Nimekuelewa sana, kuna jamaa alikuwa alikuwa akimsakama sana mkewe kuwa anajichelewesha kum bebea mimba ama ni mgumba, yule dada akahangaika anavyojua yeye, alilia, alisali na kufanya kila ajualo yeye mwisho wa siku akashika mimba, furaha ikarudi ndani ya nyumba na yule bi dada akafanikiwa kujifungua mtoto wa kike, bahat mbaya alipofikisha miaka mitano yule mtoto akawa na kansa, walihangaika sana na jamaa alikuwa na kipato kizur tuu, lakin mwisho wa yote mtoto alifariki, ilikuwa ni huzun isiyoelezeka sasa wakaanza harakat za kutafta mtoto mwingine, walihangaika sana, ila sfar hii mke akamwambia mumewe waende wote hospital, jamaa mwanzo alikataa kata kata ila mwisho akakubali, walipofika majibu yalikuwa tofauti sana, ni haya hapa, daktari alimwambia jamaa mkewe hana tatizo lakin yeye ndio ana tatizo na mbegu zake hazina uwezo wa kutungisha mimba milele, dah jamaa akapaniki, inawezekanaje nawalishapata mtoto, ilikuwa ni USA, Lakin mshikajia alienda mpaka Iran na India kutafta majib tofauti ila jibu lilikuwa lilelile yaan yeye anaweza kugonga ila ishu ya kuzalisha haiwezekan na haitowah kutokea..dah mchiz alidata na alifukuzwa kazi kwenye kitengo sababu alikuwa mwenye maamuz ya hasira na yeye ndiye kiongozi.