Kuhusu changamoto za kisiasa zinazotokea, Wagombea binafsi inaweza kuwa suluhisho?

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
1574700421573.png

'Mtu asilazimike kuwa na chama ili kuwa kiongozi'.
Tushawishi bunge waone umuhimu wa hili.
Kwa kuwa,
  • Siasa za vyama vingi Tanzania zinachukua sura isiyopendeza sana,
  • Vyama vimejanga hali ya wao na sisi,ambayo sio chanya,
  • Watu wanabeba lawama au sifa zisizo zao bali kwa sababu ya vyama,
  • Watu wanashindwa kuwa wakweli yanapokuja masuala ya vyama vyao,
  • Vyama vilivyopo havisimamii tena misingi wala falsafa,bali misimamo ya viongozi wa vyama husika na vingine havina vinachosimamia kabisa,
  • Kuna watu wenye mawazo mazuri ila wanabanwa na misimamo ya chama
  • Kuna watu wanakosa nafasi za kuwa viongozi kwa sababu ya vyama Lakini ni watu wazuri tu,
  • Kuna watu wasiokubaliana na yanayotendeka ndani ya vyama, n
  • Kwa kuwa kuna watu hawana vyama lakini ni watu wazuri;

Umefika wakati wa kulishawishi bunge kufikiria umuhimu wa wagombea binafsi. Tunasema bunge kwa sababu suala hilo kwa sasa haliko kikatiba na kwa mujibu wa hukumu ya Mahakama ya rufaa ya mwaka 2010 kati ya Mtikila na AG ilishasema 'suala hilo ni la kisiasa na wenye uwezo wa kulishughulikia ni bunge' .Ni muhimu kulishauri bunge lione umuhimu wa suala hili na kufanya marekebisho madogo ya Katiba ili kuli 'accommodate'.

Faida zake itakuwa ni kama ifuatavyo;

1. Dhana ya sisi na wao itakufa,

2. Kila mtu atabeba lawama au sifa kulingana na matendo yake mwenyewe, hakuna atakayesulubiwa kwa makosa ya mwenzake, au kubebwa kwa sifa za wenzake,

3. Itakuwa rahisi kuwawajibisha wanaokosea au kuvunja sheria ,

4. Tutakuwa na bunge lenye watu mchanganyiko na walio huru,

5. Migogoro kwenye uchaguzi itapungua na haki itatawala,

6. Kutakuwa na mawazo ya aina mbalimbali na kwa kadiri kunavyokuwa na mawazo tofauti ndivyo uwezekano wa maendeleo unavyoongezeka.

7. Umoja wa kitaifa utaimarika

Hasara ni kama ifuatavyo;-

Kila lenye faida lina hasara pia, hasara watasaidia kuziainisha wengine.

Asanteni!

======

Hoja za wadau

Napenda sana maandiko yako. Yamejaa weledi na hoja nzuri. Nasikitika wana JF wengi huwa wanapenda maandiko mepesi mepesi, ya kusutana na kushambuliana. Nadhani mfupo wa elimu yetu una-play part kubwa. Tuna kizazi chenye ushabiki bila tafakari. Back kwenye mada: Moja ya ''hasara'' za kuwa na wagombea binafsi (kama inavyosema na wanasiasa) ni kuwa maadui wa Taifa watakuwa na urahisi wa ku-sponsor ''mwanasiasa kibaraka mzalendo'' na kumfanya awe mbunge kwa maslahi yao. Au watu matajiri wanaweza kutumia ufukara uliokithiri ''kununua'' eg ubunge kwa maslahi yao.

Mimi sikubalini nao. Hata mgombea mwakilishi wa Chama cha siasa anaweza kununuliwa tu. Leo nimekutana na habari kutoka BBC inayozungumzia jinsi Australia inavyoilamu China kwa kutaka kuingiza mbunge kibaraka kwenye bunge la Australia. (Habari yake iko hapa Australia probes alleged Chinese spy MP plot ). Kama Taifa kubwa kama Australia linachezewa huu mchezo, je haya mataifa yetu ya madongokuinama wamewekwa wangapi? Nikakumbuka jinsi Zitto alivyolivalia njuga suala la bandari ya Bagamoyo na mchina.
 
Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,505
2,000
Tatizo watawala hawataki vyama au upinzani sasa wataruhusu chochote kweli
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Tatizo watawala hawataki vyama au upinzani sasa wataruhusu chochote kweli
Usiwe too negative mkuu,
by the way hii mada haizungumzii vyama vya upinzani. kinachozungumziwa kwenye mada hii kikifanikiwa hakutakuwa na kitu kinachoitwa mpinzani na asiyempinzani, kutakuwa na viongozi wanaowakilisha wananchi na wanaosimamia masuala ya jumla jumla yanayohusu watu wote na atakayekuwa anaenda kinyume itakuwa rahisi kumbana
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,792
2,000
Napenda sana maandiko yako. Yamejaa weledi na hoja nzuri. Nasikitika wana JF wengi huwa wanapenda maandiko mepesi mepesi, ya kusutana na kushambuliana. Nadhani mfupo wa elimu yetu una-play part kubwa. Tuna kizazi chenye ushabiki bila tafakari. Back kwenye mada: Moja ya ''hasara'' za kuwa na wagombea binafsi (kama inavyosema na wanasiasa) ni kuwa maadui wa Taifa watakuwa na urahisi wa ku-sponsor ''mwanasiasa kibaraka mzalendo'' na kumfanya awe mbunge kwa maslahi yao. Au watu matajiri wanaweza kutumia ufukara uliokithiri ''kununua'' eg ubunge kwa maslahi yao.

