Kuhusu bodi ya mikopo ya elimu ya Juu (HESLB)

Kuhusu bodi ya mikopo ya elimu ya Juu (HESLB)

suluta

Senior Member
Joined
Dec 22, 2016
Posts
115
Reaction score
40
Wadau mimi kuna jambo linanitatiza sana.

Ni kuhusu HESLB. Kila moja anafahamu kwamba kabla ya serikali hii ya awamu ya 5 haijaingia madarakani chini ya Dr. JPM, wanafunzi wa Elimu ya juu waliokuwa wakiomba mkopo kwenye form za maombi walisaini kwamba watarejesha mkopo huo kwa interest ya 7% wakati wakulipa. Mimi nilikuwa ni mmoja wapo.

Baada ya awamu ya 5 kushika hatam, mambo yakabadilika na ikawa sasa ni kulipa kwa interest ya 15% kwa kigezo kuwa sheria imebadilika.

Swali nalojiuliza ni; Je, ni sahihi?

Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba mfumo wa serikali yetu na sheria tulizorithi kutoka kwa wakoloni, Sheria zetu hazitekelezwi kurudi nyuma (Retrospectivity of the Law). Yaani namaanisha kwamba LEO HAIWEZI TUNGWA SHERIA AMBAYO HAIKUWEPO WAKAT JAMBO LINATENDEKA KISHA JAMBO HILO LIKATATULIWA KWA SHERIA HIYO MPYA ILIYOTUNGWA BAADA YA JAMBO KUTENDEKA.

Swali langu, NI ZIPI HAKI ZA WATU AMBAO TAYAR WALIKWISHA SAINI MKATABA WA 7% na sasa wanalipa 15%?

Serikali yetu iliangalie hili kwa jicho la pili kwa sababu kuna maumivu tunapata ambayo hatukustahili kuyapata.


Maoni yenu Wana JF.
 
15% si interest ni deduction rate.

What difference does it make? Kama inakatwa kwa kuzingatia mshahara au kipato cha mtu kwa mwezi. Zamani ilikuwa 7% sasa ni 15%, whatever we may call it, haitabadilisha maana kwamba ni nyingi sana
 
Back
Top Bottom