Kuhusu gharama za kumsafirisha mtuhumiwa

Kuhusu gharama za kumsafirisha mtuhumiwa

zanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
201
Reaction score
257
Wadau nashindwa kupata title nzuri, na ningependa nipate mawazo yenu juu ya hili

kuna mtuhumiwa alifanya kitendo cha kinyama mkoani Tanga, na taarifa zika fika polisi na rb tukapewa, ila kwa bahati mbaya yule mtuhumiwa akatoroka.

ni kama wiki tatu sasa toka alivyotoroka, jana mtuhumiwa amekamatwa dar es salaam, na kufikishwa oysterbay, ilikua mida ya jioni kama saa mbili hivi, polisi waka waagiza wakamataji warudi leo asubuhi.

mshitakiwa ana umri wa miaka 21, kosa aliloshitakiwa nalo ni kumlawiti mtoto wa miaka 4, na sio mara moja na vipimo vya daktari vime thibitisha hilo,

cha ajabu ni kwamba polisi wana sema gharama za kumtoa mshitakiwa dar na kumpeleka tanga kufunguliwa mashitaka ni za watu waliomshitaki, mimi hili jambo nimeshindwa kuelewa, na tulivyo jaribu kufatilia ikaonekana ndio utaratibu eti serikali haina hela, nimwe zungumza na watu tofauti polisi wana sema ndio utarartibu

swali ambalo najiuliza ikitokea huna hela ina maana huyu mshitakiwa wata muacha huru bila kuangalia uzito wa kosa?.hakuonekani kama kuna muafaka na polisi wana cho dai ni hela kutoka upande wa walioshitaki ili wamsafirishe mtuhumiwa kwenda tanga

huyu mshitakiwa kamuharibu mtoto, sioni uwajibikaji wa serikali katika hili.hadi muda huu mshitakiwa yupo oysterbay,wanasubiri hiyo hela
 
Nijuavyo mimi kesi yoyote ya jinai mshtaki ni jamhuri na wewe ulieenda kushtaki utakua kama shahidi namba moja upande wa jamhuri ili kusaidia haki itendeke.
 
ndugu Yangu usichokijua ni sawa na usiku wa giza kwakifupi polisi ndo wanatakiwa kumsafirisha mtuhumiwa hadi mahala anapotakiwa kwa gharama za serikali na pesa hizo zote ziko chini ya RPC wa mkoa husika na ndiye mwenyejukumu la kuzipeleka kwa wakuu wa polisi wilayani,kasheshe ni pale ma RPC husika wanapozitumia hizo pesa kwa shughuri zingine tafauti na malengo husika, sasa inapotokea dharura kamahiyo ya kusafirisha mtuhumiwa nauli inakosekana matokeo yake mzingo wote unabebeshwa mlalamikaji, kwasababu mkuu wakituo hawezi kwenda kumuomba nauli bosi wake ataonekana hana nidham.lakini kwakifupi polisi ndo wanaotakiwa kugharamia nauli ya mtuhumiwa.
 
yaani kwa kweli haijakaa vyema.na hadi hadi muda huu mtuhumiwa yupo oysterbay.kwanza wamesema wana subiri simu ya upepo kutoka tanga.hadi hawaja pata.na pili wmedai 250,000 ili huyo mtuhumiwa asafirishwe.hiyo imr punguzwa walidai laki 6,

ndugu Yangu usichokijua ni sawa na usiku wa giza kwakifupi polisi ndo wanatakiwa kumsafirisha mtuhumiwa hadi mahala anapotakiwa kwa gharama za serikali na pesa hizo zote ziko chini ya RPC wa mkoa husika na ndiye mwenyejukumu la kuzipeleka kwa wakuu wa polisi wilayani,kasheshe ni pale ma RPC husika wanapozitumia hizo pesa kwa shughuri zingine tafauti na malengo husika, sasa inapotokea dharura kamahiyo ya kusafirisha mtuhumiwa nauli inakosekana matokeo yake mzingo wote unabebeshwa mlalamikaji, kwasababu mkuu wakituo hawezi kwenda kumuomba nauli bosi wake ataonekana hana nidham.lakini kwakifupi polisi ndo wanaotakiwa kugharamia nauli ya mtuhumiwa.
 
Iliishia wapi hii mkuu? Kwasababu nami leo hii nimekumbwa na mkasa kama huo ambapo kuna mtu alinitapeli kisha akatokomea na kufanikiwa kukamatwa mkoa mwingine baada ya mwaka. Sasa polisi wanadai nitoe pesa asafirishwe na nikikaa muda mrefu bila kutoa itabidi wamwachie. Hizi sheria ni ngumu sana kwani hadi mkuu wa kituo anasema ndio utaratibu.
 
Back
Top Bottom