Pamekuwa na mitazamo tofauti kuhusu dawa mbadala kuhusu utendaji wake wa kazi. mitazamo na matarajio ya watu na uharaka wa kupata outcome haraka umeweka maswali mengi kwa watu.
Kwa uhalisia si sahihi kuziita hizi ni dawa kwasababu ki asili haziponyi kama watu wanavyo fikiri. sasa nini kanacho fanyika?
Kwa kawaida miili yetu imeumbwa kwa mifumo yake maalum kwa ajili ya kupambana na vijidudu vya magonjwa na mifumo inayotoa taarifa pindi panapo kuwa na hitilafu katika mfumo fulani katika mwili. Kutokana na mfumo wa maisha na vyakula tunavyokuala ambavyo asilimia kubwa ni sumu mfano soda, sukari, juice za viwandani, hamira zitumikazo kutengeneze mikati na vitafunwa vingine, madawa tunayotumia tuumwapo, moshi wa magari n.k. Yote haya yameondoa mfumo wa miili yetu kujilinda yenyewe.
Tunapokunywa dawa za hospitalini, Tunasimamisha ugonjwa usiendelee (sio kuponya). Inawezekana ugonjwa ukatoka au ukabaki pale pale lakini umesitishwa na hautasikia dalili za kuumwa, Dawa hizi za hospitali zikisha maliza kazi yake zinaacha vile vibebeo vyake ambavyo vinabaki kama sumu mwilini. mfano ili kuua vijidudu vya malaria inabidi unywe dawa ya malaria ambayo ki uhalisia ni sumu ya kuwauwa hao vijidudu, sasa ilesumu ikabaki mwili kisha ukaugua tena, ukanywa dawa hiyo kisha tena na tena? sumu ina baki nyingi mwilini.
Kinachoitwa dawa mbadala ni vyakula na matunda pamoja na viungo vya asili ambavyo havija haribiwa na madawa ya kisasa. Mwili unapopata hivi unajikarabati wenye na kuamsha ile kinga yake ya asili. Sasa inategea wewe kama mgonjwa umeathirika na ugonjwa wako kiasi gani, na umetumia dawa za kisasa kwa muda gani. Kwa mfano itakuhijaji ule tangawizi kila siku kwa miaka mitano au saba uli kuamsha sehemu fulani ya mfumo wa mwili kuwa nomo, sasa hii itakuwa ni muda mrefu.
INAKUWA HIVI: Wataalamu wa dawa mbadala wanachukua tangawizi na kuindaa kama kidonge au dawa ya maji ambayo vipimo vyake ni sawa na kula idadi fulani ya tangawizi kwa miaka kadhaa. Ukiweza kutumia dawa hizo kwa kiwango na muda uliopewa na utaratibu na masharti, ukawa mvumilivu wa muda, mfumo wa mwili utakurudi katika uhalisia wake na kupambana na ugonjwa wako.
Tatizo kwa watu wengi ni MUDA.