Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,738
- 7,110
Kwanza nitamke kuwa nimesikitishwa sana na tukio la kuuawa kwa askari polisi wetu wanane huko mkoa wa Pwani. Niwatakie familia zao faraja itokayo kwa Mungu katika mapito haya ambayo sii mepesi.
Nikirudi kwenye mada, Ninasikitishwa na watanzania wenzangu wanaofurahia kutokea kwa tukio hilo. Wengi wanadai kuwa *wanafurahia* kwa sababu ya utendaji wa Polisi m'bovu na unaowakandamiza wananchi.
Mimi ninajiuliza, kama askari polisi amekutendea ndivyo sivyo, kwa mfano amekudai rushwa, kwanini usichukue hatua za kum'bana kwa kushirikiana na Taasisi yetu ya TAKUKURU ili muandae mtego na kumtia hatiani????
Au kama amekubambikiza kesi, kwanini usitoe malalamiko yako kwa kueleza jinsi alivyokubambikizia hio kesi kwa kufuata uongozi wake kwa mfano: askari akikubambikiza kesi unaweza ukafuata mlolongo huu kudai haki yako:
Nenda kwa mkuu wa kituo (OCS) asipokusaidia nenda kwa OC-CID, Naye asipokusaidia nenda kwa OCD, ikishindikana nenda kwa RPC, ... Endelea hivyo hivyo hadi utakapoipata haki yako (kumbuka haki hudaiwa, haki haiombwi). Usiruhusu kulichukia jeshi lote kwa sababu ya uovu wa mtu mmoja.
Sasa kutokana na chuki zako unafurahia kuuawa kwa askari na kuchukuliwa kwa silaha! Hujui hizo silaha zimeingia kwenye mikono ya wahalifu ambao kesho na keshokutwa watakuja kukudhuru nazo wewe?
Kamwe usiruhusu hali ya kuyafurahia matatizo ya wengine kwa sababu -ukifanya hivyo NI USHETANI.