kugombania penzi!vita kwa thirdy party!

kugombania penzi!vita kwa thirdy party!

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
15,347
Reaction score
11,626
kila mtu anapenda kuwa na mahusiano stable!
kuna mambo huwa yananishangaza naombeni mnisaidie ipi njia sahihi?
assume una mpenzi wako ..au mume/mke...ikatokea akawa na mtu mwingine...kuna watu wengine wakiona hivi solution yao ni kujivua gamba na kuachana
wengine wanawafata hao wapenzi wa wapenzi wao na kuwafanyia vurugu ili waachane na wapenzi wao...yaani kwa kifupi vita inaanzishwa na hao thirdy party!
mimi nilishawai kutukanwa na mdada mmoja vibaya sana alikuta mpenzi wake kaniandikia sms alikuwa ananitongoza ! mimi nilishangaa maana sms ilikuwa inajieleza kabisa kwamba mimi nipo clean kwenye hilo! halafu jamaa mwenyewe hakuwa ametulia hata kiivo alikuwa na wengine pia yaani huyo dada kazi yake ni kupigana na wanawake wenzake wao ndo anawaona adui wa penzi lake...kwake mwanaume wake hana kosa???????????!!!!!!!!!!
naombeni swali kuna haja ya kupigana na wapenzi wa wapenzi,waume au wake zetu?
 
Ndoa hasa za kikristo ndio tatizo kubwa kujhnasua. Ila km ni mpnz tu bora kujivua gamba. Ya nini kuchangia na maradhi yalivyojaa? Hata kama me mbaya yupo atakayenithamini na kunipenda nilivyo na kufurahia mapenzi. Haina haja kama hakupendi hakupendi tu na atatotongoza kila kukicha.
 
Mi sioni haja kama mpenzi wangu anatoka na mtu mwingine nikagundua nitadili na wangu sababu naamini ckuzote mwanaume ndo huanzisha mahusiano!lakini huyo bidada lazima nimpe onyo maana huwezi jua pengine alidanganywa kuwa yupo peke yake so ili kumfahamisha lazima apokee ujumbe but si lazima matusi! Cjui kwa wanaume ngoja waje!
 
Inategemea kwa kweli

1. Third party mstaarabu na hakujua kama wewe ulivyotukanwa ni kwamba mwenye mzigo alikuwa anatuma salamu kuwa ujue huyo jamaa ana kwake ila jinsi ya na content ya weza kuwa matusi,mkwara au request

2. Third party yuko informed yet persistent wanasema amani haiombwi ila hupiganiwa!!!

3. Status yenu pia itaamua,jist gf,fiance au mke/mume;

Lakini kikubwa ni assessment ya tukio zima kama lina issues za wewe kuwa chanzo,hapa maamuzi yaweza backfire ukaonekana mwehu mtu mzima!!!!
 
Huko ni kujipotezea nguvu na heshima,hivi badala umuweke mtu wako chini muongee ukaanzishe vurugu kwa watu usiowajua????mi ujinga huo sifanyi maana in reality huyo wa tatu pengine hana hata kosa
 
Inategemea......wewe unaishi na wanandoa hao mtaa mmoja alafu unatembea na mke/mume wa mtu basi ujue kipigo kinakuhusu.

Mawasiliano ya huyo 3rd party yanabambwa na mwenye mali,unaambiwa we unatukana.....ooohh kama we mtamu asingekuja kwangu-kipigo kinakuhusu
 
wote wanahusika ,ina muhusika sana ni wako kwa sababu anaonyesha hajaridhika na wewe so all is doing is to fight off her /his weakness thats Y the better medicine is distance(separation) ili umpate amabye karidhika na wewe kila kitu kama nyuma ubao.......kama muhindi wa kariakoo(ke) au mwanaume hana fedha ,mlevi n.k.!!
 
kupigana hapana aisee. i prefeer kuongea tuone 'what went wrong', ikishindikana then separation (temporary au permanent depending na response yake). kupigana na kuishia kuchomana visu kisa mwanamke, sifanyi
 
Mi sioni haja kama mpenzi wangu anatoka na mtu mwingine nikagundua nitadili na wangu sababu naamini ckuzote mwanaume ndo huanzisha mahusiano!lakini huyo bidada lazima nimpe onyo maana huwezi jua pengine alidanganywa kuwa yupo peke yake so ili kumfahamisha lazima apokee ujumbe but si lazima matusi! Cjui kwa wanaume ngoja waje!
je kama wewe ndo unadanganywa ananipenda mimi?
 
