KUFUNGA NDOA

KUFUNGA NDOA

Habari za saa hizi ndugu zangu.

Napenda niwape ushauri vijana wenzangu kabla hujakubali kuishi na mtu mpaka kufikia kuzaa nae ni vyema mkafunga ndoa kabisa kwa maana itawasaidia kupata baraka katika mahusiano yenu.
Pia inasaidia kwa upande wa watoto wenu pia.
Ni hayo tu.Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa wale waliopo chuo unakuta wamepanga chumba kimoja unawashaurije

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shirikisha ubongo kidogo
Hivi unapoishi na mtu ukiwa na hicho ulichonacho kutakuwa na tofauti gani ya matumizi mkifunga ndoa?!
Kwamba mnavyoishi pamoja mnatumia 10,000
Mkifunga ndoa mtatumia 20,000??


Sent using Jamii Forums mobile app
hivi unatambua kabla ya kufunga ndoa kuna gharama inabidi zilipwe? vifuatavyo lazima vitimizwe kabla ya kufunga ndoa;

  1. fikilia mahali lazima ilipwe japo nusu, mfano ng'ombe nane! chukulia ndama mmoja @250,000/=
  2. mkaja Wa mama; mfano 100,000/=
  3. kitenge cha shangazi 30,000/=
  4. mbuzi Wa mjomba 80,000/=
  5. debe la asali ya 100,000/=
  6. sweta la babu 20,000/=
  7. doro la bibi 100,000/=
  8. Namsaza- kuku mwenye vigaranga - 30000/=
  9. kanzu moja
  10. sanduku la biharusi
HAPO HUJAWEKA GHARAMA ZA USAFILI SIKU YA NDOA HATA KAMA MTATUMIA BODABODA, NI VIJANA WANGAP WATAMUDU HIYO? HALAFU WAKATI UKIANDAA JIBU TAMBUA NYEGE HAZISUBILI, Tunawalaumu Bure vijana
 
Hivi dhambi mnaiona hiyo tu ya kuishi na MTU bila ndoa? Acheni hizo mambo bhana.

Naunga mkono hoja ya watu kuishi na kuzaa kwanza kabla ya ndoa. Maana unaweza funga ndoa na bi dada aliyetoa mimba kama zote halafu kwenye ndoa akawa hazai

Sasa nani kasema tumeona dhambi hiyo tu?

Endelea kuunga mkono hoja unayoona kwako ya msingi...halafu sio kila mwanamke asiye na uwezo wa kuzaa ni alishawahi kutoa mimba usikariri
Process ya kutunga mimba inahusisha mwanaume pia
 
Mpaka mnaishi na kuzaa kipato kinakosekana?


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mim kwa upeo wangu mkisha pendana mmemaliza kila kitu sio lazima mpak sijui harus ni kumaliza tu pesa afu mbona wazaz wetu walipendana tu hakuna ndoa Wala nn mpak Leo wanaishi ni makubaliano tu na kujua neno samani akikosea ova
 
Habari za saa hizi ndugu zangu.

Napenda niwape ushauri vijana wenzangu kabla hujakubali kuishi na mtu mpaka kufikia kuzaa nae ni vyema mkafunga ndoa kabisa kwa maana itawasaidia kupata baraka katika mahusiano yenu.
Pia inasaidia kwa upande wa watoto wenu pia.
Ni hayo tu.Shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hio kampuni LDA inajushughulisha na masuala ya ndoa?
 
Yupi bora kati ya hawa???

1. Aliyezaa pasipo ndoa lakini anaishi vizuri na mwenza wake bila shida??
2. Aliyetoa mimba kadhaa ili asubiri ndoa ndipo azae??
3. Aliyepo ndani ya ndoa lakini ana michepuko na watoto kadhaa nje??
 
Formula ya mahusiano ipo, kwavile hatuifuati ndio tunajipa moyo kuwa hakuna formula. Na hii ni kwasababu tunataka kujiridhisha na kuhalalisha njia zetu zisizofaa ambazo ndio zimeleta matatizo yote haya.

Tena kwa kuonyesha ushindi kwa shetani tunatumia ndoa zilizoshindwa kama mfano ili kuhalalisha mfumo huu mbovu wa kuzaa zaa hovyo mwisho wa siku tunakuwa na Taifa la hovyo hovyo lisilo na misingi.

Tufuate utaratibu,tuwalee watoto wetu katika ndoa halali kwa upendo, tuishi kwa misingi then tuone kama kutakuwa na shida.
Siku hizi wanaume Kuzaa na michepuko ni kama fashen, then anarudi kwa mkewe kuomba radhi Ila wengine wanaonesha ubabe kiasi kwamba ndoa haina thamani tena. Kuzaazaa hovyo sio tu kwa wasio na ndoa hata walio na ndoa vimwanaharamu kibao
 
Yupi bora kati ya hawa???

1. Aliyezaa pasipo ndoa lakini anaishi vizuri na mwenza wake bila shida??
2. Aliyetoa mimba kadhaa ili asubiri ndoa ndipo azae??
3. Aliyepo ndani ya ndoa lakini ana michepuko na watoto kadhaa nje??
Nambari moja. Ndoa ya usaliti haina maana kabisa...
 
Back
Top Bottom