Kuhofia uwekezaji wa China au Magharibi ni dalili za kukosa mipango

RWEZAURAJOHN

Member
Jul 5, 2011
24
26
Kama kuna nia ya kweli ya kuimarisha chumi za nchi za Afrika Tanzania ikiwemo, tujipange na kuwa na mikakati badala ya kujenga hofu ya kununuliwa au kunyanganywa miradi mikubwa na Wachina au nchi za Magharibi. Ni kujidanganya tunapofikiri kwamba Watanzania bila kuigiza (KUIBA) teknolojia ya nje, tunaweza kujenga viwanda kwa haraka.

Lazima tukubali wawekezaji wakubwa, lakini tukiwa tumejipanga kama walivyofanya serikali ya China. Kuhofia uwekezaji wa China au Magharibi, ni dalili za kukosa mipango na mikakati yakinifu na maono ya mbali. Hapa hatuhitaji vibaraka, bali Wazalendo. Tunahitaji viongozi wenye fikra za Tanzania kwanza badala ya familia kwanza.

Historia ya uchumi wa nchi duniani, inaonesha China miaka ya 1960 ilikuwa sawa na Tanzania. Ilikuwa na Waandisi wa kila tabaka. Marekani, Ujerumani, Uingereza, na nchi nyingine kama Japani, bàada ya kupungua kwa utumwa, walikimbilia China kutafuta nguvukazi rahisi (cheap labor). Wakaruhusiwa kujenga viwanda kwa masharti nafuu sana. Walilipa kodi kidogo, na walipata usaidizi wa serikali kuhakikisha viwanda vyao vinakua na kuwapatia faida waliyoilenga. Walifanya hivyo kwa kuwa walikuwa na mkakati wao wa ndani.

China ilitumia ujio huo kama fursa ya kuchukua (kuiba) teknolojia kwa kuwaingiza Waandisi wabobevu kuwa vibarua kwenye viwanda vilivyojengwa China. Waandisi hao walikuwa waajiriwa wa serikali ya China, ndiyo maana walistahimili kuitwa vibarua na kulipwa kidogo na wageni.

Baadaye wakahamisha teknolojia yote kwenye viwanda vyao. Baada ya muda, Waandisi wakajiondoa na kuimarisha viwanda vyao. Kwa sasa, vifaa karibu vyote vya Computer, na mitambo ya kisasa ya nchi za Magharibi, kwa sasa mtengenezaji mkubwa ni China. Walitanguliza mikakati ya muda mrefu badala ya hofu. Walirahisisha kila kitu kuvutia wawekezaji, huku wakiwa na jambo lao.

Je, Tanzania kama taifa litakaloendelea kudumu, tuna jambo letu?

Je, Waandisi wabobevu hapa nchini, wako tayari kufanyika vibarua kwa wawekezaji wageni au wanapenda kupewa nafasi za juu za usimamizi?

Je, Serikali ipo tayari kuwaingiza waandisi wake kama walivyofanya China ili kuchukua ujuzi?

Wachina najua hawatataka vibarua wa kuingia ndani ya teknolojia yao. Ni kwa sababu wanajua alichofanya. Nchi za Magharibi hazijali hilo, wanachohitaji ni cheap labor.

Kwa hiyo, badala ya kutanguliza hofu kama taifa, tuandae kwa siri wataalamu wabobevu na kuwaweka tayari kwa zoezi la miaka ishirini au thelathini ijayo. Walipwe vizuri, nje ya kile wanachopewa na wageni. Na waonywe sana na kuangaliwa wasitoboe siri kwa vyovyote vile. Wakubali manyanyaso yote huku wakifanya walichotumwa.

Kama tunataka kutoboa na kwenda uchumi wa juu, lazima tukubali wawekezaji waje na wataalamu wao. Wataalamu wetu wakubali kuwa vibarua wa wataalamu wao, huku wakiwa wamebeba jambo letu. Kwa njia hii tutatoboa kama walivyofanya wachina. Hili linahitaji utashi wa kisiasa, mikakati ya pamoja, na uelewa wa wasomi wetu.

John Rweyemamu Rwezaura
(MBA)

Screenshot_20221111-205004.jpg
 
Kama kampuni unazalisha kidogo kwa sababu hutumii Mali ghafi zako vizuri. Ila unategemea wawekezaji wakupe nguvu kubwa wakati unaweza fanya kikubwa mwenyewe na kutumia nguvu ndogo ya wawekezaji. .
Mwenye akili kubwa ndio anaweza elewa hii. .
 
Back
Top Bottom