Kuhusu bei halisi ya matrekta

Kuhusu bei halisi ya matrekta

Kuna elimu unatakiwa uwe nayo unapotaka kununua trekta vitu kama unataka kulima binafsi au kibiashara.aina ya udongo unaloenda Lima ,ukijua haya utajua uchukue yrekta sina gani,lenye uwezo wa kulima hekta ngapi kwa siku,aina ya jembe,na vitendea kazi vingine,tela,kama ni udongo wa kunasa basi unahitaji LA 4wheel n.k
 
Sina hofu na afya zenu, natumaini mko wazima , ni salama na amani.

Kama kichwa kinavyosomeka, shida yangu ni kujua bei halisi ya matrekta kwa kuainisha aina zake na uwezo wake.
Mfano-Massey fergussion, swalaj, john deere na mengine mengi nisiyoyajua.
Naomba nijuzwe pia kama kuna utaratibu wa kulipia kidogo kidogo kwa kuanza na malipo ya awali, dhamana ikiwa ni trekta lenyewe,katika hili, malipo ya awali yasizidi milioni 14(14,000,000/=)
Nina hamu kubwa ya kupanua kilimo changu, kuna utajiri kwenye kilimo na nimeona hili mwaka jana na msimu wa mwaka huu.

Naomba kupata msaada.
Unalima mazao gani mkuu, wapi na kwa kiasi gani maana inategemeana, funguka waja wakusaidie
 
Habari. Nina taarifa kidogo. Kwanza inabidi ujue unahitaji trekta lenye uwezo gani yaani horse power na unataka brand new au used. Kwani bei inatofautiana kutokana na upya au imetumika, capacity , where is it made, brand na payment mode. John Deere wana payment arrangements ya kulipa 50% at the spot na balance unalipa ndani ya mwaka lakini kuna mfuko wa pembejeo wa serikali ingawaje una urasimu lakini waweza pitia hasa ukitaka kununua on credit. Kuna kampuni ya Kirasa inauza matrekta za Massey Ferguson new from Pakistan nadhani. Watembelee Ubungo opposite na njia ya kwenda kwa mzee wa upako.

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
Unashangaa nn?
kuna utajiri kwenye kilimo??? et serious??
 
mkuu ka upo serious nikuunganishe na mtu yupo ujerumani akufanyie mpango wa tractor jipya ila hela ni kwanzia million 35 ila si toleo jipya ka wataka used pia waweza pata toka Finlandi. pakistani au hapo South Africa ila mzigo toka Afrika unakuwa katika uchakavu mkubwa zaidi, ila MF 188 mpaka kulitoa bandarini ni mill 23 haizidi hapo but ni kutoka South afrika
 
mkuu ka upo serious nikuunganishe na mtu yupo ujerumani akufanyie mpango wa tractor jipya ila hela ni kwanzia million 35 ila si toleo jipya ka wataka used pia waweza pata toka Finlandi. pakistani au hapo South Africa ila mzigo toka Afrika unakuwa katika uchakavu mkubwa zaidi, ila MF 188 mpaka kulitoa bandarini ni mill 23 haizidi hapo but ni kutoka South afrika

TRECTOR haina makato yoyote bandarini. All capital goods import duty is zero.
 
Back
Top Bottom