Inategemea......wewe unaishi na wanandoa hao mtaa mmoja alafu unatembea na mke/mume wa mtu basi ujue kipigo kinakuhusu.

Mawasiliano ya huyo 3rd party yanabambwa na mwenye mali,unaambiwa we unatukana.....ooohh kama we mtamu asingekuja kwangu-kipigo kinakuhusu
ni kweli kama ni wanandoa na tunajuana hapo nakubali kipigo...ila kama ni mpenzi tu na hatujuani kwa nini ulipige au kunitusi ? je kama ni kweli ananipenda mimi na sio wewe?
 
kupigana hapana aisee. i prefeer kuongea tuone 'what went wrong', ikishindikana then separation (temporary au permanent depending na response yake). kupigana na kuishia kuchomana visu kisa mwanamke, sifanyi
umeona ya aunt ezekiel ?
 
Nakubaliana kabisa na smile wakati mwengine mtu anakuwa so innocent hajui kama mtu ana mume/mchumba anaingizwa mjini kisha anakuja kuporomeshewa matusi inakuwa sio haki kwa kweli na wanawake wanachukua hatua hizo nawaona wana matatizo sana na siajabu hata huyo mwanaume akatoka nje..Ni kweli uchungu wa mume ajuaye mke lakini inawezekana huyo mwanaume ndio chanzo cha matatizo yote kwahio masuala hayo anatakiwa adeal na mumewe na si vingenevyo....Kawaida kabla hujamhukumu mtu lazima kitu kifanyiwe uchunguzi wa kina ,Kwa vithibitisho ulivyopata then unaweza kuamua la kufanya sio JUMPING INTO CONCLUSSIONS!
 
eeh mbona unatumia jina langu my real name is mimi!
bora sasa angekuwa mke au mume ...unakuta hata mahari hajatolewa ni kigegedio tu.ila anapigana mtaa mzima
 
eeh mbona unatumia jina langu my real name is mimi!
bora sasa angekuwa mke au mume ...unakuta hata mahari hajatolewa ni kigegedio tu.ila anapigana mtaa mzima
Aiiii sorry jamani sikujua kama na we waitwa mimi basi tutakuwa mapacha,Hao wanaopigania mtaa mzima kwaajili ya kigegedio tu ndo hakuna kabisa kumkichwa lohhhh:smile-big:Mi nikishaona mwanaume yuko hivo ndo nakaza kamba za viatu nitoke baruti vizuri he he he...Kujitakia kifo kabla sijaenjoy life....Halafu na sie wadada tuwe makini na watu tunaotoka nao,lazima umchunguze mtu kwanza kama kweli yupo available au ndo wale danganya toto....
 
1. Siwezi kugombania penzi hata kama ninampenda vipi, nitakufa kishujaa. Kama kweli mpenzi wangu ameamua kutoka na mwingine, siwezi kuhusisha third part kwa vile yeye ana akili timamu, anajua lipi afanye lipi aache, i will confront her... na naamini mwisho wa yote we will go separate ways.

2. Ikiwa tuko kwenye ndoa, tutakaa tujadiliane, sababu za yeye kutoka nje ya ndoa, najua itachukua nguvu nyingi kunishawishi nimuelewe....
ila nadhani sitaweza kumwamini tena ktk maisha yangu... na pia sioni sababu ya kufanya vurugu na huyo aliyelala nae ila nitamweleza kuwa ni mke wangu, amuache.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom