naona hisa kama za TBL najua saivi tumehamia kweny VANT na NYAGI ila si kupenda kwetu ni pochi inatupeleka uko baadae jiwe akipumzika naona wengi watairudia ''NGANO'' kama awali na mambo yataanza kuimarika tena.

HAPA Nimejaribu kuona uzuri kwenye ubaya.. Yaani kuona fursa kwenye matatizo.. yaani sina tofauti na jamaa aliyetengeneza mkaa kotokana na kinyesi cha binadam. Niachie hapo hii mizaha sasa.. Kwa yeyote anayeamini hili linawezekana na anautaalam kidogo wa haya masuala anaweza kuongezea nyama kidogo na mwisho wa siku tukatengeneza kina BUFFET wa kwetu hapa hapa Msata

Naomba kuwasilisha kwenu wanabodi, Michango yenu itachukuliwa kwa uzito mkubwa. Kumbuka baadae mtu atagoogle haya masuala ataletwa kwenye huu uzi yale majibu kama ya Bwakila naomba yabaki Inbox kwa leo... Hahaha

THANKS IN ADVANCE
 
Duuu asante umeniamsha nilisha usahau kabisa huu upande


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Biashara ya hisa ni kati ya yule mwenye tamaa za haraka haraka(muuzaji) na yule ambaye anaweza kuongea/kuahirisha tamaa zake(mnunuzi)

Mwanzisha mada ulipaswa utoe mifano SPECIFIC ya bei ya baadhi ya hisa za makampuni na kuelezea jinsi gani zilivyodororora na kushindwa kukua kwa muda gani na kutoa makisio yako jee ikiwa hali itatengemaa jee unatarajia ongezeko gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sisi wazee wa imani kali huwa tunatupia mkeka sema nadhani nako jamaa amekaza kama barcelona anapigwa 4 sio mchezo jiwe kakaza kote mkuu hahahah
 
Biashara ya hisa ni kati ya yule mwenye tamaa za haraka haraka(muuzaji) na yule ambaye anaweza kuongea/kuahirisha tamaa zake(mnunuzi)
Mwanzisha mada ulipaswa utoe mifano SPECIFIC ya bei ya baadhi ya hisa za makampuni na kuelezea jinsi gani zilivyodororora na kushindwa kukua kwa muda gani na kutoa makisio yako jee ikiwa hali itatengemaa jee unatarajia ongezeko gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mm ndio nahitaji kupata speculation kupitia hao wataalam
 
Nilishawahi kuwaza, ila niliingiwa na hofu kuwa jiwe walilolikataa waashi laweza kuwa jiwe kuu la pembeni hadi 2025. Na hii itarefusha safari ya kusubiri
 
Kununua as the market is down is a good idea, lakin kwa hivi tunavyo endelea soko bado litaendelea kushuka, Check hisa za Acacia zilivyoguma kwa nguvu baada kupigwa ile fine kutoka juu and i strongly believe itashuka.

Hisa zina dividend ambayo inalipwa kama kampuni imepata faida, Crdb hawajatoa dividend for almost 4yrs meaning imekula hasara (according to their own reporting through the value of DSE at the moment being 150/share).

Unless una ka pesa pemben kimekaa tu hauna mpango nacho for the next 10yrs apo ndo naweza kukuambia uinvest kwenye hisa at the moment.

Uchumi ukiwa unaenda vizuri utaona hizi prices za share zina nenepa then thats a sign you buy and hold and wait for your dividends.
 
Mkuu nisaidie jinsi ninavyoweza kuwasiliana na Wakala yeyote wa SOKO LA HISA DSM -DSE.
 
Back
Top Bottom