Kugombea ni KUTUMWA na wananchi au DHAMIRA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kugombea ni KUTUMWA na wananchi au DHAMIRA?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NGULI, Mar 23, 2010.

 1. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kila mgombea nayemsikiliza anasema wananchi wameniomba nigombee niwe kiongozi wao wameniona nafaa.....mimi huu msemo hauningii kichwani hata kidogo.

  Nafikiri wewe kama kiongozi au unataka kuwa kiongozi lazma dhamira yako ikusukume na uwe una zile leadership qualities. Hao unaosema wamekutuma au kukuomba wanaweza kuwa ni kundi la watu wachache ambao wanataka masalai yao yatimizwe endapo utakuwa kiongozi. Linaweza kuwa hata kundi la majambazi linalohitaji ulilinde lisiingie kwenye mikono ya sheria na form wanakuchangia na ile siku ya kuchukua form wanakubeba ju juu uonekane unakubalika kwenye jamii.

  Siujui wenzangu wa jukwaa hili mnamtizamo gani kwenye hili swala la watu kutumwa kugombea na wanachi hata kama azma yao sio kuwa kiongozi.
   
 2. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nguli nakuunga mkono, kitu kikubwa katika kugombea ni dhamira binafsi ya mgombea. hiyo kusema wananchi wameniomba nigombee haina mashiko kwa sehemu kubwa.

  Nakubali watu wengine wanaweza kushawishiwa na wapiga kura baada ya kuonyesha uwezo wao katika nyanja mbali mbali., lakini hiyo ni asilimia ndogo sana. waliobaki wanasema wameombwa kugombea they are just good for nothing.
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Probably vyote ni muhimu. Kuwa na dhamira sana bila support ya wananchi kunaweza kuchukuliwa kamauchu wa madaraka bila kukubalika.

  Ila nakubaliana na Nguli kwamba wagombea wengi- wengi, si wote- wana hii fake modesty ya kusema "nimeombwa na wazee" as if they are doing wananchi one big favor by running.This is dishonesty.

  Probably wanataka kujionyesha kwamba wao ni humble na hawakuwa na ambition ya kugombea mpaka walipoombwa na wananchi, kibaya zaidi wengine huwaomba wananchi wawaombe kugombea, utakuta mtu anapandikiza wapambe wake waanze kupeleka maneno kwa wazee wa vijijini kwamba wamchague, halafu wazee hawa influential waki mu endorse, wanajitia kusema "wameombwa na wazee" wakati ukweli ni kwamba wao ndio wamewaomba wazee kuwaomba, crazy.

  Yote haya ynatokana na ukweli kwamba katika siasa bado ambition inaonekana kuwa si kitu kizuri, wakati this doesnot need to be so.

  Tunahitaji kuona mtu mwenye confidence akasimama na kusema mimi nfikiri ndiye mtu sawa wa kuongoza watu, na sababu zangu ni hizi na zile, bila kutaja uozo wa kuwa "nimeombwa na wazee". Hata kama umeombwa na wazee kikweli, ukishakubali uamuzi ni wako, na point ya kwamba uliombwa na wazee inakuwa moot.

  Wengine tukisikia umesubiri mpaka uombwe na wazee/ watu tuna ku disqualify, kwa sababu unaonekana huna personal initiative, na kila kitu inabidi uambiwe, uombwe etc.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni wezi wa akili za masikini hawakutumwa chochote, kma kweli mtu anataka kuwatumikia watu lazima awe mbunge, utakuta mtu anaacha kusomesha chuoni, shule au anaacha udakitari...anakwenda kugombea eti anataka kutumikia watu...kuna pahala muhimu pakutumikia watu kuliko hospitali,chuo,shule n.k?
  Waongo tu wanataka kujiongezea mitaji ya biashara tu na kuwaibia wanyonge kodi zao basi.
   
Loading...