Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Nisiwe mnafiki wala wa maneno mengi, nakubaliana na Spika Ndugai kuwa CHADEMA haiwezi kumfuta au kumfukuza ubunge mtanzania yeyote. Kama maamuzi ya CHADEMA yaliyotangazwa na Karibu Mkuu wao Mnyika yalikuwa ya kuwafukuza ubunge akina Lwakatare, Spika Ndugai yuko sahihi kukemea.
Naamini Spika Ndugai anajua kuwa kikatiba na kisheria, sifa mojawapo ya lazima ya kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge ni kuwa mwanachama wa chama kimojawapo cha siasa hapa nchini na afadhiliwe na chama hicho katika kugombea. Hilo ni takwa la kikatiba na kisheria.
Naamini pia kuwa Spika Ndugai anajua fika kabisa kuwa kukoma kwa ubunge kumeainishwa kikatiba na kisheria kwa kuorodhesha mambo yanayofanya ubunge ukome. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura Nambari 2 ya Sheria za Tanzania, moja ya jambo la lazima linalokomesha ubunge ni kukoma/ kuacha/ kusita kuwa mwanachama wa chama ambacho Mbunge husika alikuwa mwanachama wakati akigombea(Ibara ya 71(1)).
Iko wazi kuwa, na imeshatokea mara nyingi hapa nchini, mara tu baada ya uanachama wa Mbunge kukoma, ubunge wake nao unakoma. Hiyo ndiyo sheria halali iliyopo hivi sasa na inatumika kila uchao. Ndiyo kusema, vyama vimepewa nguvu ya kuupeperusha ubunge kwa kumfukuza uanachama tu Mbunge.
Mchungaji Marahemu Christopher Mtikila aliiona kadhia hii ya kumlazimisha mgombea wa Urais, Ubunge, Udiwani na kadhalika kuwa mwanachama na kufadhiliwa na chama. Akapambana kimahakama kuanzia kule Dodoma na hata Dar es Salaam.
Alipata ushindi mara mbili Mahakama Kuu Dodoma na Dar es Salaam lakini akagonga mwamba Mahakama ya Rufani kwenye shauri maarufu kama la Mgombea Binafsi. Bunge liliachiwa mamlaka yake ya kubadili katiba na sheria ili kuruhusu jambo hilo. Bado tunasubiri hatma ya jambo husika.
Kikatiba na kisheria, kupoteza uanachama wa chama cha siasa kilichomfadhili Mbunge wakati akigombea kunampotezea moja kwa moja ubunge wake. Kinachopaswa kufanywa na chama husika ni kupeleka kwa Mamlaka husika maamuzi yake hayo ya kumfukuza uanachama Mbunge. Basi. Baada ya hapo, Katiba na sheria zinachukua mkondo wake. Maelezo au kauli au tamko la yeyote halifui dafu.
Naamini Spika Ndugai anajua kuwa kwa hali ya sasa ya kikatiba, kisheria na kisiasa, kufukuzwa uanachama wa chama ni jambo linalopaswa kuepukwa na kila aliyechaguliwa akiwa mwanachama na aliyefadhiliwa na chama husika. Na hapo ndipo nidhamu kwa chama inapojikita na kujidai.
Itoshe kusema kuwa kikatiba na kisheria, kuanzia Rais, Mbunge, Diwani na kadhalika, uanachama unapokoma na nafasi hiyo inapotea mara moja na mhusika hawezi tena kikatiba na kisheria kuwa Rais, Mbunge, Diwani na kadhalika. Hadi hapo mambo hayo yatakavyobadilishwa kwenye Katiba na sheria zetu, kwasasa uanachama ni lulu.
Kama CHADEMA wamewafukuza uanachama akina Lwakatare, Selasini, Komu na Silinde, ubunge wao unakoma mara moja. Na hawapaswi kuwa Wabunge. Kama wamewafukuza ubunge, ni kinyume na katiba na sheria kwakuwa hawana mamlaka hayo.