KUFURU: Gharama za matibabu ya viongozi wastaafu ni BILLIONI 9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KUFURU: Gharama za matibabu ya viongozi wastaafu ni BILLIONI 9

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Jul 14, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bunge linaloendelea na kikao chake mjini Dodoma, juzi liliambiwa kwamba Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kugharamia matibabu ya viongozi wakuu wastaafu. Akihitimisha mjadala wa hotuba yake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti na Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema fedha hizo ni kwa ajili ya wastaafu wanaopaswa kutunzwa na Serikali.

  Bila kuelezea suala hilo kwa undani, Waziri Kombani alisema tu kwamba kiwango hicho kimepungua mwaka huu kutoka Sh10 bilioni zilizotengwa mwaka jana hadi Sh9 bilioni mwaka huu kutokana na idadi ya viongozi wastaafu wanaopaswa kuhudumiwa na Serikali kupungua. Wastaafu wanaoangukia katika fungu hilo ni marais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

  Mawaziri wakuu wastaafu ni Joseph Warioba, Samuel Malecela, Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim na Edward Lowasa. Waziri Kombani hakuwataja viongozi wastaafu waliopungua, lakini sote tunafahamu fika kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na Mzee Rashid Mfaume Kawawa tayari wametangulia mbele ya haki.

  Bila shaka takwimu hizo zitakuwa zimewashangaza wengi kutokana na wingi wa fedha zinazotengwa kila mwaka kugharamia tu matibabu ya viongozi, bila kutilia maanani fedha nyingine nyingi zinazotengwa kama mafao ya viongozi hao wastaafu. Kwa akili ya kawaida, fedha hizo ni nyingi mno kulinganisha na idadi ya viongozi waliokusudiwa na takwimu hizo zinaacha maswali mengi kuliko majibu.

  Tunasema hivyo kwa sababu hatuoni jinsi kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kugharamia matibabu ya idadi ndogo sana ya viongozi wetu wastaafu, kwani siyo siri pia kwamba wastaafu wetu wengi wamekuwa wakipatwa na maradhi ya kawaida ambayo siyo tu hayahitaji fedha nyingi kuyatibu, bali pia yangeweza kupata tiba hapa nchini. Ndiyo maana tunasema vifungu vikubwa vya fedha zinazotengwa kila mwaka kwa shughuli hiyo siyo tu vinatia shaka, bali pia vinaacha ukungu na kiza kinene vikiwa vimetanda.

  Sisi hatusemi kwamba viongozi wetu hao wastaafu hawastahili kupata matibabu kwa kodi zetu. Tunachosema hapa ni kwamba gharama za matibabu yao hazipaswi kuwa siri au kuacha shaka hata kama wastaafu hao walitutumikia vizuri wakati wa utawala wao. Ni sahihi kabisa kwamba walipakodi wangetaka kujua kodi zao zinavyotumika kuwagharimia viongozi wao.

  Bado tunasisitiza kwamba Sh9 billioni kwa matibabu ya viongozi hao wastaafu siyo tu ni nyingi mno, bali pia ni kufuru na za kufikirika. Takwimu hizo hazijumliki hata kidogo. Ni matibabu yapi yenye gharama hata robo ya kiasi hicho kilichotengwa, hata ukiweka usafiri, malazi na gharama nyingine? Ni kichekesho kwamba fedha hizo zimepitishwa na Bunge.  Source : Mwananchi
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,840
  Trophy Points: 280
  serikali imeshika mpini
   
 3. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah kaka umeesomeka lkn kuna pahala unatuchanganya heading yako watuambia ni Bil.9 alafu ndani unakuja kusema Tril. 9 sasa tushike lipi?
  Na ktk hao wastaafu umesahau kumuweka Mama Maria Nyerere naye yupo kwenye kundi hilo kwa heshma yake kama Mama wa Taifa hili ana hilo rungu na ndio maana hadi leo Utumishi wana mhudumia yule Mama kwa kila kitu ambacho alipaswa Hayati Mwl JKN akipate anakipata yule Mama"
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Jamani kwa nchi zetu masikini muda wa rais kuwa madarakani ungeongezwa kutoka miaka 10 hadi 20.vinginevyo tutakua na utitiri wa viongozi wastaafu vijana wa kuwahudumia
   
 5. L

  Luluka JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dah!kweli nchi inaliwa na wakubwa tu!
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hapo napo ni kichaka cha wezi!! Lol
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  wangeboresha muhimbili hizo hela zinatisha kununua vifaa tiba.....
   
