Kufungiwa kwa JamiiForums Tanzania: Salaam za shukrani na mwelekeo...

Nichukue nafasi hii, kujibu kwa heshima na taadhima, asante sana! hatuwezi kuacha kuingia humu kila siku hata watufunge mikono, nasema haiwezekani.
 
Wakati nasoma kichwa cha habari nimeona kama kufunguliwa kwa jamii forums, nimesoma kwa bashasha kumbe bado tupo kifungoni.

naungana nao walio kupa pole mkuu Maxence Melo ,pongezi, kutia moyo , na kujaribu kusaidi.
Mimi nakupongeza sana kule kutii kwako , ni ukomavu mkubwa sana
Ungeweza kwenda mahakamani kwa vile una hoja yenye mashiko ya kujitetea na ushindi ungepatika ila uliamua kutii.

Siku 90 si nyingi na wala si chache ila zi simalizike kwa kukosa la kujifunza na kufahamu namna ya kuenenda na mamlaka za kiserikali.

Nadhani mwakani ni maadhimisho ya mwaka wa 20 wa kuanzishwa jukwaa hili , hivyo pamoja na mengi sana uliyo pitia mpaka hapa hili nali liingine katika somo la kujifunza.

Kiujumla tulio nyuma yako ni wengi mno, si kila mmoja wetu anaweza kufanya cha mno ila ile uwepo wake unatia nguvu kwamba changu hiki nyuma yake kina ungwa mkono na wengi kuliko wanao piga vita.

Hio ikutieni nguvu, uvumilivu ama subira , uweledi na umakini kesho ikawe bora kuliko jana.

Kule Instagram kwenye ukurasa wako nilitoa maoni kwamba wakati historia ikiandikwa kuwatambua mashujaa wa ukombozi wa pili wa taifa hilo jina lako litakuwa nafasi za mwanzoni.

Bravo brother.
 
Naunga mkono hisia hizi hapa; ila nimefadhaishwa kidogo na baadhi ya yaliyomo kwenye andiko huko juu.
Ungeweza kwenda mahakamani kwa vile una hoja yenye mashiko ya kujitetea na ushindi ungepatika ila uliamua kutii.

Siku 90 si nyingi na wala si chache ila zi malizike kwa kukosa la kujifunza na kufahamu namna ya kuenenda na mamlaka za kiserikali.
Sikuelewa ulikuwa na maana gani katika mistari yako hii miwili.
 
Kati ya Septemba 5 -7 2025, JamiiForums ilipita changamoto mbalimbali huku Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikisitisha leseni ya utoaji maudhui nchini humo kupitia Jukwaa la JamiiForums kwa siku 90.

Baada ya matukio haya, wadau wengi wamewasiliana nasi kwa njia mbalimbali wakitaka kuelewa hali yetu na kama kuna namna tungehitaji msaada wa aina yoyote. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wote waliotumia muda wao kuwasiliana nasi, kupaza sauti kwa niaba yetu, na kuonesha kwa namna moja au nyingine kuwa wapo pamoja nasi na kuonyesha wazi kutofurahishwa na kilichotokea.

Tunathamini sana umoja na mshikamano mliotuonyesha. Natambua kuwa bado kuna ambao sijajibu ujumbe au kuwarudishia salamu zao, si kwa makusudi; napenda kuwafahamisha kuwa salamu zilikuwa nyingi, lakini ninaendelea kujibu kadri ninavyoweza.

Kipekee, tunawashukuru wadau wa Asasi mbalimbali za Kiraia, Sekta Binafsi, Vyombo vya Habari walioonyesha ushirikiano mkubwa kwetu

Sasa, wengine walitaka kujua WHAT’S NEXT. Niseme, kwa wateja wetu walio Tanzania, jukwaa halipatikani tokana na mamlaka kututaka kufanya hivyo. Jitihada za kuhakikisha huduma zinarejea kawaida zinaendelea.

