Kugombana na kubadili lugha vinahusianaje?

Kugombana na kubadili lugha vinahusianaje?

Sijaweza kuweka link yake hapa maana sijauona tena, ni uzi mdada mmoja anauza nyumba yake huko morogoro akatokea memba mmoja akamtifua dada wa watu hadi akaanza kujibizana nae kwa kiingereza, aah mie walinipa burudani tuu vile napenda kucheka hehehehhee.

Majibizano yangu na Tyta yalikuwa na vijembe tuu hakuna matusi japo lugha ilikuwa ya malkia.
Nimeuona..Ila nawe mbea teh teh
Nyumba inauzwa Morogoro

Halafu mtoa mada aliomba umtag ati..

cc swank
 
Hahahahaaa kwahiyo kiinglish kina poza ukali wa maneno sio....

Naona hata humu ukiweka matusi ya kiinglish hauli ban ila ukiweka matusi ya kizaramo weeh huchukui raundi unabanikwa fastaa hahahaha.
Yeah..Mana mpaka uende kuligoogle tusi ujue linamaanisha nini munkari unakuwa ushapungua .
 
Dhamira iliyojengeka vichwani mwetu maneno mengi ukiyaweka kwa lugha ya kiyunani yanaleta maana zaid
 
Hahahahahaha kwahiyo kwa kifupi tuseme inglish inapunguza ukali wa matusi ya kiswahili......

Ila, wakati huo huo, waliokunywa au wanywaji wa kilevi, kilevi kikishapanda kichwani huanza kuongea lugha ya kiingereza hata kama hawajasoma...... hapo napo pananipaga mshangao.....!!!

Wa matukio haya mawili mie naona mtu ukitaka kujua kiinglish kwa urahisi kasirika uwe unabishana na mtu na unywe kilevi kipande kichwani hehehheee.
[emoji23] hatari sana, kuna jamaa yangu mmoja hupenda kuiita bia ni dictionary [emoji23]
 
Wazungu wametuzunguka si mchezo, mana tumekuwa watumwa sana.
 
Ebu leta hapa huo uzi tuone kwanza walivotukanana kiingereza then mambo mengine yatafuata. Tusije kuwa tuajadili kitu hewa.
 
Kassiiieeee Matrrraaattaaaa!

Umenitungia uzi kweli jamani!

Kiukweli hata mm sijui inakuaje, yaani najikuta tuu maneno ya kiswahili hayaji yaani kuna donge linakaa rohoni hili nikitaka kulitoa kwa kiswahili halitoki

Kiingereza chenyewe si kwamba ninakijua laa huwa nagoogle tuu! So please excuse my broken English!
 
Nimeuona..Ila nawe mbea teh teh
Nyumba inauzwa Morogoro

Halafu mtoa mada aliomba umtag ati..

cc swank

Hahahahaaa wala sio mmbea hata kidogo maana kule nilisema naenda anzisha uzi, sijawateta bana sana sana yake nimejipiga taswira kumbe namie nakuwaga hivohivo hehehehehehee ndo nikapata wazo la kuleta uzi.

Nashukuru kwa kumtagi ameshafika.
 
Yeah..Mana mpaka uende kuligoogle tusi ujue linamaanisha nini munkari unakuwa ushapungua .

Hahahaha kweli kabisa, ila inglish bana yaani unajikuta tuu ulimi unateleza kama umekula bamia aahahahahaaa looh.
 
Back
Top Bottom