Mimi sikubalini nao. Hata mgombea mwakilishi wa Chama cha siasa anaweza kununuliwa tu. Leo nimekutana na habari kutoka BBC inayozungumzia jinsi Australia inavyoilamu China kwa kutaka kuingiza mbunge kibaraka kwenye bunge la Australia. (Habari yake iko hapa Australia probes alleged Chinese spy MP plot ). Kama Taifa kubwa kama Australia linachezewa huu mchezo, je haya mataifa yetu ya madongokuinama wamewekwa wangapi? Nikakumbuka jinsi Zitto alivyolivalia njuga suala la bandari ya Bagamoyo na mchina.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
macho_mdiliko,
Mkuu hoja yako ni sahihi lakini maadui hata huko kwenye vyama vya siasa wanaweza kupitishwa tu vizuri sana. Angalau jambo la kufurahisha ni kwamba hizi nchi zinazoendelea kama Tanzania hatuna maadui wa kutisha sana. Lakini hata wangekuwepo, vyama sio guarantee ya kuwazuia.

Hiyo habari ya Australia nimeisoma ila Australia mazingira yake pia ni tofauti.

Nafikiri suala la watu kununuliwa na kuwa vibaraka ni linaweza kuwa gumu zaidi kwenye mfumo huo (wa wagombea binafsi wengi)kuliko uliopo sasa kwa sababu ni vigumu kununua watu waliotawanyika na wenye mitizamo tofauti, mazingira tofauti na kutokea sehemu tofauti kuliko kununua waliokusanyika.

Ni sawa na useme unanunua wana JF, ni ngumu kidogo kwa sababu namna ya kuwa mobilize na katika mobilization hiyo siri isivuje ni ngumu, lakini kama ni kundi 'homogenous' ni rahisi zaidi.

Unaonaje hoja hii mkuu?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,657
2,000
Azizi Mussa,

..hoja zako ni nzuri.

..lakini kama ccm inakandamiza vyama vyenzake vya siasa, unafikiri haitasita kukandamiza wagombea binafsi?

..kuna culture ya uhuni na ukatili imepandikizwa ndani ya ccm ambayo inaathiri ustawi wa demokrasia hapa nchini.

..utamaduni huo mpya kwangu mimi ni lazima ukome ili vyama vya siasa na wagombea binafsi waweze kushiriki siasa kwa haki na usawa.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,657
2,000
macho_mdiliko,

..umesahau jinsi China ilivyofadhili ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa ccm.

..umesahau pia jinsi mgombea Uraisi wa ccm ilivyofanyiwa shopping na matajiri wa nchi moja ya Kiarabu.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
11,792
2,000
..umesahau jinsi China ilivyofadhili ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa ccm.

..umesahau pia jinsi mgombea Uraisi wa ccm ilivyofanyiwa shopping na matajiri wa nchi moja ya Kiarabu.
Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,657
2,000
Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini.
..Kweli.

..mimi nadhani kwanza tufanye kwa USAHIHI yale tuliyokubaliana kuyafanya.

..tuna sheria ya vyama vingi lakini sina uhakika kama inatekelezwa kwa haki na usawa.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Yapo mengi. Na mengi zaidi ndiyo hatuyajui. Hayana Chama, hayana kabila, hajana jinsia na wala hayana dini.
Kuna mtu mmoja anaitwa Robert Mueller, Hutu anatoka idara ya mahakama ya Marekani na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza jinsi Urusi ilivyoilingia uchaguzi wa USA mwaka 2016 na kum suppport Trump.

Ripoti hiyo ya zaidi ya kurasa 500 iliyowekwa hadharani miezi micheche INA mambo mengi ikiwemo majibu ya hoja zako.

Hata hivyo kwa ujumla ishu sio wagombea binafsi maana Trump hakuwa mgombea binafsi
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
31,736
2,000
Kuna vitu vingi vinawezekana na ni bora
Mada yako ina mantiki, huenda mgombea binafsi isiwe suluhisho, ila kwa hapa tulipofikia haikwepeki, tena tumechelewa. Kama sio hila na mahakama kukwepa wajibu wake, leo hii tungekuwa na mgombea binafsi. Madhara ya wagombea kuwa watumwa wa vyama, yako wazi peupe na mifano hai ipo. Lakini waliohofia uwepo wa mgombea binafsi huko nyuma, leo hii ndio wanataka kwasababu kwa sasa wanaona wako salama. Ila walioona umuhimu wa mgombea binafsi wako sahihi toka wakati huo, lakini kama nchi tunakosea sana kuwapa kazi wabunge kutunga sheria, ambapo sheria hazitungwi kwa uhalisia wa sheria, bali ni vipi chama cha walio wengi watafaidika na sheria husika.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
31,736
2,000
..Kweli.

..mimi nadhani kwanza tufanye kwa USAHIHI yale tuliyokubaliana kuyafanya.

..tuna sheria ya vyama vingi lakini sina uhakika kama inatekelezwa kwa haki na usawa.
Tatizo kubwa la sheria za nchi kutekelezwa kwa utashi wa mtu ni madaraka aliyonayo rais. Kitendo cha katiba kutoa nguvu kubwa kwa rais kuwa juu ya sheria hata kutoshitakiwa akiwa madarakani au akiwa ametoka, hii ndio imechangia amri toka juu kuwa na nguvu kuliko sheria na katiba. Iwapo hatutapata katiba ya kuweza kumfikisha mtu yoyote mahakamani na kumpunguzia rais madaraka, tutacheza makida makida bila kusogea. Angalia sheria nyingi za nchi yetu zinatungwa kuendana na tabia binafsi ya rais aliye madarakani na genge lake.
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,596
2,000
Changamoto ni nyingi, ila kazi zaidi inakuja pale ambapo wanaotakiwa wakabiliane nazo ama hawafanyi kitu, au wanaongezea changamoto mpya. Ila tutafika tu taratibu taratibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom