Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,429
Napenda sana maandiko yako. Yamejaa weledi na hoja nzuri. Nasikitika wana JF wengi huwa wanapenda maandiko mepesi mepesi, ya kusutana na kushambuliana. Nadhani mfupo wa elimu yetu una-play part kubwa. Tuna kizazi chenye ushabiki bila tafakari. Back kwenye mada: Moja ya ''hasara'' za kuwa na wagombea binafsi (kama inavyosema na wanasiasa) ni kuwa maadui wa Taifa watakuwa na urahisi wa ku-sponsor ''mwanasiasa kibaraka mzalendo'' na kumfanya awe mbunge kwa maslahi yao. Au watu matajiri wanaweza kutumia ufukara uliokithiri ''kununua'' eg ubunge kwa maslahi yao.
Mimi sikubalini nao. Hata mgombea mwakilishi wa Chama cha siasa anaweza kununuliwa tu. Leo nimekutana na habari kutoka BBC inayozungumzia jinsi Australia inavyoilamu China kwa kutaka kuingiza mbunge kibaraka kwenye bunge la Australia. (Habari yake iko hapa Australia probes alleged Chinese spy MP plot ). Kama Taifa kubwa kama Australia linachezewa huu mchezo, je haya mataifa yetu ya madongokuinama wamewekwa wangapi? Nikakumbuka jinsi Zitto alivyolivalia njuga suala la bandari ya Bagamoyo na mchina.
Usiwe too negative mkuu,Tatizo watawala hawataki vyama au upinzani sasa wataruhusu chochote kweli
Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini...umesahau jinsi China ilivyofadhili ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa ccm.
..umesahau pia jinsi mgombea Uraisi wa ccm ilivyofanyiwa shopping na matajiri wa nchi moja ya Kiarabu.
Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini.
Kuna mtu mmoja anaitwa Robert Mueller, Hutu anatoka idara ya mahakama ya Marekani na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza jinsi Urusi ilivyoilingia uchaguzi wa USA mwaka 2016 na kum suppport Trump.Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini.
Kuna vitu vingi vinawezekana na ni bora
..Kweli.
..mimi nadhani kwanza tufanye kwa USAHIHI yale tuliyokubaliana kuyafanya.
..tuna sheria ya vyama vingi lakini sina uhakika kama inatekelezwa kwa haki na usawa.