Kugombana na kubadili lugha vinahusianaje?

Kugombana na kubadili lugha vinahusianaje?

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,229
Habari ya jumapili na usiku mnene,

Nimepitia uzi flani humu iko kwa lugha ya kiswahili sasa baadhi ya wachangiaji wakaanza kumuuliza maswali mtoa mada na baadhi ya maswali yakaonekana kumkera mtoa mada na kushindwa kudhibiti hasira ikabidi na yeye aanze kumjibu visivyo ila akabadili lugha kutoka kiswahili wakaanza kujibizana kingereza. Na yule mchangiaji naye hakuwa nyuma aliendeleza kujibu kingereza hadi wakaagana.

Kasie napenda sana kucheka nikajikuta nacheka kila nilivokuwa nasoma majibizano yao.

Halafu nikajiuliza hivi kwanini huwa inatokea watu wakigombana saa zingine huanza kuchanganya maneno ya kiingereza au kuanza kutukana na kutumia lugha ya kiingereza tupu?

Mimi mwenyewe ni mchanga wa hiyo hali ndo maana nikacheka japo sio mara zote, kuna muda nikichukia nagomba kiswahili mwanzo mwisho. Ila kuna muda najikuta nagombana kwa kingereza utasema nimezaliwa London kumbe nimezaliwa Uyui.

Pia nimekumbuka kichaa wangu Tyta tulikuwa kila tukigombana lugha inabadilika hadi yeye anakimbia mwenyewe.

Sijui yukwapi mpiga picha yule maamuzi wa JF miaka ile. Usijekuta amesha rest in peace mie naendelea kumtaja taja hapa. Ila kama yupo na ID ingine aje tuu tuendelee kubishana kiinglish. I love it.

Nani mwingine hii hali humkuta ya kugombana na mtu akajikuta anabadili lugha toka kiswahili hadi kingereza au lugha gani nyingine?

Usiku mwema.

Kasie mambo yote.

Kasie matata.
 
Ni dhana mbovu iliyowajaa watu kuwa ukitumia lugha ya kigeni utaonekana msomi au hoja itaonekana ya maana.

Mmhh kweli...!!! Huwa inakuwa hivyo...!!???

Kumbuka wakati watu wanagombana wanakuwa katika hali ya hasira.... labda lakini yawezekana.
 
Kasie Mambo yote...

Mbona sielewi chochote...

Au ndio mambo kote kote...

Kasie Matata...

Leo umemkumbuka Tyta...

Haya mie napita...
 
Kasie Mambo yote...

Mbona sielewi chochote...

Au ndio mambo kote kote...

Kasie Matata...

Leo umemkumbuka Tyta...

Haya mie napita...

Hahahahahaa umenikumbusha safari na marashi ya Pemba looh. Sijui lini nitafika eeehhh. ......

Ukimuona huyo jamaa almaaruf Tyta mwambie Kasie anakusabahi hehehehehe.

Habari ya siku mingi rafiki, so long.... kika nikikuona nakumbuka kike kiko mie cha hot chocolate milk.

Uko mtaalam wa vina na mizani katika mashairi eeh....

Kasie Matata leo ni Kasie Mambo Yote.

Ushawahi jibizana na mtu weye? Halafu ntakuelewesha taratibu tuu.
 
Hahahahahaa umenikumbusha safari na marashi ya Pemba looh. Sijui lini nitafika eeehhh. ......

Ukimuona huyo jamaa almaaruf Tyta mwambie Kasie anakusabahi hehehehehe.

Habari ya siku mingi rafiki, so long.... kika nikikuona nakumbuka kike kiko mie cha hot chocolate milk.

Uko mtaalam wa vina na mizani katika mashairi eeh....

Kasie Matata leo ni Kasie Mambo Yote.

Ushawahi jibizana na mtu weye? Halafu ntakuelewesha taratibu tuu.
😀😀😀😀😀.

Hapana sijawahi.

Una Vituko wewe😀.

Yaani ni raha tu
 
Nini kugombana! Mie naona pia kutongoza kiinglish ni rahisi sana
Yaani hata kutukana kiinglish ni rahisi mno
Kiswahili maneno yake kwenye pande hizo yana ukakasi sana

Tafsiri motherfu.....Kwa kikwetu uone ukakasi wake,lakini wale wenzetu wanaliimba jukwaani na audience inashangilia
 
Ha ha ha ni kuchanganya lugha tuu
 
😀😀😀😀😀.

Hapana sijawahi.

Una Vituko wewe😀.

Yaani ni raha tu

Basi itabidi siku moja tugombane mie na wewe nione kama lugha inabadilika heheheee
 
Humu tutatukanana kilugha chakiingilishi hadi uzi ufutwe, maana kila mmoja atataka tuyajue madarasa yake.

Mmh inakuwaga hivyo..... kuwa ishu ni kutaka kujulikana kuwa umesoma au laah!!??? Sasa mbona isubiri wakati ukiwa na hasira na si wakati hata unatongoza au kutongozwa! !?? eehehehehehhe
 
Mi matusi ya kiinglish uwa hayaniumi sana.. Mana vingine nakuwa hata sielewi.. Ila ya kizaramo sasa..

Hahahahaaa kwahiyo kiinglish kina poza ukali wa maneno sio....

Naona hata humu ukiweka matusi ya kiinglish hauli ban ila ukiweka matusi ya kizaramo weeh huchukui raundi unabanikwa fastaa hahahaha.
 
Huo uzi ukwapi tukajifunze matusi ya kingereza?

Sijaweza kuweka link yake hapa maana sijauona tena, ni uzi mdada mmoja anauza nyumba yake huko morogoro akatokea memba mmoja akamtifua dada wa watu hadi akaanza kujibizana nae kwa kiingereza, aah mie walinipa burudani tuu vile napenda kucheka hehehehhee.

Majibizano yangu na Tyta yalikuwa na vijembe tuu hakuna matusi japo lugha ilikuwa ya malkia.
 
Nini kugombana! Mie naona pia kutongoza kiinglish ni rahisi sana
Yaani hata kutukana kiinglish ni rahisi mno
Kiswahili maneno yake kwenye pande hizo yana ukakasi sana

Tafsiri motherfu.....Kwa kikwetu uone ukakasi wake,lakini wale wenzetu wanaliimba jukwaani na audience inashangilia

Hahahahahaha kwahiyo kwa kifupi tuseme inglish inapunguza ukali wa matusi ya kiswahili......

Ila, wakati huo huo, waliokunywa au wanywaji wa kilevi, kilevi kikishapanda kichwani huanza kuongea lugha ya kiingereza hata kama hawajasoma...... hapo napo pananipaga mshangao.....!!!

Wa matukio haya mawili mie naona mtu ukitaka kujua kiinglish kwa urahisi kasirika uwe unabishana na mtu na unywe kilevi kipande kichwani hehehheee.
 
Ha ha ha ni kuchanganya lugha tuu

Hivo eeeh hakuna kingine zaidi......

Na wale wanaoanza kuzungumza kiinglish baada ya kunywa chupa kadhaa za laga inakuweje. ..??
 
Back
Top Bottom