KUFUNGWA KWA BUREAU DE CHANGE ZANZIBAR

Jagina

Member
Jan 29, 2019
71
125
Mimi mpaka hivi sasa linaniuma suala la kufungiwa Bureau de changes hasa hizi za hapa Zanzibar. Bado nina masuali lukuki najiuliza kichwani mwangu ambayo siyapatii majibu.

Kila nikichunguza Zanzibar itanufaika vipi na ufungaji wa hizi Bureaux de change, sipati jawabu. Ina maana leo hii Serikali ya Muungano inataka dola zinazopatikana Zanzibar kutoka sekta ya utalii ambayo kimsingi si ya Muungano wazidhibiti wao kupitia Bureau de change yao ya posta?

Kwa tuliosoma utalii hili ni kinyume na matakwa ya utalii endelevu, na ni kinyume na Sera yetu ya Zanzibar ya Utalii kwa wote. Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzíbar ina Sera nzuri ya Utalii kwa wote, sasa ikiwa mjasiriamali wa Bureaux de change anafungiwa duka lake maana yake yeye hatofaidika tena na mapato ya utalii. Katika hali hii ni sawa na kusema kwamba utalii wa Zanzibar hautomnufaisha tena mfanyabiashara huyu? Sasa je hatuoni kwamba tunapingana na Sera yetu ya utalii kwa wote!

Katika Utalii kuna kitu kinaitwa Tourism Leakage. Wataalamu wanaitafsiri “Leakage” kama ni kitu chochote kinachopelekea mapato ya utalii ya nchi moja kutoka nje ya mfumo wa kiuchumi wa nchi husika. Ni wazi kwamba uchumi si suala la Muungano, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na chumi mbili tafauti. Sasa je dola inayopatikana Zanzibar kutokana na utalii sekta ambayo kimsingi si ya muungano ikitolewa nje ya mzunguko wa fedha na uchumi wa Zanzibar itaitwaje kama si Leakage hiyo.

Kwa ufupi, katika takwa moja la utalii endelevu ( sustainable tourism) ni kuajiri jamii inayozunguka utalii wenyewe (surrounding community) ili nayo inufaike na shughuli na mapato ya utalii. Sasa hatuoni kwamba kuzifunga bureau de changes za Zanzibar ambazo kimsingi zinamilikiwa na jamii ya kizanzibari ambao walipaswa kufaidika na utalii wa Zanzibar kwa njia moja ama nyengine na kuifuisha bureau de change ya posta ambayo si milki ya jamii ya Kizanzibari si ni kwenda kinyume na Sera yetu utalii kwa wote tu bali pia ni kwenda kinyume na matakwa ya utalii endelevu? Maana yake dola inayotokana na utalii wa Zanzibar kwa mfumo wa sasa itakwenda kuwanufaisha watu walio nje ya Zanzibar badala ya hawa Wazanzibari walio humu ndani.

Mwisho labda nitowe rai kwa Serikali yetu tunayoipenda ya Zanzíbar na kuitanabahisha kwamba si kila sera inayotungwa na Tanganyika ina maslaha na Zanzibar. Mazingira ya kiuchumi ya Zanzibar ni tafauti sana na mazingira ya kiuchumi ya Bara. Basi ifike wakati kila nchi iwe na sera zake za kifedha ( fiscal and monetary policies) pamoja na kuwa na central banks zake ili kila mmoja apange uchumi wake kwa mazingira ya nchi yake.
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,482
2,000
Hivi exchange rate ya huko na huku huwa ziko sawa?
Kama ni tofauti basi kila mtu ale anavyotaka

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,505
2,000
Suala la currency Ni la Muungano hivyo Kufungiwa Maduka ya kubadikishiwa Fedha Rais wa Znz Hana Cha kufanya wala kuamua Yeye Ni Mpenzi mtazamaji Kama Mimi Na Wewe

Zamani enzi Za Mzee Kambarage ilikuwa ili ubadili Fedha zako lazima upate Kibali Cha Governor

Vijana mliokuwa mnamsoma Kambarage Kwenye Vitabu sasa Na nyinyi onjeni 'asali' tulioishi nayo kwa 23 years

Mkiona nyakati zingine tunamkosoa Mjue tuliumia

Nanyi mtakapokuwa mnaona watu wanasoma Kwenye vitabu kuhusu awamu ya Tano mtakuwa mnakosoa Na vizazi hivyo havitowaelewa
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,806

Nyakati zinafanana??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,505
2,000
Nyakati zinafanana??