 8. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi namfahamu mwanajeshi mmoja alikuwa na cheo hivi...yaani yeye mpaka na mke wake huwa wanapelekwa India kwa matibabu...! chezea viongozi wenye akili ndogo weye...
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hivi mzee Jumbe haingii kwenye kundi hili?
   
 10. a

  augustino ameri JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo ndiyo bongo ,NDIO MAANA VIONGOZI WETU WAMEGOMA KUTATUA MGOMO WA MADAKTARI.WANABAJETI ZA KODI ZA KUTIBIWA NJE KUANZIA MAFUA HADI KUPASULIWA.MANAENDA NJE WANAJUA HAPA HAKUNA VIFAA,MSANII SAJUKI ALIKUWA ANASUBIRIA MAUPI,DR.ULIMBOKA KAKIMBIZWA SAUZ,DR,MWAKYEMBE INDIA NA WENGINEO.MADAKITARI BINGWA TUNAO TATIZO VIFAA ,VINGEKUWA MAGARI,RISASI,MWENGE,BUNDUKI AU UCHAGUZI PESA ISINGEKUWA TATIZO.FIKIRIA MAGARI YA KIFAHARI YA SERIKALI NUSU YAKE TU VINGEKUWA VIFAA,MPAKA HOSPITALI ZA KATA ZINGEFANYA UPASUAJI.
   
 11. D

  Doreen22 JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 475
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo hizo bil. 10 za mwaka jana ziliisha zote au, zikibaki inakuwaje, eeh, hizi ni hela za kutibu watu au mitambo, viongozi gani wa kubwa na wangapi mwaka jana, ulisikia wanaumwa seriously, au wakifa ghafla huwa zinatumika kwa mazishi pia, hivi kweli hawa watu hawajiwezi katika kujigharamia matibabu yao madogo madogo ya hospitali, hata watoto wao wanaweza kuwasaidia kwenye ugonjwa mdogo mdogo, hizo fedha zikasaidia wale wasiojiweza kwelikweli, Ocean Road na kwingineko
   
 12. B

  Bijou JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Swali la kujiuliza, bajeti iliyowekwa KWA ajili ya watanzania MILIONI 40, dhidi ya VIONGOZI wastaafu 8, eh Mungu uliye mwingi wa rehma legeza mioyo ya wote, Maono yaelekezwe KWA watanzania wAlio wengi, Ameeeeeeeeeeeeeeeeen!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Kumbakumba

  Kumbakumba JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtuonee huruma jaman,mtatutoa damu
   
 14. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,063
  Trophy Points: 280
  Swali zuri Doreen22 maana kuugua ni tofauti na kuchimba visima yaani kama umepanga kujimba visima 2000 kwa kiasi flani lazima uchimbe na ela iliyotengwa inaweza kuisha au kuzidi lakini kwenye kuugua inategemea maana si wote wanaweza kuugua na tunategemea ela inaweza kubaki japokuwa kwa nchi yetu kwa kuwa budget imepangwa utaona mtu anajilazimisha kuitumia ela (au swali la kuuliza lingine hizo ela wanapewa kama allowance au nini maana kitendo cha kupunguza toka 10 bilion to 9 bilion inaonyesha kama wanapewa directly as allowance, kama ni hivyo nadhani itabidi tuwakatie BIMA YA AFYA
   
 15. M

  Mkuki JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 363
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mmmmmmmh
   
Loading...