Kwa wateja wetu wa nchi jirani (Rwanda, Uganda & Kenya) na kwingine duniani, tunaenda kuboresha na kutanua wigo zaidi kwa kuongeza huduma/bidhaa mpya ambazo zitazinduliwa kivi karibuni zikilenga kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kukidhi kiu yenu.

Yajayo yanafurahisha 😎
Uache sasa uchawa mambo ya kufuta nyuzi tu kisa yametajwa majina flani flani, tunakuwa tunafikiri na wewe umefika bei kama mwamba tuvushe
 
20250730_203222.jpg
 
Naunga mkono hisia hizi hapa; ila nimefadhaishwa kidogo na baadhi ya yaliyomo kwenye andiko huko juu.

Sikuelewa ulikuwa na maana gani katika mistari yako hii miwili.
Maana yangu, siku ile alipo letewa barua ya kusitisha huduma na sababu zile walizotoa wenye barua ile angaeweza kwenda mahakamani kuweka zuio na angeweza kufanikiwa kwa sababu sababu zile zilikuwa zinajibika ila aliamua kutii moja kwa moja pamoja na kwamba jana yake ofisi yake ilivamiwa.
 
Kati ya Septemba 5 -7 2025, JamiiForums ilipita changamoto mbalimbali huku Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikisitisha leseni ya utoaji maudhui nchini humo kupitia Jukwaa la JamiiForums kwa siku 90.

Baada ya matukio haya, wadau wengi wamewasiliana nasi kwa njia mbalimbali wakitaka kuelewa hali yetu na kama kuna namna tungehitaji msaada wa aina yoyote. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wote waliotumia muda wao kuwasiliana nasi, kupaza sauti kwa niaba yetu, na kuonesha kwa namna moja au nyingine kuwa wapo pamoja nasi na kuonyesha wazi kutofurahishwa na kilichotokea.

Tunathamini sana umoja na mshikamano mliotuonyesha. Natambua kuwa bado kuna ambao sijajibu ujumbe au kuwarudishia salamu zao, si kwa makusudi; napenda kuwafahamisha kuwa salamu zilikuwa nyingi, lakini ninaendelea kujibu kadri ninavyoweza.

Kipekee, tunawashukuru wadau wa Asasi mbalimbali za Kiraia, Sekta Binafsi, Vyombo vya Habari walioonyesha ushirikiano mkubwa kwetu

Sasa, wengine walitaka kujua WHAT’S NEXT. Niseme, kwa wateja wetu walio Tanzania, jukwaa halipatikani tokana na mamlaka kututaka kufanya hivyo. Jitihada za kuhakikisha huduma zinarejea kawaida zinaendelea.

Kwa wateja wetu wa nchi jirani (Rwanda, Uganda & Kenya) na kwingine duniani, tunaenda kuboresha na kutanua wigo zaidi kwa kuongeza huduma/bidhaa mpya ambazo zitazinduliwa kivi karibuni zikilenga kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kukidhi kiu yenu.

Yajayo yanafurahisha 😎
Bila kusahau sisi wa Malawi Bado tunapatika 😆
 
Kongole kwa kuendelea kuipigania haki ya uhuru wa kutoa maoni.

Kwa mara ya kwanza imenibidi ninunue android phone, nikanunua VPN kwa ajili ya kuipata JF.
Mkuu Maxence Melo mpe na huyu mkongwe platinum membership kisha na mimi usinisahau kwenye ufalme wako kwa kumrefer nikireport kutokea hapa Astana, kazakhstan.
 
hawa jamaa mpm kuna SITE kadhaa za VPN wamezofungia pia
yaan ile unataka kudownload VPN unakuta nayo wamepita nayo
Almost site nyingi za VPN za uhakika ambazo hazipo PRAYSTORE wamezopiga pini
ni wajinga fulani fulani
 
Back
Top Bottom