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyakati hazifanani ila Kinafiki mlikuwa mnalilia Azimio la Arusha lililofutwa Na Wazee wenye busara 1992 Mkawa hamkumbuki hiyo hoja ya 'nyakati'

Sasa limerudi Na Kama mlikuwa mnalililia kinafki Kwenye midahalo Sasa hivi mnakula Matunda ya Kinafki

Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa 'kukata' Mirija ya 'kinyonyaji'

Unaijua Mirija hiyo?

Kama huijui sema nikupe Darsa fupi mujjarab kwa bundle yako ya Mia Tano tu?
 
AVRAM

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
564
1,000
Mimi mpaka hivi sasa linaniuma suala la kufungiwa Bureau de changes hasa hizi za hapa Zanzibar. Bado nina masuali lukuki najiuliza kichwani mwangu ambayo siyapatii majibu.

Kila nikichunguza Zanzibar itanufaika vipi na ufungaji wa hizi Bureaux de change, sipati jawabu. Ina maana leo hii Serikali ya Muungano inataka dola zinazopatikana Zanzibar kutoka sekta ya utalii ambayo kimsingi si ya Muungano wazidhibiti wao kupitia Bureau de change yao ya posta?

Kwa tuliosoma utalii hili ni kinyume na matakwa ya utalii endelevu, na ni kinyume na Sera yetu ya Zanzibar ya Utalii kwa wote. Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzíbar ina Sera nzuri ya Utalii kwa wote, sasa ikiwa mjasiriamali wa Bureaux de change anafungiwa duka lake maana yake yeye hatofaidika tena na mapato ya utalii. Katika hali hii ni sawa na kusema kwamba utalii wa Zanzibar hautomnufaisha tena mfanyabiashara huyu? Sasa je hatuoni kwamba tunapingana na Sera yetu ya utalii kwa wote!

Katika Utalii kuna kitu kinaitwa Tourism Leakage. Wataalamu wanaitafsiri “Leakage” kama ni kitu chochote kinachopelekea mapato ya utalii ya nchi moja kutoka nje ya mfumo wa kiuchumi wa nchi husika. Ni wazi kwamba uchumi si suala la Muungano, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na chumi mbili tafauti. Sasa je dola inayopatikana Zanzibar kutokana na utalii sekta ambayo kimsingi si ya muungano ikitolewa nje ya mzunguko wa fedha na uchumi wa Zanzibar itaitwaje kama si Leakage hiyo.

Kwa ufupi, katika takwa moja la utalii endelevu ( sustainable tourism) ni kuajiri jamii inayozunguka utalii wenyewe (surrounding community) ili nayo inufaike na shughuli na mapato ya utalii. Sasa hatuoni kwamba kuzifunga bureau de changes za Zanzibar ambazo kimsingi zinamilikiwa na jamii ya kizanzibari ambao walipaswa kufaidika na utalii wa Zanzibar kwa njia moja ama nyengine na kuifuisha bureau de change ya posta ambayo si milki ya jamii ya Kizanzibari si ni kwenda kinyume na Sera yetu utalii kwa wote tu bali pia ni kwenda kinyume na matakwa ya utalii endelevu? Maana yake dola inayotokana na utalii wa Zanzibar kwa mfumo wa sasa itakwenda kuwanufaisha watu walio nje ya Zanzibar badala ya hawa Wazanzibari walio humu ndani.

Mwisho labda nitowe rai kwa Serikali yetu tunayoipenda ya Zanzíbar na kuitanabahisha kwamba si kila sera inayotungwa na Tanganyika ina maslaha na Zanzibar. Mazingira ya kiuchumi ya Zanzibar ni tafauti sana na mazingira ya kiuchumi ya Bara. Basi ifike wakati kila nchi iwe na sera zake za kifedha ( fiscal and monetary policies) pamoja na kuwa na central banks zake ili kila mmoja apange uchumi wake kwa mazingira ya nchi yake.
Mtu mweupe umesema sahihi sana, na kiukweli utashangaa sana SMZ wanafuata na kuiga kila kitu kinachofanyika Tanganyika, ila hivi wanavyoiga ni vile vibaya na vyenye kurejesha nyuma waru na nchi kwa ujumla, hawa SMZ hawaigi kujenga miundombinu mizuri na imara wataiga vitu visivyo na macho wala miguu ambavyo haviwahusu ndewe wala sikio.
Wanaudhii ghaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,305
2,000
Mimi mpaka hivi sasa linaniuma suala la kufungiwa Bureau de changes hasa hizi za hapa Zanzibar. Bado nina masuali lukuki najiuliza kichwani mwangu ambayo siyapatii majibu.

