seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,654
Kabla ya mwaka 2015 Vijana wengi walipata kazi serikalini na waliridhika kabisa na mishahara yao. Nyuma ya pazia kulikuwa ni siri kubwa zilizojificha ambazo ziliwafanya waone mishahara inatosha na kukidhi mahitaji.
Semina na Mikutano ndio chanzo kikubwa kilichowasaidia wazee wetu kusomesha na kujenga makazi ya kuishi. Lakini semina na mikutano ya wazee wa zamani ilisaidia kutatua changamoto za wakati huo
Semina na warsha ziligeuka kuwa eneo la upigaji enzi za Rais wetu mpendwa J Kikwete, Watu waligawana safari kuelekea bara ulaya, America kaskazini, Asia na Australia na pesa za semina hizi zilifanya watu walidhike na mishahara huku wakisomesha ndugu na jamaa
Spana na kishindo cha awamu ya tano maeneo kama Halmashauri za wilaya na manispaa hali imekuwa tete kwa vijana kwani mrija wa semina na warsha zimekata
Walimu wa sekondari na msingi wao maisha yao ni yale yale hawakutegemea warsha na mikutano kama taasisi zingine za Serikali
Mshahara wa mtu ni siri, Na kama ingekuwa sio siri basi taasisi zinazosemwa zinalipwa pesa nyingi utacheka sana, Ni kweli wale waliofikia level au hatua ya Ukurugenzui au Umanager wana unafuu kidogo sana
Wafanyakazi wa taasisi zinazosemwa kubwa basi watu wanaacha kazi huko na kwenda kwenye taasisi binafsi zenye mishahara mikubwa.
Watu wa taasisi zinatuhumiwa humu wanaishi kwa mikopo tu, Wamekopa kuanzia magari ya kutembelea, Nyumba na bado wanasubiri wakistaafu pension yao ikatwe kufidia mikopo ya nyumba na magari, Haya maisha yana siri kubwa sana usione watu wapo kwenye Landcruiser Vx V8 halafu ni wafanyakazi wa BOT au TRA kuna siri kubwa labda kama ni Mzee wa mangumasha, misheni town na mpiga dili hao hakuna shida
Tatizo ukiwa na gari haramu la kuzulumu watu, au nyumba umejenga haramu kwa kuzulumu watu roho huwa inauma sana sana maishani unakosa furaha kabisa, Mimi ni muhanga wa kununua kitu kwa kupiga deal hakika baada ya miaka kadhaa niliamua kukiuza kile kitu maana kila wakati roho ilinisuta kuwa nimepiga dili haramu na kuzulumu wengine
Ni kawaida kuwakuta vijana wameacha kazi BOT baada ya kupata uzoefu na kwenda CRDB ,CITi Bank au USAID kutafuta maslahi makubwa baada ya spana za awamu ya tano
Ni kawaida vijana wa TRA kukimbia kazi na kuelekea taasisi binafsi au kuamua kufanya biashara binafsi
Maneno ni mengi sana lakini ikumbukwe taasisi baadhi za serikali walijipangia wao mishahara kutokana na kuwa na uhakika wa kupata pesa
Hakuna siku mtu mshahara utamtosha maishani mwake ishu ni mpangilio na vipaumbele tu, Kuna vijana maofisini umemzidi mshahara mara 10 lakini mwisho wa mwezi ukikaribia unajikuta huna kitu lakini dogo yupo vizuri kila wakati na unamuazima pesa. Ishu hapa ni utunzaji wa fedha na hii kitu wachache wanaweza kutunza pesa labda wahindi na wakinga wana roho ngumu