Kila nikichunguza Zanzibar itanufaika vipi na ufungaji wa hizi Bureaux de change, sipati jawabu. Ina maana leo hii Serikali ya Muungano inataka dola zinazopatikana Zanzibar kutoka sekta ya utalii ambayo kimsingi si ya Muungano wazidhibiti wao kupitia Bureau de change yao ya posta?

Kwa tuliosoma utalii hili ni kinyume na matakwa ya utalii endelevu, na ni kinyume na Sera yetu ya Zanzibar ya Utalii kwa wote. Serikali yetu ya Mapinduzi ya Zanzíbar ina Sera nzuri ya Utalii kwa wote, sasa ikiwa mjasiriamali wa Bureaux de change anafungiwa duka lake maana yake yeye hatofaidika tena na mapato ya utalii. Katika hali hii ni sawa na kusema kwamba utalii wa Zanzibar hautomnufaisha tena mfanyabiashara huyu? Sasa je hatuoni kwamba tunapingana na Sera yetu ya utalii kwa wote!

Katika Utalii kuna kitu kinaitwa Tourism Leakage. Wataalamu wanaitafsiri “Leakage” kama ni kitu chochote kinachopelekea mapato ya utalii ya nchi moja kutoka nje ya mfumo wa kiuchumi wa nchi husika. Ni wazi kwamba uchumi si suala la Muungano, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na chumi mbili tafauti. Sasa je dola inayopatikana Zanzibar kutokana na utalii sekta ambayo kimsingi si ya muungano ikitolewa nje ya mzunguko wa fedha na uchumi wa Zanzibar itaitwaje kama si Leakage hiyo.

Kwa ufupi, katika takwa moja la utalii endelevu ( sustainable tourism) ni kuajiri jamii inayozunguka utalii wenyewe (surrounding community) ili nayo inufaike na shughuli na mapato ya utalii. Sasa hatuoni kwamba kuzifunga bureau de changes za Zanzibar ambazo kimsingi zinamilikiwa na jamii ya kizanzibari ambao walipaswa kufaidika na utalii wa Zanzibar kwa njia moja ama nyengine na kuifuisha bureau de change ya posta ambayo si milki ya jamii ya Kizanzibari si ni kwenda kinyume na Sera yetu utalii kwa wote tu bali pia ni kwenda kinyume na matakwa ya utalii endelevu? Maana yake dola inayotokana na utalii wa Zanzibar kwa mfumo wa sasa itakwenda kuwanufaisha watu walio nje ya Zanzibar badala ya hawa Wazanzibari walio humu ndani.

Mwisho labda nitowe rai kwa Serikali yetu tunayoipenda ya Zanzíbar na kuitanabahisha kwamba si kila sera inayotungwa na Tanganyika ina maslaha na Zanzibar. Mazingira ya kiuchumi ya Zanzibar ni tafauti sana na mazingira ya kiuchumi ya Bara. Basi ifike wakati kila nchi iwe na sera zake za kifedha ( fiscal and monetary policies) pamoja na kuwa na central banks zake ili kila mmoja apange uchumi wake kwa mazingira ya nchi yake.
Gomesheni kuburuzwa wazenji sio wabara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nsanzu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,901
2,000
Imebakia tu mtu mmoja kusimama aseme, "Kesho wote nchi nzima mvae pensi bila mashati wala tisheti"
 
kimondo msolopa

Senior Member
Feb 18, 2011
164
250
Ndugu yangu usilalamike sana hata Arusha na Dar zimefungwa nchi inayoanguka kiuchumi inafikiri kufunga bureau de change itashusha rate ya dola kumbe inaharibu kila kitu sasa ujue kwamba nchi iko malaha pabaya...!! haijawahi kutokea karibuni kufungwa kwa bureau de change kila sehemu ...nchi export imeshuka sana wanalazimisha bank kwasababu inatoa rate za kuumiza wananchi mfano NMB wananunua dola kwa 2280 wanauza kwa 2395 kama kweli bureau de change zinapandisha rates kwanini bank inunue kwa 2280 iuze kwa 2395? kama dola ingekuwa stable bank ingenunuliwa kwa 2270 iuzwe kwa 2280 au 2290 tungesema sawa. Bureau de change walikua fair kwasababu Dar ilikua kununua 2370 kuuza 2395... ndugu yangu anguko la uchumi limeifika nchi hii kilichobaki ni ubabe ambao hautasaidia taifa!! Wame fail completely! Hizo bank wangekuwa fair wangenunua 2270 wauze 2290 tungejua bureau zina shida lakini wanaibia wananchi wao wanauza kwa 2395 ndio ujue ukweli uko wapi!! Nani mwizi na ujue status ya uchumi wa nchi uko vipi... wasiojua wanacheeeeka eti tuko kwenye right track!! Mjomba life is not rehearsal is perfomance
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
20,193
2,000
Nyakati hazifanani ila Kinafiki mlikuwa mnalilia Azimio la Arusha lililofutwa Na Wazee wenye busara 1992 Mkawa hamkumbuki hiyo hoja ya 'nyakati'

Sasa limerudi Na Kama mlikuwa mnalililia kinafki Kwenye midahalo Sasa hivi mnakula Matunda ya Kinafki

Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa 'kukata' Mirija ya 'kinyonyaji'

Unaijua Mirija hiyo?

Kama huijui sema nikupe Darsa fupi mujjarab kwa bundle yako ya Mia Tano tu?
Huyu sasa ndiye Pohamba ninayemjua siyo yule aliyedai maji ni anasa.

Mi naomba uniambie, kwa mtazamo wako unadhani awamu hii inatumia vigezo vya nyakati zilizopita kuamua upi ni mrija wa kinyonyaji na upi siyo?

Inasaidia lolote?
 
platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
8,806
2,000
Nyakati hazifanani ila Kinafiki mlikuwa mnalilia Azimio la Arusha lililofutwa Na Wazee wenye busara 1992 Mkawa hamkumbuki hiyo hoja ya 'nyakati'

Sasa limerudi Na Kama mlikuwa mnalililia kinafki Kwenye midahalo Sasa hivi mnakula Matunda ya Kinafki

Msingi wa Azimio la Arusha ilikuwa 'kukata' Mirija ya 'kinyonyaji'

Unaijua Mirija hiyo?

Kama huijui sema nikupe Darsa fupi mujjarab kwa bundle yako ya Mia Tano tu?
Mimi si wa kupewa darsa.
Nimeuliza kuhusu nyakati, kwa hakika haya 'mambo' tunayoyaona hayafanani na yale ya 'azimio'. Leo hata kama Kiwanda kikizuiwa (kwa mujibu wa sheria) kuzalisha bidhaa fulani kwa sababu ya kukiuka masharti kadhaa habari zitakuwa nyingi sana, kwa maana ya hii habari ya social media

Kesho kutwa napita hapo, tukutane Libya street tunywe gahwa wakati tukinangana kuhusu mechi ijayo ya Simba!

Ila wewe unazeeka vizuri, habari za Diamond umo, Ruge umo, Masha'Allah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,496
2,000
Kwani benki huko Zanzibar hawabidilishi fedha?

Si hivyo,Zanzibar haina Benki Kuu isipokuwa kati ya mabenki yanayofanya kazi ipo Benki inayomilikiwa na Serikali ya Zanzibar.

Benki hiyo imekuwa ikitaka kubinafsishwa lakini BENKI KUU imekuwa ikiweka vizingi kwa kutaka wawekezaji wapite kwao na kudeposite fedha kwao ili ziende kwa Benki ya Watu wa Zanzibar.

Tumekuwa tukidanganywa mengi juu ya Zanzibar lakini ukweli umekuwa ukifichuka taratibu.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,268
2,000
Hivi hujuwi kuwa Zanzibar ni kimkoa chetu? Kwani huko Zanzibar mna sarafu yenu ya pekee?

Mtafata tunayoyataka sisi mkitaka msitake. Mapinduzi daima.
 
Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
28,496
2,000
Hivi hujuwi kuwa Zanzibar ni kimkoa chetu? Kwani huko Zanzibar mna sarafu yenu ya pekee?

Mtafata tunayoyataka sisi mkitaka msitake. Mapinduzi daima.

Viongozi wa Zanzibar ma CCM hayaambiliki kwa Bara .Ni mijoga katika kulinda mitumbo Yao.
Washapewa ardhi Dodoma wakajenge wizara zao.
Washaombwa wafanye serikali moja.
Wabara hawaulizwi wanapokuja kufanya makaazi Zanzlbar.
Sasa takriban Zanzibar ina watu millioni mbili Hapa mtu wa bara ana hadhi zaidi kuliko Mzenji

Mkuu wa Wilaya Mjini aitwa Marina joseph,

Kamanda Polisi Mkoa Mjini Magharib aitwa Tobias,

Waziri Wanawake nà watoto aitwa Modelina Kastiko.

Juzi kulifanyika mabadiliko ya maafisa wa juu polisi na kuletwa wabara hapa.

Zaidi ya 90% ya wanajeshi ni wabara.

Hawa hawaambiliki!!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom